Ndege za Tanzania zapigwa marufuku kutua viwanja vya Kenya kutokana na janga la Corona

Achana nao hao Mzee Wana njaa Sana imewapanda mpaka kwenye ubongo ndio maana wanafanya maamuzi Kama hayo.
 
Kwahiyo wewe unashinda kwenye makaburi yote Tanzania ?.Unataka kuniambia kazi yako ni kuuliza ndugu waliofiwa na wapendwa wao.
Nimesema mtaani kwetu hakuna case ya Covid19 hata moja niliyo iisikia. Nielekeze huko watu wanako kufa kwa Covid19 kwa wingi kiasi cha kufanya hadi shughuli za nchi nzima kusimama ili na Mimi nikashuhudie. Jamani hivi watu wanavyo songamana hivyo kwenye mabasi, masoko, vivuko n.k Corona ingekuwa hatari Kama inavyo daiwa si watanzania tungeisha? Acheni kulazimisha mambo yasiyo kuwa na maana.
 
Partiner airlines zinakuja hapa! KQ na hizo wanagawiana wasafiri! Ikija BA, kwanini asiwakaie tiketi?
Kwahiyo anawakatia ticket partiner airlines wasafiri toka dsm kwenda Nairobi wakati anajifanya amazuia ndege toka tz? Zuio lake la nini sasa au alitaka tu watu wajue Tz si kwema?
 
UWE MWANGALIFU , NIMEZUNGUMZA NAO MIDA SIO MREFU , WANASEMA USIPOSAFIRI UNAWEZA KUSAFIRI KWA TIKETI HIYO HIYO BAADAE
 
Hii imekaeje wadau, kenya wamezuia flights from Tz lkn ndege yao ukiingia mtandao wao bado wanakatisha ticket, au shida ni kutuhujumu tu ili dunia ijue tz sio salama?

We dogo muongo! Wanakatishaje ticket wakati hakuna safari za ndege!!?? Au kwa kuwa portal yao haikuzuii kununua ndio unasema wanakatisha?? Umefanikiwa kufanya hata booking???

Sijui inakusaidia nini kudanganya!!
 
UKIKATA ONLINE UTAKUWA UMEFANYAJE ?
 
Achana nao hao Mzee Wana njaa Sana imewapanda mpaka kwenye ubongo ndio maana wanafanya maamuzi Kama hayo.

Njaa unayo wewe mkuu. Kama taifa tuliposema hakuna tena corona na kuacha kutoa takwimu (hata za kutengeneza) hatukuwa tunaangalia mbele!! Wanaofanya maamuzi sahihi (informed decisions) huangalia taarifa. Bila taarifa mambo haya yatatukuta na hata watalii watasubiri taarifa hizi kufanya maamuzi yao. Sisi tulifanya maamuzi yetu na wakayaheshimu. Wamefanya yao, tuyaheshimu. Hatupendi kuingiliwa maamuzi, tusiingilie yao!!
 
Hii imekaeje wadau, kenya wamezuia flights from Tz lkn ndege yao ukiingia mtandao wao bado wanakatisha ticket, au shida ni kutuhujumu tu ili dunia ijue tz sio salama?
Subiri tunajipanga ili tuwanyooshe! You just wait and see! Very soon we will fix this Kunyaland people! Nawashauri watz wasikate tiketi hizo wasije wakapata hasara bure.
 
Njaa unayo wewe mkuu. Kama taifa tuliposema hakuna tena corona na kuacha kutoa takwimu (hata za kutengeneza) hatukuwa tunaangalia mbele!! Wanaofanya maamuzi sahihi (informed decisions) huangalia taarifa. Bila taarifa mambo haya yatatukuta na hata watalii watasubiri taarifa hizi kufanya maamuzi yao. Sisi tulifanya maamuzi yetu na wakayaheshimu. Wamefanya yao, tuyaheshimu. Hatupendi kuingiliwa maamuzi, tusiingilie yao!!
Hata sisi maamuzi yetu yafuatayo wayaheshimu pia!
 
Hii imekaeje wadau, kenya wamezuia flights from Tz lkn ndege yao ukiingia mtandao wao bado wanakatisha ticket, au shida ni kutuhujumu tu ili dunia ijue tz sio salama?

Sisi hatuna tatizo kenya ni ndugu zetu wana hasira zikitulia watatambua ukweli na hatuna mpango wa kuwazuia!
 
Tz na kenya naona ni zaidi ya wake wenza sio kwa wivu huo na hii inachangiwa zaidi na mke mdogo kuona mke mkubwa akiendelea
 
Ndiyo maana sijaona faida ya EAC.wivu was kike utawaua hawa.ngoja corona iwachakaze
 
Sisi hatuna tatizo kenya ni ndugu zetu wana hasira zikitulia watatambua ukweli na hatuna mpango wa kuwazuia!
mkuu samahani hii mambo ya kusema kenya ndugu zetu inanikera kweli, hawa ni jirani tu ambao wanaweza kuwa adui zetu vilevile kama ambavyo imewahi kutokea kwa uganda.
 
Ama kwa hakika mambo si shwari. Naona ndege za Tanzania nazo zimeanza kupata hitilafu kama ile ya Kenya

---

Akizungumza jijini Nairobi wakati akitoa taarifa kuhusu mwendendo wa maambukizi ya janga la Covid-19 nchini Kenya, Waziri wa Usafirishaji James Macharia amesema kuwa anga la Kenya halitafunguliwa kwa kila mtu. Orodha ikionesha wazi Tanzania ikiwa si mmoja wa nchi inayokaribishwa kwenye anga ya Kenya.

Macharia amesema ni raia wa nchi 11 pekee wa kigeni ndio watakaoruhusiwa kutua Kenya katika viwanja vyake vinne vya kimataifa vilivyopo Nairobi, Mombasa, Eldoret na Kisumu.

Nchi zilizoruhusiwa ni China, Korea Kusini, Japan, Canada, Zimbabwe, Ethiopia, Switzerland, Uganda, Rwanda, Namibia na Morocco.
Waziri huyo amesema nchi hizo zimedhibiti janga la Covid- 19 kwa kiasi cha kuridhidha.

Amesema nchi hizo zimepunguza maambukizi ya ugonjwa huo na raia wake wamekuwa wakipata dalili za kawaida za ugonjwa wa mfumo wa upumuaji.

''Tutaendelea kuboresha orodha yetu kwa kutegemea na hali ilivyo na mazingira. Hii ni orodha yetu kwa leo tutaipitia tena kesho na siku zinazokuja.''

''Abiria wote watakaowasili kwa ndege za kimataifa wakiwa na hati zinazoonesha kuwa hawana dalili za Covid-19 na wale waliopima saa 96 kabla ya safari hawatakaa karantini,'' alisema.

Mara tu orodha ilipotolewa, Wakenya kwa haraka waligundua kuwa Tanzania haimo.

Siku ya Jumatatu tarehe 27 mwezi Julai, Rais Uhuru Kenyatta alitoa kauli ambayo haikuilenga Tanzania moja kwa moja kuwa Kenya haifichi idadi ya watu wenye maambukizi ya Covid-19.

''Sisi tuko wazi na tunajua fika kuwa ugonjwa huu upo tofauti na majirani zetu ambao wanauficha ukweli huu,'' alisema Rais Kenyatta.

Chanzo: BBC
Leo umefurahi kwa habari hii
 
Back
Top Bottom