Paul Makonda atoa onyo kali kwa viongozi wa chama na serikali wanaotembea vifua mbele bila kutimiza majukumu yao vyema kuwa hatawafumbia macho

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
15,262
9,714
Ndugu zangu Watanzania,

Katibu wa itikadi, uenezi na mafunzo wa CCM Taifa Mheshimiwa Mwamba Mwenyewe Paul Christian Makonda kijana jasiri kusini mwa jangwa la sahara ,akiwa Shinyanga mjini ametoa onyo kali sana na kalipio kali kwa viongozi wa serikali na watumishi wa chama wanaotembea vifua mbele Bila kutekeleza majukumu yao vyema na kusababisha wananchi kuichukia serikali ya CCM ,kwamba hatawavumilia wala kuwafumbia macho katika uenezi wake.

Amesema haiwezekani Mheshimiwa Rais anafanya kazi bila kupumzika katika kuwahudumia wananchi kwa kushirikiana na viongozi wakuu wengine halafu anatokea mtendaji au mtumishi mwingine huko wa serikali au chama anashindwa kutimiza na kutekeleza majukumu yake.

Ameendelea kusema kuwa haiwezekani yeye mwenezi wa chama Taifa anazunguka na kutembelea mikoa 20(ishirini) bila kupumzika halafu huko mitaani kuna mwenezi wa CCM tawi au kata lakini hafahamiki mtaani kwake au katika kata yake na kuishia kuvaa tu shati la njano au kijani .amesema hiyo haitavumilika katika kipindi cha uenezi wake.

Nami namuunga mkono Mheshimiwa Makonda kabisa kwa asilimia zote kabisa. Kuna viongozi wengine wa serikali wanajifanya miungu watu,wakubwa kuliko chama ,wajuaji ,majeuri na kuanza kutoa lugha za kiburi na dharau.mara mwingine unamsikia akisema mimi bosi wangu ni fulani na fulani na kwamba hakuna mwingine wa kunipa maagizo au maelekezo.

Ukimsikiliza kiongozi huyu mpaka unamshangaa na kusikitika kabisa na kusema amepata wapi kiburi na jeuri hii? Anajielewa kweli au analeta dharau kwa chama? Unajiuliza hivi anajuwa kuwa chama ndicho kilichounda serikali na siyo serikali iliyounda chama? Hivi anajuwa na kufahamu kuwa chama ndicho kitakacho kwenda kuomba kura majukwaani na siyo yeye anayetoa maneno ya shombo na dharau? Hivi hajuwi kuwa chama ndicho kinachoandaa ilani na kwenda kuinadi kwa wananchi? Hivi hajuwi yeye asipotekeleza majukumu yake vyema kinachochukiwa ni chama kilichounda serikali?

Unachokuja kugundua ni kuwa ni ulevi wa madaraka ndio unaomsumbua na kule kujisahau baada ya kuwa mtu ameshiba na kusahau kwanini yupo hapo na amefikaje hapo. unajiuliza yaani mwenyekiti wetu tu wa chama Taifa anaheshimu sana viongozi wa chama hata ngazi ya mkoa sembuse huyu anayekuwa ameteuliwa serikalini? Unajiuliza hivi kama siyo kiburi na kukosa hekima na busara unaanzia wapi kuongea ongea maneno ya namna hiyo hadharani?

Unapata wapi hicho kiburi? Unataka kuonyesha kwamba wewe ndio mbabe? Au kwamba wewe una akili nyingi sana? Au kwamba wewe ni msomi sana? Au kwamba aliyempendekeza huyo hana akili na alikosea? Wewe ni nani mpaka umdharau kiongozi wa ngazi ya juu ya chama?

Ni lazima kila mmoja aelewe kuwa chama ndio mwamvuli wetu sote Wana CCM ambao tunapaswa kuulinda kwa jasho ,machozi na damu. Ni lazima tujuwe kuwa hakuna aliye mkubwa ndani ya chama hata kama upo serikalini umeteuliwa na Rais .kama wewe unajiona ni mkubwa kuliko chama na viongozi wa chama basi tafuta chama chako kagombee ndio upeleke kiburi chako na dharau lako huko ,halafu uone waliokujaza upepo kama watakufuata au kuwa na wewe mgongoni mwako.

