Ndege za Tanzania zapigwa marufuku kutua viwanja vya Kenya kutokana na janga la Corona

G Sam

JF-Expert Member
Apr 20, 2013
9,966
2,000
Ama kwa hakika mambo si shwari. Naona ndege za Tanzania nazo zimeanza kupata hitilafu kama ile ya Kenya

---

Akizungumza jijini Nairobi wakati akitoa taarifa kuhusu mwendendo wa maambukizi ya janga la Covid-19 nchini Kenya, Waziri wa Usafirishaji James Macharia amesema kuwa anga la Kenya halitafunguliwa kwa kila mtu. Orodha ikionesha wazi Tanzania ikiwa si mmoja wa nchi inayokaribishwa kwenye anga ya Kenya.

Macharia amesema ni raia wa nchi 11 pekee wa kigeni ndio watakaoruhusiwa kutua Kenya katika viwanja vyake vinne vya kimataifa vilivyopo Nairobi, Mombasa, Eldoret na Kisumu.

Nchi zilizoruhusiwa ni China, Korea Kusini, Japan, Canada, Zimbabwe, Ethiopia, Switzerland, Uganda, Rwanda, Namibia na Morocco.
Waziri huyo amesema nchi hizo zimedhibiti janga la Covid- 19 kwa kiasi cha kuridhidha.

Amesema nchi hizo zimepunguza maambukizi ya ugonjwa huo na raia wake wamekuwa wakipata dalili za kawaida za ugonjwa wa mfumo wa upumuaji.

''Tutaendelea kuboresha orodha yetu kwa kutegemea na hali ilivyo na mazingira. Hii ni orodha yetu kwa leo tutaipitia tena kesho na siku zinazokuja.''

''Abiria wote watakaowasili kwa ndege za kimataifa wakiwa na hati zinazoonesha kuwa hawana dalili za Covid-19 na wale waliopima saa 96 kabla ya safari hawatakaa karantini,'' alisema.

Mara tu orodha ilipotolewa, Wakenya kwa haraka waligundua kuwa Tanzania haimo.

Siku ya Jumatatu tarehe 27 mwezi Julai, Rais Uhuru Kenyatta alitoa kauli ambayo haikuilenga Tanzania moja kwa moja kuwa Kenya haifichi idadi ya watu wenye maambukizi ya Covid-19.

''Sisi tuko wazi na tunajua fika kuwa ugonjwa huu upo tofauti na majirani zetu ambao wanauficha ukweli huu,'' alisema Rais Kenyatta.

Chanzo: BBC
 

Omulasil

JF-Expert Member
May 5, 2015
3,133
2,000
Si wazuie na Precision au wanadhani ninya Kenya?
Wakoloni waliharibu sana ndugu zetu kuna haja ya kuwakomboa kama tulivyofanya kusini mwa Afrika. Wako mentaly colonized
 

BUSH BIN LADEN

JF-Expert Member
Mar 16, 2019
2,245
2,000
Kama wanapima, weka hapa updates ya corona virus cases in Tanzania!!

Kwamba Wizara inatoa certificates ni kwa sababu wanalazimika kufanya hivyo since huwezi kuingia nchi ya watu wakati status yako haifahamiki!
We jamaa nae ni kama unajua vitu vingi hadi unachanganyikiwa. Sisi kwetu tumeshakubaliana kwamba corona ni ugonjwa kama yalivo mengine, tumekubali kuishi nao. Ila kama kuna nchi itatutaka tuwapime raia wetu kama kigezo cha kuingia kwao ndo wizara inafanya na kuwapa certificate. Ni kama tunavochoma chanjo ya yellow fever, inaweza kuwa sio matakwa yetu lakini kwa kuwa nchi nyingi ukitaka kuzitembelea wanahitaji uthibitisha kama umechanjwa ndo maana serikali wanatuchoma na kutupa certificate. So unapoomba takwimu za wangapi wamepimwa corona wakati huulizi takwimu za wangapi wamechanjwa yellow fever ni kama ukichaa. Ishu ni kuwa tumetofautiana na wenzetu jinsi ya kulitazama janga kitu ambacho sio cha ajabu. Ukiforce tuweke hadharani takwimu za wangapi wamepimwa corona usiishie hapo, omba na takwimu za waliopima HIV, homa ya ini nk. Tumeamua kuichukulia sawa na mengine ila kwa watakaohitaji uthibitisho raia wetu tutawapima na kuwapa certificate sawa na tunavowapa za yellow fever, homa ya ini nk
 

wagagagigi

JF-Expert Member
Dec 9, 2014
503
1,000
Kenya wanachekesha, wao Corona imewachapa hasa alafu wanakuja na mbwembwe kuwa hizo nchi zimepambana na Corona vilivyo!
Mbona wao wameshindwa?

