Resilience
JF-Expert Member
- Jan 4, 2023
- 879
- 4,125
Viongozi wa Tanzania wanakiburi sana, wanakamatwa kwa rushwa na tuhuma nyingine za maadili lakini uwezi kusikia wamejiuzulu. Wanasubiri hadi Mh. Rais awatumbue jambo ambalo ni dharau kwa mamlaka. Kujiuzulu ni Ishara ya kuomba radhi na kukaa pembeni ni Ishara ya kufungua milango usafishwe au ukaangwe
Kuna mkurugenzi wa Sumbawanga kafikishwa mahakamani lakini hakuwahi kujiuzulu. Kuna huyu DAS kutuhumiwa kuiba mafuta lakini hakuna Sehemu unamsikia akiwajibika. Anamsubiri MH. Rais amtoe na akikaa kimya maisha yanasonga bila kujali kama wale waliopo chini yake bado ataweza kuwasimamia?
Jana Makamu wa Rais akiwa Mwanga anabaini Mkurugenzi ametoa kazi ya ukandarasi kwa mtu asiye na qualifications; utetezi anasema wilaya haina mtaalamu wa ujenzi! Kwamba wataalamu na mainjinia waliojaa nchini wanakosa kushinda tenda? Unapata picha kabisa kwamba hapa lipo tatizo. Lakini hadi Mhe. Makamu wa rais anakuja kuliona liletatizo na kumhoji mkurugenzi je amechukua hatua gani ya uwajibikaji? Yupo kimya
Nini kinachopelekea kukosekana kwa uwajibikaji kiasi hiki nchini? Kwanini tufanye Madudu tusubiri Mh.Rais atauadhibu ? Leo hii hawa wote wanaotuhumiwa hakuna mamlaka inayoweza kuwahoji kwa sababu ni wateule wa Rais. Kuchelewa kwa maamuzi ya juu hakuwezi kuwaharibu ushahidi? Hadi watumishi wanaanza kurekodiana audio na video unadhani huyo mtu yupo vizuri na anaowaongoza?
Watanzania tujifunze kutubu tuache miyoyo migumu; dini zote zinasisitiza toba na toba ya mteule wa Rais ni kukaa pembeni unapoelekezewa tuhuma ambazo hata aliyekuteua akisikia ataelekza uhojiwe na kuchunguzwa.