Chama ndio kila kitu. Tumeona namna Mheshimiwa Rais wetu mpendwa,makamu wa Rais, waziri mkuu namna walivyo wanyenyekevu kwa chama chetu.tumeona namna viongozi mbalimbali katika taasisi mbalimbali namna wanavyokiheshimu chama chetu na viongozi wake.sasa wewe ni nani hadi uanze kutoa lugha za kuonyesha kuna mgawanyiko au kwamba kiongozi fulani hafai au wewe una akili sana na mjuaji sana? Kwanza nani kakwambia kuwa chama na serikali vinashindana? Nani na umewahi kuona wapi viongozi wa chama na Serikali wakitunishiana misuli?

Ni lazima kila mmoja ajuwe chama chetu ni kikubwa na ndicho kilichounda serikali,ni lazima chama kinapoomba majibu kutoka serikalini kipewe ushirikiano.sasa wewe umeteuliwa serikalini ili usaidie utekelezaji wa ilani yetu ,sasa unaanzeje kutokipa ushirikiano chama na viongozi wake? unataka iwaje? Usipowasikiliza wenye duka unawezaje kuendelea kusema unauza duka? Utauza duka la nani wakati unawadharau wamiliki wa duka walikuweka hapo?

Paul Makonda chapa kazi kwa kwenda mbele. Chama kipo na wewe na Mheshimiwa mwenyekiti wetu yupo bega kwa bega na wewe na ndio maana alikupendekeza na kuridhiwa na chama,makamu wa Rais, waziri mkuu wapo na wewe na serikali yote. atakayetaka kukukwamisha ajuwe anakikwamisha chama na anamkwamisha mwenyekiti wetu ambaye ni Rais wetu.hivyo atatoka yeye na kukaa pembeni na kukiacha chama chetu kikishirikiana na serikali yetu katika kuwahudumia wananchi.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Katibu wa itikadi, uenezi na mafunzo wa CCM Taifa Mheshimiwa Mwamba Mwenyewe Paul Christian Makonda kijana jasiri kusini mwa jangwa la sahara ,akiwa Shinyanga mjini ametoa onyo kali sana na kalipio kali kwa viongozi wa serikali na

0742-676627.
Hivi yeye Bashite ndiye aliyewateua? Au aliwapa kazi?

Si na afanye kazi za Chama!
 
Ndugu zangu Watanzania,

Katibu wa itikadi, uenezi na mafunzo wa CCM Taifa Mheshimiwa Mwamba Mwenyewe Paul Christian Makonda kijana jasiri kusini mwa jangwa la sahara ,akiwa Shinyanga mjini ametoa onyo kali sana na kalipio kali kwa viongozi wa serikali na

0742-676627.
Hongera sana mkuu. Lkn kazi hii ikimtumikia aliekuumba utakuwa umefanya jambo kubwa sana
MALARIA 2
03000040
 
Ndugu zangu Watanzania,

Katibu wa itikadi, uenezi na mafunzo wa CCM Taifa Mheshimiwa Mwamba Mwenyewe Paul Christian Makonda kijana jasiri kusini mwa jangwa la sahara ,akiwa Shinyanga mjini ametoa onyo kali sana na kalipio kali kwa viongozi wa serikali na watumishi wa chama wanaotembea vifua mbele Bila kutekeleza majukumu yao vyema na kusababisha wananchi kuichukia serikali ya CCM ,kwamba hatawavumilia wala kuwafumbia macho katika uenezi wake.
Kijana fanya kazi achana na uchawa na kujipendekeza,Mwanadamu hana future yako
 
Kati ya serikali na chama kipi kinachotangulia? Nani mkubwa kati ya chama na serikali? Nani anayekwenda kuomba kura kwa wananchi?
kuna utaratibu wa kiserikali wa chama kuisimamia serikali na sio anavyofanya bashite
Chama kinapata taarifa za kiutendaji wa serikali kupitia Ilani inayowasilishwa na Waziri Mkuu kupitia Mkutano Mkuu wa Chama huko na Rais ndio Mwenyekiti kama wanaona kuna mtendaji hatekelezi majukum yake wanaweza kuishinikiza kamati kuu itengue nafasi yake
Lakin sio Bashite kuja kutoa amri kwa viongozi kwa kigezo cha ukatibu uenezi
 
Mheshimiwa Makonda yupo kwa niaba ya chama na anafanya kazi ya kukisemea chama. Fahamu ya kuwa Mheshimiwa Makonda ni mjumbe wa vikao vyote vya juu unsvyovifahamu wewe
 
kuna utaratibu wa kiserikali wa chama kuisimamia serikali na sio anavyofanya bashite
Chama kinapata taarifa za kiutendaji wa serikali kupitia Ilani inayowasilishwa na Waziri Mkuu kupitia Mkutano Mkuu wa Chama huko na Rais ndio Mwenyekiti kama wanaona kuna mtendaji hatekelezi majukum yake wanaweza kuishinikiza kamati kuu itengue nafasi yake
Lakin sio Bashite kuja kutoa amri kwa viongozi kwa kigezo cha ukatibu uenezi
Hao watendaji wakitoa taarifa za uwongo, kuna shida chama kikienda au mtu akienda kwenye chanzo cha taarifa?
 
Ndugu zangu Watanzania,

Katibu wa itikadi, uenezi na mafunzo wa CCM Taifa Mheshimiwa Mwamba Mwenyewe Paul Christian Makonda kijana jasiri kusini mwa jangwa la sahara ,akiwa Shinyanga mjini ametoa onyo kali sana na kalipio kali kwa viongozi wa serikali na watumishi wa chama wanaotembea vifua mbele Bila kutekeleza majukumu yao vyema na kusababisha wananchi kuichukia serikali ya CCM ,kwamba hatawavumilia wala kuwafumbia macho katika uenezi wake.

Amesema haiwezekani Mheshimiwa Rais anafanya kazi bila kupumzika katika kuwahudumia wananchi kwa kushirikiana na viongozi wakuu wengine halafu anatokea mtendaji au mtumishi mwingine huko wa serikali au chama anashindwa kutimiza na kutekeleza majukumu yake.

Ameendelea kusema kuwa haiwezekani yeye mwenezi wa chama Taifa anazunguka na kutembelea mikoa 20(ishirini) bila kupumzika halafu huko mitaani kuna mwenezi wa CCM tawi au kata lakini hafahamiki mtaani kwake au katika kata yake na kuishia kuvaa tu shati la njano au kijani .amesema hiyo haitavumilika katika kipindi cha uenezi wake.

Nami namuunga mkono Mheshimiwa Makonda kabisa kwa asilimia zote kabisa. Kuna viongozi wengine wa serikali wanajifanya miungu watu,wakubwa kuliko chama ,wajuaji ,majeuri na kuanza kutoa lugha za kiburi na dharau.mara mwingine unamsikia akisema mimi bosi wangu ni fulani na fulani na kwamba hakuna mwingine wa kunipa maagizo au maelekezo.

Ukimsikiliza kiongozi huyu mpaka unamshangaa na kusikitika kabisa na kusema amepata wapi kiburi na jeuri hii? Anajielewa kweli au analeta dharau kwa chama? Unajiuliza hivi anajuwa kuwa chama ndicho kilichounda serikali na siyo serikali iliyounda chama? Hivi anajuwa na kufahamu kuwa chama ndicho kitakacho kwenda kuomba kura majukwaani na siyo yeye anayetoa maneno ya shombo na dharau? Hivi hajuwi kuwa chama ndicho kinachoandaa ilani na kwenda kuinadi kwa wananchi? Hivi hajuwi yeye asipotekeleza majukumu yake vyema kinachochukiwa ni chama kilichounda serikali?

