Ndimu ya Mchange: kufurahia tozo kufutwa ni kufurahia umasikini

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Jan 5, 2013
664
829
KUFURAHIA TOZO KUFUTWA NI KUFURAHIA UMASIKINI

Na. Habibu Mchange

Ni bahati mbaya sana jambo jema la Tozo limetafsiriwa tofauti na kugeuzwa agenda hasi dhidi ya serikali

Sijui kama tunafurahi kuomba msaada Japan kujenga matundu ya vyoo kama nchi.

Kuomba ufadhili ulaya na America kununuliwa vitabu vya mitaala ya mashuleni mwetu

Tunafurahi kuona barabarani Mabango yameandikwa BARABARA HII IMEJENGWA KWA MSAADA WA KODI ZA WATU WA MAREKANI/ULAYA ni hatari sana hii

Hatutaki kuchangia maendeleo, lakini tunataka maendeleo ya haraka.

Tunadai barabara, madaraja, mikopo vyuo vikuu, madrasa, vituo vya Afya, ajira mpya, ruzuku katika pembejeo za kilimo, miradi ya umeme, maji nakadharika.

Watu wavivu kufukiri wanasema mbona huko nyuma huduma hizo zilitolewa, zilitolewaje bila tozo?.

Hataki kujua kuwa hata katika level tu ya familia yake miaka kumi nyuma alikuwa na familia kubwa kiasi gani na alikuwa anatumia unga/Mchele/Mboga kiasi gani kwa siku, maana yake ni Nini, maana yake ni kuwa mahitaji huongezeka kila mara na vyanzo vya mapato visipoongezeka jamii huduma.

Kwenye hili la Tozo nafikiri lilipaswa kuita Mchango wa maendeleo kwamba mtu anakatwa kuchangia maendeleo maalum tena lingewekewa kipindi maalum. Nafikiri watu wangeeleweshwa wangeelewa na wangechanga bila shaka.

Yaani, Serikali ilipaswa kutuambia uwezo wake wa makusanyo kwa mwaka, ikalinganisha na matumizi yake (ikiwemo kulipa madeni ya muda mrefu na mfupi, kusomesha watoto bila malipo, kulipa mishahara watumishi wa umma, kujenga miradi ya kimkakati kama niliyoitaja huko juu. Nakadharika). Wakaonyesha gharama zake.

Automatic kabisa makusanyo tunayokusanya kama nchi hayawezi kuhudumia mahitaji yote hayo, hivyo Serikali ingeelimisha watu umuhimu wa hiyo miradi, na kuwashauri watu kubuni njia ya dharura kufikia lengo ikiwemo kubana matumizi kwa serikali kuu, Bunge na Mahakama.

Ingetokea tangazo limetoka Bungeni, na wabunge wakatangazia umma kuwa katika posho zao za siku zinazofikia Hadi 360,000/= wameridhi wakatwe 200,000/= kila siku ya kikao Ili kuchangia mchango wa maendeleo japo kwamba nao wanakatwa Tozo wakifanya miamala hakuna mtu asingeelewa umuhimu wa kuchangia

Yaani Serikali inatangaza hadharani kuwa Rais anapokea mshaha kiasi X, Makamu wa Rais kiasi Y, Waziri Mkuu kiasi Z, spika, jaji mkuu na wengineo kiasi L, na kwa pamoja watapunguziwa mshahara na marupurupu kwa asilimia 40 au 50 katika kipindi hiki maalum. Watu wangeshangilia na wasingeona ugumu wa tozo wanazotozwa.

TUMECHELEWA?
Hatujachelewa sana, wenzetu nchi walizoendelea wanalipa Tozo Hadi za kumiliki Tv nyumbani kwao, kwamba ukimiliki TV, friji na vitu vyovyote ambavyo havikuzuii kuishi basi lazima ulipie Tozo.

Kama Taifa tunatakiwa turudi kwenye mjadala muhimu huu kujinusuru. Lazima tutafute suluhu kusonga mbele,

Tunapomlaumu Waziri Dkt. Mwigulu tukaliacha Bunge lililopaswa kutuelewesha umuhimu wa hii hatua ni kumuonea tu.

Tunapomlaumu Dkt. Mwigulu badala ya kupima dhamira, malengo na matumizi ya kilichokusanywa hadi sasa, ni kumsimanga tu na kuendeleza Nongwa.

Tunayo nafasi kama Taifa kuamua kujenga Taifa letu au tuendelee kutegemea wajomba na mashangazi.

