Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,813
- 11,991
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akishiriki Maadhimisho ya Siku ya kupambana na Rushwa Afrika, leo Julai 11, 2023 jijini Arusha.
===
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema moja ya vikwazo vikubwa vya maendeleo barani Afrika ni pamoja na janga la rushwa ambalo linadhoofisha mifumo ya kitaasisi na kuathiri mipango na mikakati ya kujikomboa kiuchumi.
Rais Samia amesema hayo leo wakati wa kilele cha maadhimisho ya Siku ya Mapambano dhidi va Rushwa Barani Afrika na maadhimisho va utekelezaji wa miaka 20 ya Mkataba wa Umoja wa Afrika wa Kuzuia na Kupambana na Rushwa yaliyofanyika AICC.
Aidha, Rais Samia amesema viongozi wote barani Afrika hawana budi kuimarisha ushirikiano katika mapambano dhidi ya rushwa.
Vile vile, Rais Samia amewataka viongozi kutafakari na kuchambua kwa dhati masuala ya rushwa ili kubainisha changamoto au vikwazo vya mapambano hayo na kuchukua hatua muafaka.
Kwa upande mwingine, Rais Samia amesema Serikali inaendelea kuimarisha Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kibajeti na kimfumo ikiwemo kuanzisha taasisi zinazosimamia utawala bora na haki za binadamu nchini
Rais Samia pia amesema Serikali imewekeza zaidi katika matumizi va mifumo va
TEHAMA inayosaidia kupunguza mawasiliano ya ana kwa ana katika kutoa huduma kama michakato ya zabuni, usajili wa biashara na namba ya mlipa kodi ili kupunguza mianya ya rushwa.
Kupitia Divisheni ya Mahakama Kuu inayosikiliza kesi za washtakiwa wa makosa ya rushwa kubwa, Serikali imeokoa na kudhibiti matumizi va fedha vasivostahili va zaidi ya Shilingi bilioni 139 kuanzia mwaka wa fedha 2019/ 20 hadi 2021/ 22

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi wa Taasisi mbalimbali, Wanafunzi pamoja na Wananchi wakati wa Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Mapambano dhidi ya Rushwa Barani Afrika
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Kamishna wa Polisi (CP) Salum Hamduni kuhusu kazi mbalimbali ambazo Taasisi hiyo inafanya kwenye Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Mapambano dhidi ya Rushwa Barani Afrika.
Wasanii wa Kikundi cha ngoma za asili kutoka Zanzibar Kibati wakitumbuiza kwenye Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Mapambano dhidi ya Rushwa Barani Afrika tarehe 11 Julai, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea Tuzo kutoka Bodi ya Ushauri ya Kupambana na Rushwa Afrika iliyowasilishwa na Makamu Mwenyekiti wa AUABC Mhe. Pascoal Antonio Joaquim
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akinyanyua juu Tuzo kutoka Bodi ya Ushauri ya Kupambana na Rushwa Afrika mara baada ya kukabidhiwa wakati wa Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Mapambano dhidi ya Rushwa Barani Afrika