Lamborghini
Senior Member
- May 30, 2014
- 122
- 55
nimelaik nikaona haitoshi. Yaani hapa nacheka mpaka machozi. Huwa nabaki mdomo wazi pale napoona watu wazima wakidaka safari toka kwa askofu "pokea safari ya china, pokea safari ya amerikani" halafu watu wazima wanaruka kwa furaha, wanadaka huku wengine hata wakiwa hawana paspoti. Kali kuliko zote ni pale wanapopokea gari, hihihihihihiiiiii,,,pokea funguo funguo za gari lako, ameeeeeeeen! Wanadaka funguo za kufikirika halafu wanaambiwa wawashe gari. Hapo hata kama huna bandama lazma ucheke. Watu wazima wanawasha gari, mkono mmoja umeshika usukani, mwingine unawasha. Wanasema, "chonyonyonyooo" halafu wanaitikia njii njii njii njiiiiii. katikati ya kicheko unashtuka kuwa hili ni janga, unaingiwa na huzuni unahamia chaneli nyingine.
seriously??.... sounds funny