Naishia hapa Kwa sasa nikiamini kuwa, kuliko kushangilia TOZO KUFUTWA TUSIKITIKE kwa sisi kuchagua kukataa kuchangia maendeleo yetu wenyewe.

Ndimi,
Habibu Mchange
Mwananchi wa kawaida

Screenshot_20220923-092643.jpg
 
Watu wa Nchi hii ni WA ajabu Sana, Kodi hawataki Kulipa,tozo hawataki harafu Wanadai maendeleo na huduma.

Serikali ikikopa hawataki kana kwamba Nchi imesimama mahitaji yamesimama au yameisha.

Wanaojifanya wanapiga makelele kwenye redio watoto wao hawasomi kwenye shule zenye msongamano wa madarasa Wala huko Vijijini ila mdomo sasa.
 
Tozo haina ubaya. Ubaya uko kwenye matumizi. Fikiria
1. Tuliambiwa madarasa na zahanati zilijengwa kwa hela ya UVIKO 19

2. Tukaambiwa tena madarasa hayo hayo na zahanati hizohizo zimejengwa kwa hela ya tozo.

Magufuli alijenga mabarabara, madaraja; mazahanati, vituo vya afya , bwawa la mwl Nyerere n SGR bila tozo na bila mikopo mingi kama hii leo.

Wabane matumizi na tuone vitendo na maisha bora tutawaunga mikono.

Pia kauli za viongozi wachunge.
 
Mnasema nchi nyingi Zina tozo, hakuna anaetoa mfano wa nchi gani, ni tozo ya sh ngapi kwa muamala gani, ambao Kodi yake ya kawaida ni sh ngapi. Watu wanataka kujua Kodi yote kwa mwaka ni sh ngapi, mikopo ni sh ngapi na tozo ni sh ngapi, faida kwenye uwekezaji wa serikali ni ngapi, misaada n.k sio kukamuliwa tuu Kama maiti.
 
Huyu naona hajielewi kabisa. Haelewi hata kinacholalamikiwa.

Barabara hazijengwi kwa tozo. Shule hazijengwi kwa tozo. Vitabu vya rejea na kiada kwa wanafunzi havinunuliwi kwa tozo. Hivi vitu vyote vinagharamiwa na kodi tunazolipa.

Kama vyote alivyoandika, anataka vigharamiwe na tozo, kodi tunazolipa anataka zifanye nini?
 
Wewe, Masanja Mkandamizaji, Suphian, Habibu na wengi wengine mnaoshangilia tozo hamjui kanuni za kodi, hamjui kitu gani hasa kinatakiwa kitozwe kodi. Mngefunga tu midomo yenu muwaache wajuzi wa hayo mambo wayachambue, msilazimishe siasa za uchawa katika kila issue, lihurumieni taifa lenu na vizazi vyenu vijavyo.
Watu wa Nchi hii ni WA ajabu Sana,Kodi hawataki Kulipa,tozo hawataki harafu Wanadai maendeleo na huduma..

Serikali ikikopa hawataki kana kwamba Nchi imesimama mahitaji yamesimama au yameisha..

Wanaojifanya wanapiga makelele kwenye redio watoto wao hawasomi kwenye shule zenye msongamano wa madarasa Wala huko Vijijini ila mdomo sasa..
 
Kwa thread nzima cha maana ulichoandika ni kupunguza posho za wabunge kutoka tsh 360000 kwa siku mpaka 160k hapo sawa kwani haileti logic mbunge alipwe posho ya kuhudhuria kikao dodoma wakati analipwa mshahara mwisho wa mwezi na kuhudhuria vikao vya bunge ndio wajibu wa kwanza kwa kazi aliyoiomba kwa wapiga kura wake
 
Ni bahati mbaya sana jambo jema la Tozo limetafsiriwa tofauti na kugeuzwa agenda hasi dhidi ya serikali

Sijui kama tunafurahi kuomba msaada Japan kujenga matundu ya vyoo kama nchi.

Kuomba ufadhili ulaya na America kununuliwa vitabu vya mitaala ya mashuleni mwetu

Tunafurahi kuona barabarani Mabango yameandikwa BARABARA HII IMEJENGWA KWA MSAADA WA KODI ZA WATU WA MAREKANI/ULAYA ni hatari sana hii

Hatutaki kuchangia maendeleo, lakini tunataka maendeleo ya haraka.

Tunadai barabara, madaraja, mikopo vyuo vikuu, madrasa, vituo vya Afya, ajira mpya, ruzuku katika pembejeo za kilimo, miradi ya umeme, maji nakadharika.

