Ndege za Tanzania zapigwa marufuku kutua viwanja vya Kenya kutokana na janga la Corona

G Sam

JF-Expert Member
Apr 20, 2013
11,555
35,880
Ama kwa hakika mambo si shwari. Naona ndege za Tanzania nazo zimeanza kupata hitilafu kama ile ya Kenya

---

Akizungumza jijini Nairobi wakati akitoa taarifa kuhusu mwendendo wa maambukizi ya janga la Covid-19 nchini Kenya, Waziri wa Usafirishaji James Macharia amesema kuwa anga la Kenya halitafunguliwa kwa kila mtu. Orodha ikionesha wazi Tanzania ikiwa si mmoja wa nchi inayokaribishwa kwenye anga ya Kenya.

Macharia amesema ni raia wa nchi 11 pekee wa kigeni ndio watakaoruhusiwa kutua Kenya katika viwanja vyake vinne vya kimataifa vilivyopo Nairobi, Mombasa, Eldoret na Kisumu.

Nchi zilizoruhusiwa ni China, Korea Kusini, Japan, Canada, Zimbabwe, Ethiopia, Switzerland, Uganda, Rwanda, Namibia na Morocco.
Waziri huyo amesema nchi hizo zimedhibiti janga la Covid- 19 kwa kiasi cha kuridhidha.

Amesema nchi hizo zimepunguza maambukizi ya ugonjwa huo na raia wake wamekuwa wakipata dalili za kawaida za ugonjwa wa mfumo wa upumuaji.

''Tutaendelea kuboresha orodha yetu kwa kutegemea na hali ilivyo na mazingira. Hii ni orodha yetu kwa leo tutaipitia tena kesho na siku zinazokuja.''

''Abiria wote watakaowasili kwa ndege za kimataifa wakiwa na hati zinazoonesha kuwa hawana dalili za Covid-19 na wale waliopima saa 96 kabla ya safari hawatakaa karantini,'' alisema.

Mara tu orodha ilipotolewa, Wakenya kwa haraka waligundua kuwa Tanzania haimo.

Siku ya Jumatatu tarehe 27 mwezi Julai, Rais Uhuru Kenyatta alitoa kauli ambayo haikuilenga Tanzania moja kwa moja kuwa Kenya haifichi idadi ya watu wenye maambukizi ya Covid-19.

''Sisi tuko wazi na tunajua fika kuwa ugonjwa huu upo tofauti na majirani zetu ambao wanauficha ukweli huu,'' alisema Rais Kenyatta.

Chanzo: BBC
 
Jibu ni moja tu,ndege zenyewe kwa ujumla hakuna faida zipo kama mapambo tu na moja ya sababu tumekosa kiongozi katika hili.

Note!!
Li-Sun-Likali jana katimba stendi ya Ifakara akwaambia waliokuwa wapiga kura wake:Jamani samahanini sikujua kama hawa jamaa wako hivi,
Raia mmoja akamwambia hukuwa unawajua?Nilikupa pilipiki na laki 7 zikusaidie kwenye kampeni hukunrudishia hata jero leo unakuja kuzingua
 
Hahahaha wakenya wana hangaika sana haahaha hivi wanafikiri ugonjwa unafichwa?hahahaha tuna watakia kila la kheri hahahaha!

Kenya wanaumia sana kuona Tanzania wanaendelea na shughuli zao kama kawaida hahahha jamani kila mtu apambane na hali yake ugonjwa haufichiki!

Tunawatakia kila la kheri!
 
Haya ni ya kawaida sana kwa Nchi Washirika popote Duniani hutokea mambo ya namna hii.

Hakuna wa kulaumiwa hapa, pengine hii inafanywa kama justification ya kitu fulani.

Uzuri ni kuwa sisi kama Taifa na Mwanachama wa EAC tumeonesha njia wenzetu hata kama hawataki kukubali directly katika kukabiliana na janga la Covid-19.
 
Wakenya wanafiki tu hapo wanatufanyia kwa vita ya utalii tu na si lolote, japo hili picha ni la kutisha, nahofu sana huko mbeleni nahisi dunia itatutenga!
 
Back
Top Bottom