Ili ndege iruke (take off) kuna vitu vitatu Muhimu, cha kwamza ni Speed (take off speed) cha pili ni Mabawa (wing) ambayo husaidia ndege kupaa (lift) na cha tatu ni Mashine (Engine thrust) ambazo huchukua hewa mbele na kuirudisha nyuma kwa kasi kitendo hicho husababisha ndege kwenda mbele (thrust)...Ndege inarukaje kitoka ardhini..Rubani anapopewa clearence toka kwa Air traffic control, huanza kuondoka kwa kasi (acceleration) ili kuweza kufikia take off speed, ndege inapofikia take off speed (TOS) au B2, Rubani hurudisha nyuma Control Stick, kitendo hiki hufanya mabawa madogo (flaps) kunyanyuka juu na kufanya upepo kuyalazimisha yarudi chini, kitendo hiki husababisha Pua ya ndege kunyanyuka juu kwa vile engine za ndege kwa wakati huo zipo kwenye maximum rotation, zina provide maximum thrust na kuisukuma kwende uelekeo wa pua ya ndege ulipoinuka, na hapo hapo upepo mwingine unaopita kwa kasi chini ya mabawa ya ndege huifanya ndege ianze kuelea na engine za ndege huisukuma kwenda juu, ndege inapaa....
Pia ieleweke kuwa ndege inapokuwa angani hukalia hewa kwa msaada wa mabawa yake, na kwa vile ipo speed, ndege inapopunguza speed sana chini ya kiwango husababisha upepo unaopita chini ya mabawa kuwa mdogo, na hivyo mabaya yanashindwa kutoa lift kubwa kwa ndege na ndege huingia kwenye kitu kinachoitwa kwa kitaalam.. Aero-Dynamic-Stall, yaani ndege hupoteza lift na kuanguka kama Jiwe...mara nyingi hutanguliza Pua.....eg ajali za Ethiopia Air line, Air France nk
Sent using
Jamii Forums mobile app