Ndoa haikuzuii kutochepuka moja kwa moja.

Ndoa haikuzuii kutochepuka moja kwa moja.

Kila mtu na anywe maji ya kisima chake mwenyewe.. mambo ya kuonja maji ya wengine sio poa kabisa..

Hata kama unakiu, hakikisha unakifikia kisima chako mwenyewe.




Sent using Jamii Forums mobile app
 
Usiseme nikioa ntaachana vimada,kamwee unajidanganya.kama una madem watano na bado unawatamani wengine hivi ukiwa na mwanamke mmoja atakutosha kweli?
Hapo unajidanganya sana kaka mkubwa kama hawakukutosha vimada wale wa nje ambao ulikuwa nae zaidi ya mmoja basi jua huwezi kuridhika na huyo mke mmoja.

Zinaa ama kuchepuka kunaanza kukemewa ndani ya moyo alafu tunakuja nje ya mwili,lakini ubongo ukiutune kwamba hilo jambo hutaki jua kwamba na mwili utafuata ubongo tu,jiulize tu kwa nini mtu anapaka pilipili mikononi kwa ajili ya kuacha punyeto alafu baadae anaenda kutafuta sabuni ananawa kuondoa pilipili na anapiga punyeto,why?

Ni kwa sababu hajakemea ubongo kwanza,amekimbilia nje wakati ndani kibovu.

Lakini sasa uzuri wake ikiwa mtu amekomaa sana kibachela bila demu alafu akija kuoa atashindwaje kuvumilia siku za hedhi za mkewe na wakati wa kujifungua n.k wakati aliweza kukaa bila mke vipi ashindwe sasa?

Sasa kijana chinga sana kijana usiseme nikioa nitaacha,sema sijaoa naacha.
Ukiacha uzinzi kabla ya ndoa basi unauhakika mkubwa wa kujimudu hata baada ya ndoa.

Ukiacha kula chakula ambacho kinapatikana wakati unanjaa basi utaweza kuacha chakula ambacho kinapatikana wakati umeshiba.

Lakini ukiacha chakula ambacho kinapatikana wakati wa shibe tu basi jua hutoweza kuacha chakula ambacho kinapatikana wakati wa njaa,anza leo kukemea ubongo wako kwanza kalba ya mwili wako
SAAAAAFIIII
 
Umenena vema kabisa @ Safuha!
Kwa hiyo wewe swala la mitala kwako halina nafasi kabisa?


Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu hii ID imepigwa ban nimekuja kivingine na wacha nijibu swali kama ifuatavyo.

Suala la kuchepuka maana yake ni kutoka nje ya ndoa kwa maana kuna mwanamke wa kando ambae hukufunga nae ndoa kisheria(inategemea na dini husika)

Na suala la mitala maana yake unakuwa na mke zaidi ya mmoja kwa ndoa ambazo zipo kisheria kwa hivyo unaweza kuwa na wake wanne lakini wote ni wake zako kisheria.

Lakini pia mtu anaweza kuwa na mitala wake wanne lakini bado akachepuka tu na wake anao.

Sasa hapo ni sawa na kusema hivi.
Mimi nina maisha yangu ya kawaida tu nimeridhika nayo wala sitafuti rizki kwa njia za haramu ili niongeze kipato,natumia njia za halali lakini naridhika na kipato changu.
Lakini kuridhika huko haina maana eti ndo siwezi kutafuta biashara zingine za kufanya kwa ajili ya kuongeza kipato,naweza kuridhika na kipato lakini ikawa bado napanua wigo wa biashara kupata kipato zaidi ambacho ni Cha HALALI na kutumia kwa NJIA HALALI.

na mitala iko hivyo hivyo,unaweza ukawa na mke mmoja lakini ukaongeza wa pili na wa tatu kama vile unavyozidi kufungus biashara zaidi ya moja huku ukiwa umeridhika na kipato chako.
 
Back
Top Bottom