Baadhi ya sifa za manabii wa uongo

Baadhi ya sifa za manabii wa uongo

a sinner saved by Christ

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2017
Posts
3,781
Reaction score
4,330
Ni ngumu sana kuwatofautisha manabii WA UONGO na manabii WA KWELI mana hata shetani hujigeuza malaika na wote wanatumia jina la YESU na wanafanya miujiza kwa kutumia jina la YESU.

Mt 7:22
Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi?
Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu.

BAADHI YA SIFA ZA MANABII WA UONGO
1. NENO LA MUNGU.
Kati kati ya mahubiri yake atakuchanganyia na mafundisho ambayo yapo kinyume na NENO LA Mungu la BIBLIA(ni muhimu kulijua NENO/Biblia na kulifuata NENO linavyosema sio mahubiri ya mwanadamu,SHIKA NENO/BIBLIA.

2. KUMTUMAINIA na KUMTEGEMEA YESU...nabii WA Kweli ,lazima atakujengea Imani Yako umtegemee Yesu,napenda kumnukuu mch Laizer (RIP) mikutano yake alikuwa anapenda kusema,usiseme ni Laizer ameniponya sema ni YESU amekuponya sio Mimi Laizer,pia alikuwa anasema wote tumekutana hapa ni watumishi WA Mungu hata Mimi alikuwa anajiita mtumishi WA Mungu,akawa anasema wote sasa tuombe kwa YESU kila MTU aombe mana wote tumekuja kumuomba yeye na sisi wote ni watumishi WA Mungu.
Mtumishi WA Mungu WA KWELI atakuelekeza kwa YESU ,utukufu na heshima na SIFA atavielekeza kwa YESU.

NABII WA UONGO atakuelekeza kwenye utegemezi WA vitu(kama mafuta ya upako,maji ya upako,udongo WA upako)..au umtegemee yeye Yani ANACHUKua nafasi ya Yesu yeye au anakuelekeza utegemezi kwenye vitu VYA upako


3. MAOMBI YA KULIPIA
Mathayo 10:8
Ponyeni wagonjwa, fufueni wafu, takaseni wenye ukoma, toeni pepo. Mmepewa bure, toeni bure.Maombi ya KULIPIA maombi ya laki moja...n.k

4. ATAKUWA RAFIKI WA WENYE DHAMBI NA HATAKEMEA DHAMBI NA ATAHALALISHA DHAMBI.
Vitu AMBAVYO ni dhambi yeye atasema sio dhambi(ulevi,suruali kwa wanawake,ndoa za jinsia moja n.k yeye atasema sio dhambi,atavitolea ufafanuzi wake WA kutetea dhambi,MATENDO yake anaweza akawa mzinzi,muongozo,mfitini, masengenyo,mlevi n.k

Lakini atapendwa na wenye dhambi,injili ya KWELI inachoma UKWELI unauma,unaona manabii WA KWELI WA biblia walichukiwa na wafalme wenye dhambi,walikamatwa na kuweka magerezani,wengine walikatwa vichwa kwa kukemea movu..

6. ATAKUWA NA PEPO LA UTAMBUZI.
atakutabiria umezaliwa LINI,unaendelea kunywa soda gani.mana anakuwa na pepo la utambuzi , sasa YESU hawezi kumtuma Nabii akutabirie unakunywaga soda Gani unayoipendelea..usishangae vitu vyote anavyokutabiria vingi vitakuwa vya KWELI.(pepo la utambuzi)..lakini anaweza akawa MFARAKANISHI akakufarakanisha na ndugu zako,atakwambia ndugu Yako fulani mfano mama mkwe WAKO ndiye mbaya WAKO(anatengeneza uadui KUVUNJA familia,KUVUNJA UMOJA na maelewano)
Mt 5:9
Heri wapatanishi; Maana hao wataitwa wana wa Mungu.
Hata kama ni KWELI mama mkwe WAKO ndiye anayetumiwa na shetani kukufanya UBAYA,bado hatakiwi kukwambia mama mkwe WAKO ndiyo mbaya WAKO.
mana hapo ADUI YENU ni SHETANI,siyo uadui wa wanafamilia kuwachonganisha ndugu badala kuwapatanisha.
usipende kutaburiwa tabiriwa na mitume na manabii.

