KUFURAHIA TOZO KUFUTWA NI KUFURAHIA UMASIKINI
Na. Habibu Mchange
Ni bahati mbaya sana jambo jema la Tozo limetafsiriwa tofauti na kugeuzwa agenda hasi dhidi ya serikali
Sijui kama tunafurahi kuomba msaada Japan kujenga matundu ya vyoo kama nchi.
Kuomba ufadhili ulaya na America kununuliwa vitabu vya mitaala ya mashuleni mwetu
Tunafurahi kuona barabarani Mabango yameandikwa BARABARA HII IMEJENGWA KWA MSAADA WA KODI ZA WATU WA MAREKANI/ULAYA ni hatari sana hii
Hatutaki kuchangia maendeleo, lakini tunataka maendeleo ya haraka.
Tunadai barabara, madaraja, mikopo vyuo vikuu, madrasa, vituo vya Afya, ajira mpya, ruzuku katika pembejeo za kilimo, miradi ya umeme, maji nakadharika.
Watu wavivu kufukiri wanasema mbona huko nyuma huduma hizo zilitolewa, zilitolewaje bila tozo?.
Hataki kujua kuwa hata katika level tu ya familia yake miaka kumi nyuma alikuwa na familia kubwa kiasi gani na alikuwa anatumia unga/Mchele/Mboga kiasi gani kwa siku, maana yake ni Nini, maana yake ni kuwa mahitaji huongezeka kila mara na vyanzo vya mapato visipoongezeka jamii huduma.
Kwenye hili la Tozo nafikiri lilipaswa kuita Mchango wa maendeleo kwamba mtu anakatwa kuchangia maendeleo maalum tena lingewekewa kipindi maalum. Nafikiri watu wangeeleweshwa wangeelewa na wangechanga bila shaka.
Yaani, Serikali ilipaswa kutuambia uwezo wake wa makusanyo kwa mwaka, ikalinganisha na matumizi yake (ikiwemo kulipa madeni ya muda mrefu na mfupi, kusomesha watoto bila malipo, kulipa mishahara watumishi wa umma, kujenga miradi ya kimkakati kama niliyoitaja huko juu. Nakadharika). Wakaonyesha gharama zake.
Automatic kabisa makusanyo tunayokusanya kama nchi hayawezi kuhudumia mahitaji yote hayo, hivyo Serikali ingeelimisha watu umuhimu wa hiyo miradi, na kuwashauri watu kubuni njia ya dharura kufikia lengo ikiwemo kubana matumizi kwa serikali kuu, Bunge na Mahakama.
Ingetokea tangazo limetoka Bungeni, na wabunge wakatangazia umma kuwa katika posho zao za siku zinazofikia Hadi 360,000/= wameridhi wakatwe 200,000/= kila siku ya kikao Ili kuchangia mchango wa maendeleo japo kwamba nao wanakatwa Tozo wakifanya miamala hakuna mtu asingeelewa umuhimu wa kuchangia
Yaani Serikali inatangaza hadharani kuwa Rais anapokea mshaha kiasi X, Makamu wa Rais kiasi Y, Waziri Mkuu kiasi Z, spika, jaji mkuu na wengineo kiasi L, na kwa pamoja watapunguziwa mshahara na marupurupu kwa asilimia 40 au 50 katika kipindi hiki maalum. Watu wangeshangilia na wasingeona ugumu wa tozo wanazotozwa.
TUMECHELEWA?
Hatujachelewa sana, wenzetu nchi walizoendelea wanalipa Tozo Hadi za kumiliki Tv nyumbani kwao, kwamba ukimiliki TV, friji na vitu vyovyote ambavyo havikuzuii kuishi basi lazima ulipie Tozo.
Kama Taifa tunatakiwa turudi kwenye mjadala muhimu huu kujinusuru. Lazima tutafute suluhu kusonga mbele,
Tunapomlaumu Waziri Dkt. Mwigulu tukaliacha Bunge lililopaswa kutuelewesha umuhimu wa hii hatua ni kumuonea tu.
Tunapomlaumu Dkt. Mwigulu badala ya kupima dhamira, malengo na matumizi ya kilichokusanywa hadi sasa, ni kumsimanga tu na kuendeleza Nongwa.
Tunayo nafasi kama Taifa kuamua kujenga Taifa letu au tuendelee kutegemea wajomba na mashangazi.
Naishia hapa Kwa sasa nikiamini kuwa, kuliko kushangilia TOZO KUFUTWA TUSIKITIKE kwa sisi kuchagua kukataa kuchangia maendeleo yetu wenyewe.
Ndimi,
Habibu Mchange
Mwananchi wa kawaida