Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 374,453
- 867,150
Hebu tumsome Trevor kwanza kisha tuendelee na mjadala
Bwana Yesu aliweza kuulisha umati wa watu elfu tano pekeyake.... Leo hii watu elfu tano ndio wanamlisha mtu mmoja.
Sina tatizo kabisa na taasisi za kidini ambazo zinewekeza kwenye huduma za kijamii kama elimu afya, lishe na vituo vya misaada mbalimbali bila kusahau yatima, walemavu wazee, wajane, watoto wa mitaani na vituo vya sober house nk... Hivi ni vituo na taasisi ambazo hata unapotoa sadaka zaka ama misaada yako una amani kuwa unaenda inaenda kuwasaidia wahitaji.
Tunapomtolea Mungu matoleo yetu kwa njia ya fedha na vitu mbalimbali, hivi haviendi mbinguni bali husaidia kufanya kazi ya Mungu kwa kuwasaidia wenye uhitaji kisha ndio uwape neno. Tunapowahubiria watu imani zetu ni lazima tuhakikishe wana mahitaji ya msingi kama afya lishe elimu nk na kama hawana tufanye mikakati thabiti ya kuwapatia..... Hapo wanaweza kutusikiliza na kutuelewa.
Nina tatizo moja kubwa kwa hawa Mitume manabii na wahubiri wenye vituo binafsi vya kidini., ambao kutwa kuchwa kazi yao ni moja tuu... Kuwakamua waumini na waamini wao pesa na vitu, wanakusanya mamilioni ya zaka na sadaka na kujinufaisha binafsi na familia zao n a marafiki zao.... Zaidi ya hapo hawahusiki wala kujali matatizo mengine yote ya waumini wao, zaidi ya kutakiwa kuchangia kila huduma inayotolewa kwenye kituo husika.
Hawa wahubiri binafsi duniani ni mojawapo ya kundi linaloongoza kwa ukwasi na utajiri duniani... Wanashindana kwa magari nyumba ndege meli na vitu mbalimbali vya thamani kubwa na gharama, huku waumini wao wakizidi kutaabika.
Kuna huyu ndugu yetu naye wiki hii katupia picha za jet lake la billion mbili na ushee eti ni kwa ajili ya kueneza injili duniani...... Mungu anamuona.
Hiyo ndege itatua viwanja vingapi Tanzania!? Gharama za kuihudumia je? Hivi angeteua mikoa walau mitano na kila mkoa akawekeza kiasi cha million mia 5 hivi kwenye huduma za kijamii kama elimu afya lishe vituo vya sober house na yatima si ingekuwa bora mara million kuliko ndege ambayo itafaidisha kikundi kidogo cha watu? Kwanza angesaidia pakubwa tatizo la ajira lakini pia waumini na wasio waumini nao wangefaidika na huduma husika naye angepata thawabu kwa Mungu.
Kutuambia ndege ya kifahari ya billion 2 ni kwa ajili ya kueneza injili ni kudanganyana kiwango cha lami