Watu wavivu kufukiri wanasema mbona huko nyuma huduma hizo zilitolewa, zilitolewaje bila tozo?.

Hataki kujua kuwa hata katika level tu ya familia yake miaka kumi nyuma alikuwa na familia kubwa kiasi gani na alikuwa anatumia unga/Mchele/Mboga kiasi gani kwa siku....maana yake ni Nini, maana yake ni kuwa mahitaji huongezeka kila mara na vyanzo vya mapato visipoongezeka jamii hudumaa

Kwenye hili la Tozo nafikiri lilipaswa kuita Mchango wa maendeleo kwamba mtu anakatwa kuchangia maendeleo maalum tena lingewekewa kipindi maalum. Nafikiri watu wangeeleweshwa wangeelewa na wangechanga bila shaka

Yaani, Serikali ilipaswa kutuambia uwezo wake wa makusanyo kwa mwaka, ikalinganisha na matumizi yake (ikiwemo kulipa madeni ya muda mrefu na mfupi, kusomesha watoto bila malipo, kulipa mishahara watumishi wa umma, kujenga miradi ya kimkakati kama niliyoitaja huko juu. Nakadharika). Wakaonyesha gharama zake.

Automatic kabisa makusanyo tunayokusanya kama nchi hayawezi kuhudumia mahitaji yote hayo, hivyo Serikali ingeelimisha watu umuhimu wa hiyo miradi, na kuwashauri watu kubuni njia ya dharura kufikia lengo ikiwemo kubana matumizi kwa serikali kuu, Bunge na Mahakama.

Ingetokea tangazo limetoka Bungeni, na wabunge wakatangazia umma kuwa katika posho zao za siku zinazofikia Hadi 360,000/= wameridhi wakatwe 200,000/= kila siku ya kikao Ili kuchangia mchango wa maendeleo japo kwamba nao wanakatwa Tozo wakifanya miamala hakuna mtu asingeelewa umuhimu wa kuchangia

Yaani Serikali inatangaza hadharani kuwa Rais anapokea mshaha kiasi X, Makamu wa Rais kiasi Y, Waziri Mkuu kiasi Z, spika, jaji mkuu na wengineo kiasi L, na kwa pamoja watapunguziwa mshahara na marupurupu kwa asilimia 40 au 50 katika kipindi hiki maalum. Watu wangeshangilia na wasingeona ugumu wa tozo wanazotozwa.

TUMECHELEWA?
Hatujachelewa sana, wenzetu nchi walizoendelea wanalipa Tozo Hadi za kumiliki Tv nyumbani kwao, kwamba ukimiliki TV, friji na vitu vyovyote ambavyo havikuzuii kuishi basi lazima ulipie Tozo.

Kama Taifa tunatakiwa turudi kwenye mjadala muhimu huu kujinusuru. Lazima tutafute suluhu kusonga mbele,

Tunapomlaumu Waziri Dkt. Mwigulu tukaliacha Bunge lililopaswa kutuelewesha umuhimu wa hii hatua ni kumuonea tu.

Tunapomlaumu Dkt. Mwigulu badala ya kupima dhamira, malengo na matumizi ya kilichokusanywa hadi sasa, ni kumsimanga tu na kuendeleza Nongwa.

Tunayo nafasi kama Taifa kuamua kujenga Taifa letu au tuendelee kutegemea wajomba na mashangazi.

Naishia hapa Kwa sasa nikiamini kuwa, kuliko kushangilia TOZO KUFUTWA TUSIKITIKE kwa sisi kuchagua kukataa kuchangia maendeleo yetu wenyewe.
 
Tozo haina ubaya. Ubaya uko kwenye matumizi. Fikiria
1. Tuliambiwa madarasa na zahanati zilijengwa kwa hela ya UVIKO 19

2. Tukaambiwa tena madarasa hayo hayo na zahanati hizohizo zimejengwa kwa hela ya tozo.

Magufuli alijenga mabarabara, madaraja; mazahanati, vituo vya afya , bwawa la mwl Nyerere n SGR bila tozo na bila mikopo mingi kama hii leo.

Wabane matumizi na tuone vitendo na maisha bora tutawaunga mikono.

Pia kauli za viongozi wachunge.
Barabara aliyoijenga magufuli inayounganisha mkoa mmoja na mwingine ni ipi?Ntajie hata moja tu.Barabara zote kubwa zilijengwa ktk awamu ya nne na mzee wa msoga.Magufuli alijengea mdomoni.
 
Back
Top Bottom