Ndege ya Rais yagongwa na Gari la Usalama wa Taifa

What happened to the Plane? Well TGIF...

- Mafisadi wameiteka hawaiachilii hadi tuwaachilie

- Plane what plane? do we have presidential plane?

- Zanzibar hatuitumii ipasavyo kama sehemu ya Muungano - Mbunge wa CUF!

- Kwani tatizo lenu nini, ndege ni ya Rais nyinyi kinawasumbua nini - Waziri wa Habari

- Hii ndege ni kwa ajili ya safari maalum, kiwanja cha Songwe kikiwa tayari ndio mtaona umuhimu wake - Mbunge toka Mbeya

- Inafanyiwa matengenezo ili iongeze fleet ya ndege za ATC kusafirisha ma VIP. Itaanza safari za Dodoma kabla ya mwisho wa Bunge, tunaomba bilioni 5 - Mkurugenzi ATCL akizungumza na Kamati ya Bunge.

- Tunasubiri ndege nyingine ya Waziri Mkuu ili zote mbili ziwe kama farasi ambao wanatumiwa pamoja - Rubani Mkuu

- Kama ilivyokwishasemwa, ndege hii haiendani na hadhi ya Rais wetu hasa kutokana na wadhifa wake mpya wa Mwenyekiti wa AU hivyo tunasubiri ile Airbus 320 toka Ujerumani - Membe

- Wananchi wasiwe na wasiwasi, sasa hivi ndege inafanyiwa matengenezo ya mwisho kujiandaa na safari ya USA. Lazima Rais wetu na yeye aende na usafiri wa uhakika - Chitalilo

- Iuzwe!? hawa wapinzani wamekosa hoja, hatuwezi kuuza raslimali za Taifa - Karamagi

- CCM inaupendeleo, na tunaushahidi kuwa tarehe 2 mwezi wa 4 ndege ilionekana uwanjani ikiwa na mizigo ya aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu. Tunaamini inatumiwa na mafisadi, tumeiongeza kwenye orodha ya mafisadi - Dr. Slaa
 
Jamani kwa anayejuwa idadi ya waliokwenda Egypt atusaide? Wengine hatujui so inakuwa ngumu kujenga hoja. Please kwa anayejuwa idadi hiyo amwage hizo data. Thanks.
 
Nimesikia asubuhi katika power breakfast, kuna jamaa katuma ujumbe kuwa kuna gari imegonga ndege ya rais na dereva anashikiliwa na polisi. sina hakika kama ndio ndege hii mnayozungumzia au nyingine.
 
What happened to the Plane?

-
- Iuzwe!? hawa wapinzani wamekosa hoja, hatuwezi kuuza raslimali za Taifa - Karamagi

- CCM inaupendeleo, na tunaushahidi kuwa tarehe 2 mwezi wa 4 ndege ilionekana uwanjani ikiwa na mizigo ya aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu. Tunaamini inatumiwa na mafisadi, tumeiongeza kwenye orodha ya mafisadi - Dr. Slaa

This two are the quotes of the day!

Asha
 
Kuna mwenye taarifa inaendeleaje? Nani anaitumia kwa wakati huu? Iko salama? Na iko salama kiasi gani? Muungwana ameitumia lini mara ya mwisho? Matumizi yake yana tija kwa taifa?

Nina hamasa ya kuelewa nini kinaendelea. Hatukuuziwa mbuzi kwenye gunia?

Usalama wa rais wetu una umuhimu mkubwa kwetu kama watanzania!
Hii ndege ilikuwa imepaki wapi?
 
Hiyo ndege na mikasa ya Balali..Sasa ilimpa lifti wakati Rais anaitumia..Na sasa inatumika kubeba mizigo yake kumpelekea wapi huko aliko?
Ama usikute ni ndege yake Rais alimwazima.
Na hapo kwa Karamagi kusema eti ni Rasilimali ya Taifa ni vituko kabisa!
Ndio maana kweli hatuna viongozi! Ni swa na mtu kukipenda kiatu chako kuliko hata nyumba yako!
Utaweza vipi kusema kwa moyo wote kuwa ndege ni rasilimali ya Taifa na huku rasilimali zenyewe zilizokuwezesha kununuwa ndege hiyo ukiwa hata huziweki kwenye mahesabu ya rasimali za taifa in terms of respecting and utilizing them for the people's benefits?
Si ni sawa na kununua kiwi ambayo gharama yake ni bei ya viatu vipya pea elfu?
 
Ilipogongwa hiyo mizigo ya Ballai ilikuwa ndani ama imeshaletwa Marekani?
Iligongwa ikiwa barabara gani?
Ya bibi TITI?
Na je mara ya mwisho kutumika ilikuwa ni lini?
Je mara baada ya Ballali kupewa lifti kwenye ndege hiyo na kufanya mazungumzo ya siri na rais wakati akitokea Dodoma huku akibishana na Rais kama ajiuzulu ama wafanye nini...Je imeshatumiwa toka wakati huo?
Je kama ndege hiyo ni ya serikali...Ni nani anayepanga ratiba zake?
Na ratiba ya kubeba mizigo ya Ballali nani aliitowa?
 
imegongwa leo na kwa mujibu wa Dr ilikuwa na mizigo ya balali tarehe 2 mwezi wa 4! mwaka labda mwanakijiji anaweza kutusaidia.
 
