tisa desemba
JF-Expert Member
- Nov 13, 2011
- 434
- 115
WanaJF nisaidieni tafadhali:
- Hivi Canada, Australia na New zealand nd ni nchi huru?
- Kuna tofauti gani kati ya kupata uhuru na nchi kuwa jamhuri?
1. ni huru.
uhuru ni hali ya kujitegemea kimaamuzi (kujiondoa katika utegemezi), kufanya mambo yako bila kuingiliwa.
2. kupata uhuru ( soma maana ya uhuru hapo juu)
jamhuri ni mfumo/aina ya serikali ambayo wananchi wanakuwa na haki ya kuchagua viongozi wao (uongozi sio wa kurithi), mara nyingi serikali hizi huongozwa na rais (aliyechaguliwa na watu).
hitimisho, canada, australia na new zealand ni huru ila zimeamua kuchagua mfumo wa serikali wa kidominioni ambapo waziri mkuu anakuwa mkuu wa serikali na malikia/mfalme wa uingereza anakuwa mtawala wa nchi.