7. ANAWEZA KUNENA KWA LUGHA
lugha ya kuzimu nayo inafanana kwa KIASI na lugha za malaika,kwa sababu shetani naye kabla hajawa shetani alikuwaga malaika,na alipotupwa DUNIANI,hakunyang'anywa uwezo baadhi,hasa WA kudanganya watu,(ni baba WA UONGO) ni HILA zake.
 
Umesema vema.Lakini hebu tujiulize,hivi hawa manabii wanajitambua kwamba.

Wanatumika na mwovu shetani?Hawa jamaa wamefumbwa macho ya kiroho wasitambue kuwa wanamtumikia shetani.Kwa sababu wanatumia jina la Yesu katika maombi na wakati mwingine wanahubiri vizuri.Tutafanya makosa tukiwalaumu badala yake Mungu awatokee kama alivyomtokea sauli wapate kumtumikia yeye badala ya ibilisi
 
Umesema vema.Lakini hebu tujiulize,hivi hawa manabii wanajitambua kwamba.

Wanatumika na mwovu shetani?Hawa jamaa wamefumbwa macho ya kiroho wasitambue kuwa wanamtumikia shetani.Kwa sababu wanatumia jina la Yesu katika maombi na wakati mwingine wanahubiri vizuri.Tutafanya makosa tukiwalaumu badala yake Mungu awatokee kama alivyomtokea sauli wapate kumtumikia yeye badala ya ibilisi

Manabii WA UONGO wengi wao walianza kwa KUMTUMIKIA Mungu KWELI, mwanzoni wengi wao waliitwa KUMTUMIKIA Mungu KWELI,ila KATIKATI ya safari Yao wakabadilika na kuanza KUMTUMIKIA SHETANI kwa sababu mbali mbali,mana shetani pia anawa ahidi ana wavutia kwa mali mafanikio ya DUNIANI.Ni wachache sana ambao toka mwanzo walianza wakijua kuwa watakuwa manabii WA UONGO ila wengi walianza na Mungu(Rohoni) wakamalizia mwilini wakakengeuka wakaasi,wakifikiri wamesimama wakaja wakaangukia kumtumikia SHETANI.
Ukiwaombea wanaweza wakavunja maagano na kuzimu wakatoka...sema inakuwa ni ngumu kuwatoa HUKO kwa sababu wame asi wakiwa wanajua DHAMBI ZA MAKUSUDI WAMEASI..

ila KWA MUNGU yote yanawezekana yasiyowezekana kwa mwanadamu.

Mungu awaokoe manabii WA UONGO.
 
8.8.Manabii WA UONGO wengi wao mwanzoni walianza kwa KUMTUMIKIA Mungu KWELI, mwanzoni wengi wao waliitwa KUMTUMIKIA Mungu KWELI,ila KATIKATI ya safari Yao wakabadilika na kuanza KUMTUMIKIA SHETANI kwa sababu mbali mbali,mana shetani pia anawa ahidi ana wavutia kwa mali mafanikio ya DUNIANI.Ni wachache sana ambao toka mwanzo walianza wakijua kuwa watakuwa manabii WA UONGO ila wengi walianza na Mungu(Rohoni) wakamalizia mwilini wakakengeuka wakaasi,wakifikiri wamesimama wakaja wakaangukia kumtumikia SHETANI.
Ukiwaombea wanaweza wakavunja maagano na kuzimu wakatoka...sema inakuwa ni ngumu kuwatoa HUKO kwa sababu wame asi wakiwa wanajua DHAMBI ZA MAKUSUDI WAMEASI..

ila KWA MUNGU yote yanawezekana yasiyowezekana kwa mwanadamu.

Mungu awaokoe manabii WA UONGO.
Tuwaombee manabii WA UONGO waokoke waache kutumika na ADUI.
AMEN.🙏🏿
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom