Ndoa haikuzuii kutochepuka moja kwa moja.

Ndoa haikuzuii kutochepuka moja kwa moja.

Haya niambie nilichepuka lini sasa mkuu?
Wengine tumetulia na ndoa zetu,humu JF tupo watu tofauti sana
Ulioa lini ? Na ulioa kabila gani? Kama ulioa Tanga naweza kuhisi labda kuna ka ukweli
 
Mkuu nimeoa kwa hawa wazaramo.
Lakini hata ningeoa mchaga nisingechepuka(kwa msaada wa Mungu)kwa sababu sio kwamba sichepuki eti mke ndo ananimaliza kitandani,hapana ila sichepuki kwa sababu najiona siwi huru,ni dhambi,sio hulka yangu tokea hapo tu,hivyo siwezi na najiona nipo huru zaidi kuliko nikiwaza kuchepuka.

Naishi kwa amani sana kwa sababu sijajiwekea kuchepuka kwa ajili ya mwanamke.
Kuna ambao wanachepuka kwa sababu ya wake zao hawawaridhishi,hawa wanachepuka kwa ajili ya mwanamke.

Na kuna ambao wanachepuka kwa sababu ya nyege tu zinawazidi na tamaa,hawa ni nafsi zao.
Lakini kubwa ni kwamba hakuna mwanaume hatamani vya nje kila mwanaume inamtokea kutamani baadhi ya wakati lakini ni suala la kujua tu kwamba hayo ni mawazo kama mawazo mengine sio lazima kuyafanyia kazi.

Ulioa lini ? Na ulioa kabila gani? Kama ulioa Tanga naweza kuhisi labda kuna ka ukweli
 
Safi kabisa.
Usiseme nikioa ntaachana vimada,kamwee unajidanganya.kama una madem watano na bado unawatamani wengine hivi ukiwa na mwanamke mmoja atakutosha kweli?
Hapo unajidanganya sana kaka mkubwa kama hawakukutosha vimada wale wa nje ambao ulikuwa nae zaidi ya mmoja basi jua huwezi kuridhika na huyo mke mmoja.

Zinaa ama kuchepuka kunaanza kukemewa ndani ya moyo alafu tunakuja nje ya mwili,lakini ubongo ukiutune kwamba hilo jambo hutaki jua kwamba na mwili utafuata ubongo tu,jiulize tu kwa nini mtu anapaka pilipili mikononi kwa ajili ya kuacha punyeto alafu baadae anaenda kutafuta sabuni ananawa kuondoa pilipili na anapiga punyeto,why?

Ni kwa sababu hajakemea ubongo kwanza,amekimbilia nje wakati ndani kibovu.

Lakini sasa uzuri wake ikiwa mtu amekomaa sana kibachela bila demu alafu akija kuoa atashindwaje kuvumilia siku za hedhi za mkewe na wakati wa kujifungua n.k wakati aliweza kukaa bila mke vipi ashindwe sasa?

Sasa kijana chinga sana kijana usiseme nikioa nitaacha,sema sijaoa naacha.
Ukiacha uzinzi kabla ya ndoa basi unauhakika mkubwa wa kujimudu hata baada ya ndoa.

Ukiacha kula chakula ambacho kinapatikana wakati unanjaa basi utaweza kuacha chakula ambacho kinapatikana wakati umeshiba.

Lakini ukiacha chakula ambacho kinapatikana wakati wa shibe tu basi jua hutoweza kuacha chakula ambacho kinapatikana wakati wa njaa,anza leo kukemea ubongo wako kwanza kalba ya mwili wako

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom