Ndoa imeingia doa. Msaada wa mawazo unahitajika sana

Thomas10

JF-Expert Member
Mar 9, 2017
841
2,268
Habarini!

Ndoa ya ndugu yangu wa damu (kaka) imeingiliwa na kirusi hatarishi, maji yamezidi unga. Alimuoa binti (mke wake) kigori kabisa, na kwa utamaduni wetu, hili huwa tukio la heshima kwa muaji na waozeshaji (familia ya binti) pia.

Baada ya miaka sita ya furaha na huzuni, ndoa ya ndugu yangu imesimama wima, ikiwa na jumla ya watoto watatu, wakiume wawili na kabinti.

Kati ya watoto hao, mtoto mmoja (wa tatu) hafanani kabisa na watoto wengine, na hafanani na baba yake wala mama yakepia hafanani na yeyote katika familia yetu wala ya mwanamke.

Jambo hili lilimpa shaka bro, alijipa moyo lakini uafrika wetu ukamshinda. Maswali ya "mbona hafanani na sisi?" yalikuwa mengi, jambo lililomfanya bro aamue kutafuta suluhu ya nafsi yake.

Alianza kwa kupima DNA kwa Siri bila yeyote ndani ya familia kujua...majibu yakaonesha si wake (Tz)Akaenda nae Nairobi, huko akampima tena, ikaonesha si damu yake.

Kwa maelezo yake, anadai alienda kwa gwiji fulani huko Mombasa, nako akaambiwa si damu yake... Zaidi tena huko Mombasa, huyo mama (mganga) alimuonesha baba halisi wa mtoto yule

Bro alirudi kwake, akamkalisha kitako mke, akatumia maarifa na ujuzi wake wooote aliojaaaliwa kumshawishi mke amwambie chochote juu ya mtoto yule.

Japo lilikuwa jaribio gumu, lakini mke alikiri kuwa Moses, mtoto wa mwisho, si mtoto wa kaka. Na akamtaja baba yake halisi.

Picha iko hivi;
Shem katika makuzi yake, alikuwa na rafiki yake (mtoto mwenzake) ambaye walitengana baada ya familia ya huyo kijana kuhamia mkoa mwingine. Walipokua, walitafutana na wakaendelea kuwasiliana km wapenzi hadi shem alipoolewa.

Lakini licha ya kuolewa, mawasiliano yao yaliendelea na ahadi yao ilikuwa wazae mtoto mmoja ili iwe kumbukumbu ya mapenzi yao tangu utotoni na walipokuwa wakipata nafasi ya kukutana, basi walikuwa wananyanduana hadi mtoto huyo akapatikana..

Bro anataka kufanya maamuzi; ni moja tu kati ya mawili
1. Avunje ndoa au
2. Alinde ndoa

Binafsi km mshauri wa karibu, nimemshauri alinde ndoa. Kaniuliza KWANINI? Nimekosa jibu!
 
Habarini!!!
Ndoa ya ndugu yangu wa damu (kaka) imeingiliwa na kirusi hatarishi, maji yamezidi unga
Alimuoa binti (mke wake) kigori kabisa, na kwa utamaduni wetu, hili huwa tukio la heshima kwa muaji na waozeshaji (familia ya binti) pia.
Baada ya miaka sita ya furaha na huzuni, ndoa ya ndugu yangu imesimama wima, ikiwa na jumla ya watoto watatu, wakiume wawili na kabinti.
Kati ya watoto hao, mtoto mmoja (wa tatu) hafanani kabisa na watoto wengine, na hafanani na baba yake wala mama yake...pia hafanani na yeyote katika familia yetu wala ya mwanamke.
Jambo hili lilimpa shaka bro, alijipa moyo lakini uafrika wetu ukamshinda.
Maswali ya "mbona hafanani na sisi?" yalikuwa mengi, jambo lililomfanya bro aamue kutafuta suluhu ya nafsi yake..

Alianza kwa kupima DNA kwa Siri bila yeyote ndani ya familia kujua...majibu yakaonesha si wake (Tz)
Akaenda nae Nairobi, huko akampima tena, ikaonesha si damu yake..
Kwa maelezo yake, anadai alienda kwa gwiji fulani huko Mombasa, nako akaambiwa si damu yake... Zaidi tena huko Mombasa, huyo mama (mganga) alimuonesha baba halisi wa mtoto yule

Bro alirudi kwake, akamkalisha kitako mke, akatumia maarifa na ujuzi wake wooote aliojaaaliwa kumshawishi mke amwambie chochote juu ya mtoto yule.
Japo lilikuwa jaribio gumu, lakini mke alikiri kuwa Moses, mtoto wa mwisho, si mtoto wa kaka. Na akamtaja baba yake halisi.

Picha iko hivi;
Shem katika makuzi yake, alikuwa na rafiki yake (mtoto mwenzake) ambaye walitengana baada ya familia ya huyo kijana kuhamia mkoa mwingine. Walipokua, walitafutana na wakaendelea kuwasiliana km wapenzi hadi shem alipoolewa.
Lakini licha ya kuolewa, mawasiliano yao yaliendelea na ahadi yao ilikuwa wazae mtoto mmoja ili iwe kumbukumbu ya mapenzi yao tangu utotoni...na walipokuwa wakipata nafasi ya kukutana, basi walikuwa wananyanduana hadi mtoto huyo akapatikana..

Bro anataka kufanya maamuzi; ni moja tu kati ya mawili
1. Avunje ndoa au
2. Alinde ndoa

Binafsi km mshauri wa karibu, nimemshauri alinde ndoa..
Kaniuliza KWANINI? Nimekosa jibu!
Hekima ile aliyokuwa nayo Mfalme Suleiman inahitajika sana hapo.

Binafsi ningefunga nikisali zaidi ya siku 3 kumwomba Mungu anishauri kufanya maamuzi sahihi yasiyoweza kuleta athari baina yangu mimi binafsi na watoto.

Kwa jicho la 3 talaka ingefaa sana.
 
KWANI ,mleta mada kigori si anatakiwa awe bikra au ,kipi bora pia kuoa mke akiwa na mtoto wa nje au kuletewa mtoto wa nje kisirisiri,abaki kulea familia yake asishee nae mapenz , atajifukuz MWENYEWE TU ILA ALEE WATOTO HAWANA HATIA.
Bikra ndio kigori
Nachokiona kwa bro, ni kukosa majibu ya KWANINI avunje ndoa au alinde!?
Kwa mfano, nilimwambia akutane na huyo jamaa, amueleze everything...kisha amwambie aachane na mke wake
Akaniuliza atakuwa na uhakika gani km hawataendelea???? Nikashindwa kujibu
 
Hiv vitu havijaanza kwa kizaz hiki tu yalikuwepo toka zaman ndio maana walianzisha kamsemo kao "kitanda hakizai haramu" pia atambue yeye sio wa kwanza kulea watoto/mtoto ambaye sio wake. Hapo ndipo ulipo ukomavu wa akili na tatzo halitatuliwi kwa kukimbiwa.
Alinde ndoa yake apambane kuilinda familia yake ndio kitu pekee cha thamani alicho nacho ubinafsi usimfanye aipoteze.
 
Hekima ile aliyokuwa nayo Mfalme Suleiman inahitajika sana hapo.

Binafsi ningefunga nikisali zaidi ya siku 3 kumwomba Mungu anishauri kufanya maamuzi sahihi yasiyoweza kuleta athari baina yangu mimi binafsi na watoto.

Kwa jicho la 3 talaka ingefaa sana.
%kubwa ya fikra zake ni kuvunja ndoa..
Anahofu na mama, maana mapenzi aliyonayo mama kwa mkwe wake na wajukuu, hayapimiki
 
Hiv vitu havijaanza kwa kizaz hiki tu yalikuwepo toka zaman ndio maana walianzisha kamsemo kao "kitanda hakizai haramu" pia atambue yeye sio wa kwanza kulea watoto/mtoto ambaye sio wake. Hapo ndipo ulipo ukomavu wa akili na tatzo halitatuliwi kwa kukimbiwa.
Alinde ndoa yake apambane kuilinda familia yake ndio kitu pekee cha thamani alicho nacho ubinafsi usimfanye aipoteze.
Alinambia kuwa mke wake alimuomba amsamehe, na kuwa hatakuja kurudia tena, si tu kuzaa nje,,,bali kutembea nje ya ndoa..
Nadhani km binadamu anapoteza iman juu ya hilo
 
Back
Top Bottom