Waseme tu ndiyo masharti ya mkopo waliopata!
Mkuu,
Naona wachekeshaji zaidi ni sisi tusiotoa takwimu, tuliamu kuziweka chini ya mvungu halafu tukajitangazia kwamba tuko corona free! Bila ya takwimu ni mjinga peke yake ndie atakaeamini huu upuuzi!
 

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
3,706
2,000
We jamaa tangu April ukionaga story za Corona unashupaza shingo sana. Ulikomaa na lockdown weeeee mpaka ukajiona mjinga. Shule zimefunguliwa tangu July mpaka leo shwari tu. Mmebaki mnaokoteza maneno tu. Last week watu wamejaa uwanja wa Mkapa kumuaga Ila hakuna cha mlipuko wa COVID19 wala nini., Mmejazana airport kumpokea Lissu na hakuna cha COVID19 wala nini. Bado unakomaa na Corona tu????, Huonagi aibu mkuu?.. Tanzania hakuna Corona, kama mnaipenda sana CORONA si muhamie huko KENYA??
Pamoja na kurukia kichwa kichwa (trespassing) hoja bila hodi, Maswali yote yaliyokuwa mule hukuyaona bali kwenda kuandika huo utopolo? Hata aibu kidogo hamna?

Tulikuwapo siyo JKNIA peke yake, bali pia Uhuru na wengine hadi Lupaso achilia mbali waolikwenda Uhuru wasipate nafasi ya kuingia.

Hivyo kwenda JKNIA wala isikupe taabu.

Kote kutatu tuliweza kufika. Wewe unayejidhania kuwa mzalendo sana kuliko wengine uliweza kufika kupi, mburura wee?!

Ungekuwa na hoja ungekuwa umeyajibu maswali yale yaliyokuwa kwenye bandiko ulilorukia. Huna hoja, huna lolote zaidi ya kuwa ni mchumia tumbo, mbinafsi mkubwa usiyekuwa na mbele wala nyuma.

Eti nikajiona mjinga. Nilikwambia hayo au ndiyo ya kujitekenya mwenyewe na kujichekesha mbumbumbu mkubwa wee?!

Nyie ni mzigo na hasara kubwa kwa taifa hili. Haisaidii lolote kuacha kukupeni makavu makavu bila ya kumung'unya maneno.

Hakuna mwenye chembe ya akili mkichwa anayeweza kuthubutu kumtamkia mwingine eti aondoke nchini. Si mburura wewe wala si jiwe.

Haondoki mtu hapa!

Unataka list ya waliokufa kwa corona?

Kupisha magomvi na malalamiko uchwara, list ya wanasheria nguli iliwahi kuwekwa hapa. Ipi unataka, ya vigogo?

Tuokoteze maneno sisi au wewe ndiye mwokotezaji?

Eti hakuna Corona Tanzania - utopolo mtupu.

IMG_20200731_164008_538.jpg
 

magu2016

JF-Expert Member
Oct 8, 2017
2,674
2,000
Mkuu,
Naona wachekeshaji zaidi ni sisi tusiotoa takwimu, tuliamu kuziweka chini ya mvungu halafu tukajitangazia kwamba tuko corona free! Bila ya takwimu ni mjinga peke yake ndie atakaeamini huu upuuzi!
Wewe uko TZ au unaandika ukiwa Kunyaland? Takwimu za Corona zinakusaidia nini? kwanini Corona na wala si Malaria inayotusumbua zaidi na inaua sana?? Acha kufuata tu kama upepo! Takwimu zipo lakini siyo lazima kutangazwa publically na nchi nyingi zimeshaacha kutangaza publically.
 