Masikini huyo dereva, isijekuwa ajali ya kawaida na hata kama ndege ilikuwa mbovu tutaambiwa imeharibiwa na huyo jamaa!

"Finding yourself at wrong place at wrong time!"
 
Masikini huyo dereva, isijekuwa ajali ya kawaida na hata kama ndege ilikuwa mbovu tutaambiwa imeharibiwa na huyo jamaa!

"Finding yourself at wrong place at wrong time!"

Sasa kuna excuse nzuri sana hapa. Huyo jamaa aliyegonga hiyo ndege amelitia hasara kubwa taifa letu. NI lazima afungwe kifungo cha maisha, kutokana na uzembe wa kutojali mali za taifa. Adhabu kali ili iwe funidhso kwa wengine. I guess this is how it will go. This is us jamani, huyu jamaa anaweza kuwa mhalifu kuliko Chenge na Azizi.
 
Kumbukeni usemi usemao "kwenye miti hakuna wajenzi"
Uchumi tunao lakini twaukalia tuu.
 
Mkuu Ndege ipo salama salmini,ila inasemekana JK haitumii kwasababu eti Mlango wake ni Mfupi Mno,
Mlango ni mfupi kwasababu ilikuwa ni kwa ajili ya Rais Mkapa

JK ni mrefu kiasi,hujigonga kichwa.

Pole sana nami nashauri inunuliwe yenye mlango mrefu

...kwahiyo watu wa usalama wameshauri asiitumiye,kama utakumbuka yale magari madogo yaliyonunuliwa (lexus)kwa matumizi ya W.Mkuu nayo yaligundulika kuwa hayafai kwani nafasi ya Miguu ilikuwa ni finyu sana...."Ila waligundua tatizo hilo baada ya kufanya Manunuzi!"

Tupo tayari kula nyasi JK apate ndege yenye mlango mrefu. WATANZANIA TUTALIWA KWA STYLE TOFAUTI TOFAUTI HADI TUISHE.
 
ni hivi hiyo ndege ilikuwa imepaki sehemu yake na hilo gari ni la usalama wa taifa lilikuwa linarudi nyuma baada ya kumaliza shughuli za kusafirisha wageni. kuliendelea mjadala mkubwa eti kwa nini ndege imepaki pale, hawa wenzetu bwana badala ya kujiuliza wao kwa nini gari limeingia uwanjani. haya jamani habari ndio hiyo.
 
I love Tanzania...

For the last 6 months... we have the endless topic to discuss, EPA, BOT, Aircraft for President, Madini...

Of course it is not a problem to discuss, but the bad thing is that we have forgotten other issues... as if, once we clear the EPA, BOT, etc... then the country will be reach.


On the other side, after muafaka... CUF have decided to start another agenda and I assure you... this will be the main agenda in General Election 2010... "Whether Zanzibar is a Country/Nation/States" etc.

Ndio hivyo tena wanasiasa wanatupiga bao, badala ya kutusaidia kulima zaidi, kuzalisha.... zaidi... wanatuletea mambo ambayo hayatusaidii
 
Nimesikia asubuhi katika power breakfast, kuna jamaa katuma ujumbe kuwa kuna gari imegonga ndege ya rais na dereva anashikiliwa na polisi. sina hakika kama ndio ndege hii mnayozungumzia au nyingine.
Haya ndugu yangu, umetegua kitendawili changu! Hahaha... I knew it! Sasa kama ikigongwa na hata kunguru inahesabika kama ajali, itakuwaje kwa kugongwa na gari?

Only in Bongo! Kazi kwenu TISS
 
Kubwa zaidi ambalo mimi binafsi siwezi kulisahau ni the fact kwmba ndege hiyo ilitumika kumpa Ballali lifti kutoka Dodoma akiwa na Rais mwenyewe

Nina wasiwasi na hiyo fact yako bwana Mkubwa Mushi kwa sababu taarifa zilizopo ni kuwa ndege hii haiwezi kutua kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma. Ilielezwa ilipofika kuwa ina uwezo wa kutua kwenye viwanja vitano tu Tanzania namely; Mwalimu Julius Nyerere (Dar), KIA, Zanzibar, Mtwara na Mwanza.
Huko Dodoma ilifikaje na kutuaje ili kumpa lift Ballali?
 
Tanzania hatuna matatizo ya pesa wala anything, tuna uongozi mbovu tu maana leo ukipigiwa mapesa yanayotumika kwa safari tu za maofisa wa serikali nje ya nchi yetu utalia machozi ya damu,

Hivi unajua Egypt walienda wangapi? Ngoja tuwaombe wabunge waulize hili swali kabla bunge halijaisha!, yaani serikali yetu inatumia hela ngapi kwa ajili ya safari za nje za maofisa wetu kwa mwaka, japo huu tu ambao haujaisha!

Mzee FMES,

Tatizo jingine kubwa la Tanzania ni ni mishahara kwa wafanyakazi wa serikali. Hii imesababisha wafanyakazi wote including Mawaziri kuwa wanategemea sana safari both within and outside the country. Nilibahatika kufanya kazi serikalini kwa miezi kadhaa nikachoka wenyewe kwa jinsi watu wanavyopigania safari. Safari Tanzania ni njia moja wapo ya wafanyakazi kujiongezea kipato, period.
 
Back
Top Bottom