Unachokuja kugundua ni kuwa ni ulevi wa madaraka ndio unaomsumbua na kule kujisahau baada ya kuwa mtu ameshiba na kusahau kwanini yupo hapo na amefikaje hapo. unajiuliza yaani mwenyekiti wetu tu wa chama Taifa anaheshimu sana viongozi wa chama hata ngazi ya mkoa sembuse huyu anayekuwa ameteuliwa serikalini? Unajiuliza hivi kama siyo kiburi na kukosa hekima na busara unaanzia wapi kuongea ongea maneno ya namna hiyo hadharani?

Unapata wapi hicho kiburi? Unataka kuonyesha kwamba wewe ndio mbabe? Au kwamba wewe una akili nyingi sana? Au kwamba wewe ni msomi sana? Au kwamba aliyempendekeza huyo hana akili na alikosea? Wewe ni nani mpaka umdharau kiongozi wa ngazi ya juu ya chama?

Ni lazima kila mmoja aelewe kuwa chama ndio mwamvuli wetu sote Wana CCM ambao tunapaswa kuulinda kwa jasho ,machozi na damu. Ni lazima tujuwe kuwa hakuna aliye mkubwa ndani ya chama hata kama upo serikalini umeteuliwa na Rais .kama wewe unajiona ni mkubwa kuliko chama na viongozi wa chama basi tafuta chama chako kagombee ndio upeleke kiburi chako na dharau lako huko ,halafu uone waliokujaza upepo kama watakufuata au kuwa na wewe mgongoni mwako.

Chama ndio kila kitu. Tumeona namna Mheshimiwa Rais wetu mpendwa,makamu wa Rais, waziri mkuu namna walivyo wanyenyekevu kwa chama chetu.tumeona namna viongozi mbalimbali katika taasisi mbalimbali namna wanavyokiheshimu chama chetu na viongozi wake.sasa wewe ni nani hadi uanze kutoa lugha za kuonyesha kuna mgawanyiko au kwamba kiongozi fulani hafai au wewe una akili sana na mjuaji sana? Kwanza nani kakwambia kuwa chama na serikali vinashindana? Nani na umewahi kuona wapi viongozi wa chama na Serikali wakitunishiana misuli?

Ni lazima kila mmoja ajuwe chama chetu ni kikubwa na ndicho kilichounda serikali,ni lazima chama kinapoomba majibu kutoka serikalini kipewe ushirikiano.sasa wewe umeteuliwa serikalini ili usaidie utekelezaji wa ilani yetu ,sasa unaanzeje kutokipa ushirikiano chama na viongozi wake? unataka iwaje? Usipowasikiliza wenye duka unawezaje kuendelea kusema unauza duka? Utauza duka la nani wakati unawadharau wamiliki wa duka walikuweka hapo?

Paul Makonda chapa kazi kwa kwenda mbele. Chama kipo na wewe na Mheshimiwa mwenyekiti wetu yupo bega kwa bega na wewe na ndio maana alikupendekeza na kuridhiwa na chama,makamu wa Rais, waziri mkuu wapo na wewe na serikali yote. atakayetaka kukukwamisha ajuwe anakikwamisha chama na anamkwamisha mwenyekiti wetu ambaye ni Rais wetu.hivyo atatoka yeye na kukaa pembeni na kukiacha chama chetu kikishirikiana na serikali yetu katika kuwahudumia wananchi.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
Joka la kibisa, kawaida hutumika katika maonyesho na burudani tu. Halina athari zozote zile hasi katika uwanja wa vita, na pia kwa mahasimu wake.
 
Hao watendaji wakitoa taarifa za uwongo, kuna shida chama kikienda au mtu akienda kwenye chanzo cha taarifa?
ni sehemu ndogo sana ya wananchi anayohangaika nayo Makonda pengine asilimia 0.5 watu wana matatizo ya kijamii na kiuchumi mengi mno,suluhisho sera,katiba,mifumo iangaliwe upya.
 
Back
Top Bottom