Mbogo nyeusi

Senior Member
Dec 27, 2019
110
250
Watawala wa Tanzania na wa Kenya watuambie ukweli, siku ya maziko ya mzee wetu tuliona taarifa kwenye mitandao na vyombo rasmi vya habari kuwa ndege iliyokuwa na wajumbe kutoka Kenya waliokuwa wanakuja Tanzania kushiriki nasi kumzika mzee wetu ilizuiwa kutua uwanja wa JNIA na kutakiwa kurudi Nairobi, Kenya.

Na baada ya siku moja tuliona balozi wa Kenya akikanusha na kutoa taarifa kuwa ndege iliyokuwa na hitilafu ndio maana ikatakiwa kurudi Nairobi.

Kabla Mambo hayajakaa sawa tukiwa bado tunajiuliza nini kilitokea na kutafakari kauli ya balozi eti ndege ilikuwa na hitilafu kwa nini irudi Nairobi isitue viwanja vya karibu au hata KIA?

Gafla tunaona Kenya wanataja nchi zinazo takiwa kurusha ndege zao katika anga ya Kenya sisi majirani zao hatupo.
Ndani ya muda mfupi tunaona wabogo wanajibu mapigo kwa kufunga anga yetu kwa shirika la ndege la Kenya.

Nataka kujua kwenye hili zuio la ndege inahusu mashirika ya ndege ya haya mataifa tu kwa maana ya Air Tanzania na Kenya Airways? Au inahusu ndege yeyote itakayotua Kenya haitaruhusiwa kuja Tanzania au ndege yeyote itakayo tua Tanzania haitaruhusiwa kutua Kenya? Umoja wa nchi za Afrika Mashariki unaelekea kufa na dalili ndio hizi, kwa Mara hii Tanzania ndio tutalaumiwa kuvunja umoja wetu uliopiganiwa na kurejeshwa na mzee wetu mkapa baada ya uliokuwa Umoja wa Afrika Mashariki kuvunjika mwaka 1977.
 

Lucas Mobutu

JF-Expert Member
Jul 29, 2017
13,356
2,000
Kama Kenya haijataja Tz kuwa moja ya nchi zinazoruhusiwa raia wake kuingia kule hiyo inamaanisha lile katazo la Tz ni sio tu kwa KQ ila ndege zote za kenya na raia wake
 

Lucas Mobutu

JF-Expert Member
Jul 29, 2017
13,356
2,000
alafu mkuu tuweke tu mambo sawa,Historia sawa,ule umoja uliovunjika miaka ya 70 sisi ndio tulikuwa chanzo, sisi chanzo kikubwa na wakenya chanzo kidogo,Amin hakuwa na kosa.

alichokifanya Amin ni kwamba kwa mfano wewe usafiri alafu ukiwa safarini nyumba yako ivaniwe na majambazi ambao walipewa ushirikiano na jirani yako (kenya) so akavunja uhusiano na kenya na aliwategea na Bomu kwenye ndege ya mmoja wa viongozi wao akafa ,na kuhusu Tz ilifadhili uvamizi zaidi ya mara mbili huko Uganda kina museveni walipewa siraha na mafunzo huku ndio maana idd amin akatoa agizo watz na wakenya wote warudi kwao ndani ya masaa 48 na atakayebaki atakuwa kama amekalia moto
 

The Monk

Platinum Member
Oct 12, 2012
14,822
2,000
Kuna uwezekano maandalizi ya kutupiga ban yalishafikiwa ilibaki kutoa taarifa tu, sasa wakuu walivyosikia wenzao wanakuja huku wakaona itakua kukinzana na maazimio yao. Nafikiri hapo ndio ikabidi waambiwe wageuze wasitue kabisa. Huo ni mtazamo na mawazo yangu lakini.
 

Detective J

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
11,192
2,000
kama Kenya haijataja Tz kuwa moja ya nchi zinazoruhusiwa raia wake kuingia kule hiyo inamaanisha lile katazo la Tz ni sio tu kwa KQ ila ndege zote za kenya na raia wake
Wamesema kenya tu. Hawajasema watu. Since kwenda kenya si lazima ndege. Kuna mabasi.. hata miguu.
So hawajazuia raia.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom