Nchi yetu inaitwa Tanganyika

Nchi yetu inaitwa Tanganyika

mimi sio mtanganyika,
sikuzaliwa Tanganyika,
maana ya neno Tanganyika, siijui,
Tanganyikailitoka wapi, sijui,
ilibatizwa jina na nani, sijui

nilizaliwa Tanzania,
nilizaliwa Afrika
nilizaliwa duniani
nlizaliwa na mwanadamu

kwa hiyo;

mimi ni mtanzania
mimi ni mwafrika
mimi ni mdunia
mimi ni mwanadamu

maana ya Tanzania, najua
maana ya Afrika, najua
maana ya Dunia, najua
maana ya mwandamu, najua

nawauliza wazanzibari,
nini maana ya Zanzibari,
nani aliipa jina Zanzibari,
kwa nini wajivunie uzanzibari?
kwa nini wasijivunie utanzania?

Shairi lako zuri lakini halina internal connectivity!
 
Ni kitu cha ajabu sana kuwa na nchi moja yenye mambo yanayofanana na mithili ya kinyonga.

Mawaziri wa Tanganyika wanaitwa mawaziri wa jamhuri ya muungano, tunawaudhi wazanzibari

Mambo ya Tanganyika (yaani yasio ya muungano) yanapelekwa kwenye bunge la Tanzania, na wabunge wa zanzibar hawatoki nje wakati wa maamuzi.

Baraza la mawaziri linapozungumzia mambo ya Tanganyika, sijui kama mawaziri wasiohusika wanatoka nje.
Jimbo moja zanzibari lina wabunge wawili, Tanganyika mmoja.

Hii ni mifano tu ambayo inalilia Serikali ya Tanganyika, na bunge lake:help:

Ukiniambia nizungunzie mabadiliko ya katiba bila kuzungumzia muungano unanidanganya.

hapo Vipi wana JF:noidea:
 
Tungepata kundi kubwa la watanganyika wenye msimamo kama wako, wa Rev. Mtikila, wa G-55 na mimi na madai ya wazanzibari ya kupotea kwa mbia mwenza wa muungano basi kazi ingekuwa rahisi kuufahamisha umma wa Tanganyika.

Lakini kila nikifuatilia mijadala humu JF linalohusu kuirejesha Tanganyika ndani ya Muungano basi...list ya "influencial contibutors" kuanzia Mwanakijiji, Nguruvi3, JokaKuu, mkandara ,Miss judith wanasema hawataki hata kuisikia Tanganyika ikitajwa...Kasumba ya Mwalimu ya Tanzania ni nchi moja imewaingia vizuri na wanasahau kuwa Tanganyika na zanzibar zimeunganisha baadhi ya mambo tu. na kila sehemu kubakisha mambo mengi ya kila upande kuyashughulikia yenyewe...sasa vipi utabakisha mambo ya Tanganyika bila ya serikali na taasisi zake?

Wengine wanasema itakuwa ni kuitiA GHARAMA Tanganyika aka Tanzania bara.. hivi kuna kitu ambacho hakina gharama? Hasa kama kina manufaa? Na kama hakina manufaa/faida kwa nini tuwe nacho?, tuendelee kuking'ang'ania? Na hata kuzuia kisijadiliwe au kukosolewa?

Unajua, mimi hujiuliza kama Muungano wetu tungeu-model katika mfumo kama wa EAC basi hizi nchi nyengine zingekuja kujiunga nasi badala ya kuanzisha EAC mpya na kweli Muungano wetu ungekuwa wa kupigiwa mfano duniani. Lakini miaka 47 imepita sasa na hakuna nchi nyengine iliyotamani kuyeyuka ndani ya Muungano kama ambavyo Tanganyika imeyeyuka na kwa Sasa juhudi tunazofanya kuiyeyusha Zanzibar kwa kuelekea serikali moja.

Kuna watu wanapenda kusema Muungano wetu is unique...mimi sioni hii uniqueness isipokuwa naona utapeli tu na mazingaombwe au changa la macho. sijui itatuchukua tena miaka 47 kujua kuwa tunakawilisha na kujiongezea matatizo badala ya kuwa na ujasiri na kukabiliana na uhalisia wa siasa za kimuungano wa nchi huru!!???
 
Ni kitu cha ajabu sana kuwa na nchi moja yenye mambo yanayofanana na mithili ya kinyonga. Mawaziri wa Tanganyika wanaitwa mawaziri wa jamhuri ya muungano, tunawaudhi wazanzibari Mambo ya Tanganyika (yaani yasio ya muungano) yanapelekwa kwenye bunge la Tanzania, na wabunge wa zanzibar hawatoki nje wakati wa maamuzi. Baraza la mawaziri linapozungumzia mambo ya Tanganyika, sijui kama mawaziri wasiohusika wanatoka nje. Jimbo moja zanzibari lina wabunge wawili, Tanganyika mmoja. Hii ni mifano tu ambayo inalilia Serikali ya Tanganyika, na bunge lake:help: Ukiniambia nizungunzie mabadiliko ya katiba bila kuzungumzia muungano unanidanganya. hapo Vipi wana JF:noidea:
. Binafsi mi namkumbuka mtikila ka harakati zake, wengi walimuona kama mropoka ovyo, lkn sasa vp.
 
Tungepata kundi kubwa la watanganyika wenye msimamo kama wako, wa Rev. Mtikila, wa G-55 na mimi na madai ya wazanzibari ya kupotea kwa mbia mwenza wa muungano basi kazi ingekuwa rahisi kuufahamisha umma wa Tanganyika.

Lakini kila nikifuatilia mijadala humu JF linalohusu kuirejesha Tanganyika ndani ya Muungano basi...list ya "influencial contibutors" kuanzia Mwanakijiji, Nguruvi3, JokaKuu, mkandara ,Miss judith wanasema hawataki hata kuisikia Tanganyika ikitajwa...Kasumba ya Mwalimu ya Tanzania ni nchi moja imewaingia vizuri na wanasahau kuwa Tanganyika na zanzibar zimeunganisha baadhi ya mambo tu. na kila sehemu kubakisha mambo mengi ya kila upande kuyashughulikia yenyewe...sasa vipi utabakisha mambo ya Tanganyika bila ya serikali na taasisi zake?

Wengine wanasema itakuwa ni kuitiA GHARAMA Tanganyika aka Tanzania bara.. hivi kuna kitu ambacho hakina gharama? Hasa kama kina manufaa? Na kama hakina manufaa/faida kwa nini tuwe nacho?, tuendelee kuking'ang'ania? Na hata kuzuia kisijadiliwe au kukosolewa?

Unajua, mimi hujiuliza kama Muungano wetu tungeu-model katika mfumo kama wa EAC basi hizi nchi nyengine zingekuja kujiunga nasi badala ya kuanzisha EAC mpya na kweli Muungano wetu ungekuwa wa kupigiwa mfano duniani. Lakini miaka 47 imepita sasa na hakuna nchi nyengine iliyotamani kuyeyuka ndani ya Muungano kama ambavyo Tanganyika imeyeyuka na kwa Sasa juhudi tunazofanya kuiyeyusha Zanzibar kwa kuelekea serikali moja.

Kuna watu wanapenda kusema Muungano wetu is unique...mimi sioni hii uniqueness isipokuwa naona utapeli tu na mazingaombwe au changa la macho. sijui itatuchukua tena miaka 47 kujua kuwa tunakawilisha na kujiongezea matatizo badala ya kuwa na ujasiri na kukabiliana na uhalisia wa siasa za kimuungano wa nchi huru!!???
Nonda,'
Umesahau kunijumuisha na mimi katika hilo kundi. Tanganyika tayari imo ndani ya Tanzania sasa mnataka Tanganyika tofauti ya nini? Rais wa Jamhuri ya Mwungano wa Tanzania ni rais wa Tanganyika vile vile, sasa mnataka muwe na marais wawili? Hivi mkishapata rais wa Tanganyika, huyu rais wa Jamhuri ya Mwungano atakuwa na kazi gani? Atakuwa ceremonial tu kama rais wa Israel? Tanganyika imo ndani ya Tanzania, na mara nyingi nikisafiri kutoka Dar kwenda makwetu najisikia nimo ndani ya Tanganyika.
 
Hii ichi inaongozwa na watu wenye akili za kuku ni shida sana kuwaeleza haya wakakuelewa. Mazoea yamewalevya!
 
Kuanzisha Serikali ya Tanganyika ndani ya Muungano kutaua Muungano na hatimaye kuiua Tanganyika mpya! Mnashabikia maangamizi yenu wenyewe! Poleni sana!
 
Mkuu.

Sikuweza kuwakumbuka wote..nashukuru umejitokeza na unisamehe kwa kukusahau katika orodha.
Mkuu. sujiu kwanza kama utakubaliana na mimi kuwa Tanzania ni nchi mbili. Hii ndio iliyonifanya niseme kuwa tungekuwa na Model ya muungano wa EAC au EU..hii ingetoa nafasi kwa kila nchi ambayo ingependa kujiunga ingetimiza vigezo ingeingia katika muungano wetu.
sasa kwa kuififilisha Tanganyika ndani ya muungano nchi gani itapenda isisikike baada ya kuingia ndani ya muungano...nani zaidi ya mtikila anatumia jina Tanganyika? Hii kusema unajisikia umo Tanganyika ni jambo jipya..wengi husema Tzbara.

Lakini rais wa Muungano angetakiwa kushughulia mambo ya muungano tu...na rais wa tanganyika akashughulikia mambo ya tanganyika na rais wa zanzibar akashughulikia mambo ya zanzibar...au huelewi kuwa kuna mambo ya muungano na mambo ambayo si ya muungano kwa kila upande? na hivyo kuweka mipaka iliyo wazi ya mamlaka na kiutawala.
 
Usidharau watu simply kwa kuwa wana mtizamo tofauti na wa kwako! Washabiki wa u-Tanganyika bahati mbaya sana haelezi faida zitakazopatikana mara baada ya kuanzisha Serikali tatu! Je, ufisadi utatoweka? Je, umaskini utaondoka? Je, vifo vya mama wajawazito na watoto chini ya umri wa miaka 5 vitapungua? Kama hakuna majibu, basi sioni haja ya hiyo Serikali ya Tanganika ambayo nahisi itaongeza matatizo badala ya kupunguza!
 
Kuanzisha Serikali ya Tanganyika ndani ya Muungano kutaua Muungano na hatimaye kuiua Tanganyika mpya! Mnashabikia maangamizi yenu wenyewe! Poleni sana!
Mkuu.
Badala ya kuendeleza scare tactics, ungetusaidia kuelewa vipi haya maangamizi yatakuja.

Ikiwa maangamizi yatakuja,maangamizi gani zaidi ya umasikini, maradhi, chuki zinazojengeka na "kikombe cha babu" baada ya miaka 47 ya muungano?

Unafahamu Rwanda, Kenya walipata maangamizi na leo wametia akili mpya?..sasa kama kuboresha mfumo,muundo wa muungano
ni mangamizi basi ni kinyume chake,kukataa kuufanyia marekebisho ndio kutakakoleta maangamizi.
 
Nonda,

..mimi napinga muundo wa serikali 3 kwasabu naamini utatubebesha wa-Tanganyika mzigo mkubwa wa gharama, na pia si jibu la ambitions za wa-Zanzibar kuwa na madaraka makubwa zaidi ya kujiamulia mambo yao.

..mimi napendekeza tuachane na muungano badala yake twende kwenye kuwa wanachama wawili tofauti ktk jumuiya ya Afrika Mashariki.

..vilevile tunaweza kuwa na commision ndogo ya ushirikiano baina ya Tanganyika na Zanzibar itakayo-deal na masuala ya fedha na mashirkiano ya kibiashara baina ya pande mbili. tena katika suala la fedha/monetary union tunaweza kuwa mfano kwa nchi nyingine za Afrika Mashariki.

..masuala ya uraia na ukaazi pia yanaweza kushughulikiwa kwa kuwapa nafasi wananchi waliohama toka nchi zao za asili[Tanganyika na Zanzibar] kuamua uraia wanaoutaka.
 
Mkuu.

Sikuweza kuwakumbuka wote..nashukuru umejitokeza na unisamehe kwa kukusahau katika orodha.
Mkuu. sujiu kwanza kama utakubaliana na mimi kuwa Tanzania ni nchi mbili. Hii ndio iliyonifanya niseme kuwa tungekuwa na Model ya muungano wa EAC au EU..hii ingetoa nafasi kwa kila nchi ambayo ingependa kujiunga ingetimiza vigezo ingeingia katika muungano wetu.
sasa kwa kuififilisha Tanganyika ndani ya muungano nchi gani itapenda isisikike baada ya kuingia ndani ya muungano...nani zaidi ya mtikila anatumia jina Tanganyika? Hii kusema unajisikia umo Tanganyika ni jambo jipya..wengi husema Tzbara.

Lakini rais wa Muungano angetakiwa kushughulia mambo ya muungano tu...na rais wa tanganyika akashughulikia mambo ya tanganyika na rais wa zanzibar akashughulikia mambo ya zanzibar...au huelewi kuwa kuna mambo ya muungano na mambo ambayo si ya muungano kwa kila upande? na hivyo kuweka mipaka iliyo wazi ya mamlaka na kiutawala.
Nonda,
Nakusikia mkuu. Lakini ni mambo gani hayo ya muungano ambayo yatamshughulisha rais wa muungano full time? Nadhani rais wa Jamhuriya muungano anaweza kuyashughulikia masuala yote ya muungano na ya Tanganyika bila kumwongezea kazi. Tanganyika haikufifia ndani ya Tanzania. Nikiwa Zanzibar najua niko Zanzibar, mwenzetu katika muungano. Nikiwa Tabora, Mwanza, Bukoba, Musoma, najisikia niko nyumbani ndani ya Tanganyika ambayo kuna wanaodhani imefifilishwa. Ni hizo tofauti zinazonifanya nitambue kuwa Tanganyika ipo, kwa wale wanaotaka Tanganyika iwepo, na Tanzania inang'ara, kwetu sisi tunaojiona Watanzania. Hatuhitaji kuongeza vyeo na bureucracy ili kujusikia kuwa maslahi ya Tanganyika (Tanzania bara) yanalindwa.
 
Hii ichi inaongozwa na watu wenye akili za kuku ni shida sana kuwaeleza haya wakakuelewa. Mazoea yamewalevya!

Asante kwa uelewa huo. Maana umefika wakati sasa wa kufanya mabadiliko ya haja.
 
Kimsingi Tanganyika inahitajika na Tanzania Inahitajika..Kwa nini Matunda ya Wazanzibari wale wenyewe lakini Matunda ya Tanzania tule wote...Je wanapoanzisha EAC Hakuna Gharama? We Need Tanganyika,We need Tanzania and We KEEP Zanzibar
 
Nonda,
Nakusikia mkuu. Lakini ni mambo gani hayo ya muungano ambayo yatamshughulisha rais wa muungano full time? Nadhani rais wa Jamhuriya muungano anaweza kuyashughulikia masuala yote ya muungano na ya Tanganyika bila kumwongezea kazi. Tanganyika haikufifia ndani ya Tanzania. Nikiwa Zanzibar najua niko Zanzibar, mwenzetu katika muungano. Nikiwa Tabora, Mwanza, Bukoba, Musoma, najisikia niko nyumbani ndani ya Tanganyika ambayo kuna wanaodhani imefifilishwa. Ni hizo tofauti zinazonifanya nitambue kuwa Tanganyika ipo, kwa wale wanaotaka Tanganyika iwepo, na Tanzania inang'ara, kwetu sisi tunaojiona Watanzania. Hatuhitaji kuongeza vyeo na bureucracy ili kujusikia kuwa maslahi ya Tanganyika (Tanzania bara) yanalindwa.

Mkuu.
Kuna ile inayoitwa hati ya muungano..imeweka mambo 11 kuwa ni mambo ya muungano.
Kama rais wa Syshelles au zanzibar anaweza kufanya kazi full time kwa nini Rais wa mambo ya muungano asiweze kuwa na kazi full time?
Lakini je sisi hatutamani kuona nchi nyengine zinajiunga na muungano wetu? mfumo tunaoutumia uko rigid na hivyo unawafukuza nchi nyengine kujiunga na ndio pia tunawasikia Zanzibar wanataka ku-opt out kama haiwezekani kubadilisha muundo. Au muungano wetu umekuwa designed ubakie kuwa ni Muungano wa Tanganyika na Zanzibar tu?
 
Unajua nini? Tatizo la Wazanzibari ni kwamba badala ya kuwalaumu viongozi wao kwa kutowaletea maendeleo, wanalaumu muungano.
Na viongozi wao wanaona heri muungano ulaumiwe na wenyewe wapewe pasi kumbe uzembe wa viongozi hao hao ndio umepelekea Zanzibar kuwa pale ilipo leo. Badala ya kukaa pamoja tutafute ufumbuzi katika matatizo ya elimu, afya, uchumi kwa pamoja inakuwa rahisi kwao kulaumu muungano kana kwamba bila muungano wangekuwa mbali sana. Hii si kweli kabisa. Tena mimi naamini bila muungano wasingekuwa na tofauti yeyote na Comoro. Na angeweza kutokea mamluki yeyote pale kama alivyofanya Denard miaka ile na kujitangazia Zanzibar kuwa himaya yake. Rwanda na Burundi wanatamani kujiunga nasi licha ya matatizo tuliyo nayo na Wazanzibari. Umemsikia Raza?
Kuna wakati alikuwa mstari wa mbele kubeza muungano lakini leo baada ya kutambua kuwa biashara zake zimeshamiri kwa sababu ya muungano ameanza kuwalaumu wale wanaotaka muungano uvunjike.
 
Kweli watu ubinafsi na uchoyo vimewajaa!, hivi mnajua tofauti ya muungano na ushirikiano?, Tunachotaka sio kuua muungano na kuweka ushirikiano bali ni kuondoa zile chembe chembe za ushirikiano zilizokuwepo na kuwa na muungano kamili! Hapa namaanisha kwamba, kuwa na serikali ndani ya serikali nyingine sio muungano!, tuwe na serikali moja ya muungano ila ndani tuwe na states mbili!, kama ilivyo marekani! Tufumue kabisa mfumo wa serikali wa kiingereza na tuwe na ule wa marekani ambao kila state inawakilishwa kivyake ndani ya serikali kuu! SERIKALI 1 NDIO SULUHISHO NA NDIO MUUNGANO SAHIHI!, VINGINEVYO TUTAJIDANGANYA TU KUWA TUNA MUUNGANO WAKATI TUNA USHIRIKA!
 
Nonda,

..mimi napinga muundo wa serikali 3 kwasabu naamini utatubebesha wa-Tanganyika mzigo mkubwa wa gharama, na pia si jibu la ambitions za wa-Zanzibar kuwa na madaraka makubwa zaidi ya kujiamulia mambo yao.

..mimi napendekeza tuachane na muungano badala yake twende kwenye kuwa wanachama wawili tofauti ktk jumuiya ya Afrika Mashariki.

..vilevile tunaweza kuwa na commision ndogo ya ushirikiano baina ya Tanganyika na Zanzibar itakayo-deal na masuala ya fedha na mashirkiano ya kibiashara baina ya pande mbili. tena katika suala la fedha/monetary union tunaweza kuwa mfano kwa nchi nyingine za Afrika Mashariki.

..masuala ya uraia na ukaazi pia yanaweza kushughulikiwa kwa kuwapa nafasi wananchi waliohama toka nchi zao za asili[Tanganyika na Zanzibar] kuamua uraia wanaoutaka.
JokaKuu.

Mimi naona kuwa kama kuufanyia mabadiliko muungano huu (ambayo yataridhisha pande zote mbili) haiwezekani basi haya uliyoyasema hapa nakubaliana nayo kama second choice!

Kama haya ndio kuuboresha muungano na kuondoa kero za muungano basi iwe hivyo ili wananchi wapate nafasi kushughulikia vita ya kupambana na "magamba na sumu".

Lakini mkuu usisahau kujenga vitu vizuri haiwezekani bila ya kuingia gharama....kwa upande mmoja, kuifufua EAC imeongeza complications za muungano wetu..kuna mambo mengi ya EAC ambayo hayamo katika mambo ya muungano..wala hakuna free pass kwa Zanzibar kama ilivyo kwa Tanganyika kujiwakilisha huko ni lazima wapitie serikali ya muungano.

Inawezekana kuwa hii solution unayoipendekeza ni nzuri kukabiliana na hali kama hii lakini kama kuna njia bora si vibaya kuangaliwa pia... mimi nilifikiria kuwa tuandae mechanism ambayo Zanzibar itaweza kujiwakilisha kwa uhuru mkubwa na njia moja ni kwa kukubali kuwa wao ni wabia sawa wa muungano wetu, mengine ni rahisi kufuatia na kurekebisha kwa kupitia majadiliano ya pande za muungano. Sijafahamu kuwa Zanzibar hawataki Muungano, nililofahamu wanataka haki itendeke na kubanwa kupungue.

Ingawaje Hong kong na China si mfano maridhawa hasa lakini labda tungefuata system ya uhusiano kama wao. two systems ,one country..ingawaje bado mimi sijashawishika kuwa Tanzania ni nchi moja.. ingawaje tunajaribu kujenga picha ya kuwa Zanzibar ni "sehemu" ya Tanzania badala ya kusema kuwa ni mwanachama au mbia wa muungano.
China na Hong kong wao ni nchi moja. Lakini sio Tanganyika na Zanzibar...Hili la usanii wa jina Tanzania tumeshalijadili sana. Jina la muungano ni Muungano wa Tanganyika na Zanzibar pitia hati ya muungano.
 
Unajua nini? Tatizo la Wazanzibari ni kwamba badala ya kuwalaumu viongozi wao kwa kutowaletea maendeleo, wanalaumu muungano.
Na viongozi wao wanaona heri muungano ulaumiwe na wenyewe wapewe pasi kumbe uzembe wa viongozi hao hao ndio umepelekea Zanzibar kuwa pale ilipo leo. Badala ya kukaa pamoja tutafute ufumbuzi katika matatizo ya elimu, afya, uchumi kwa pamoja inakuwa rahisi kwao kulaumu muungano kana kwamba bila muungano wangekuwa mbali sana. Hii si kweli kabisa. Tena mimi naamini bila muungano wasingekuwa na tofauti yeyote na Comoro. Na angeweza kutokea mamluki yeyote pale kama alivyofanya Denard miaka ile na kujitangazia Zanzibar kuwa himaya yake. Rwanda na Burundi wanatamani kujiunga nasi licha ya matatizo tuliyo nayo na Wazanzibari. Umemsikia Raza?
Kuna wakati alikuwa mstari wa mbele kubeza muungano lakini leo baada ya kutambua kuwa biashara zake zimeshamiri kwa sababu ya muungano ameanza kuwalaumu wale wanaotaka muungano uvunjike.

Mkuu.
kwa hili nakubaliana na wewe kwa asilimia 65%....katika post zangu nyengine nimesema kuwa Viongozi wa Zanzibar na "wabara" wanajificha nyuma ya muungano huku wakitugawia umaskini.
Viongozi Wazanzibar wanasema wanabanwa na muungano na "wabara" wanasema hakuna Tanganyika na hivyo wananchi wameachwa kuduwaa hawajui wamshike nani? wamdai nani maisha bora? Serikali ya muungano ni ya "wabara" na wazanzibar...unaona kizungu zungu hapo? Ni sawa na kukimbiza kivuli! au ghost!

mkuu..kila kitu kinaweza kuwa na faida na hasara..na werevu ni wale wanaofanya maamuzi kwa kuelekea kule ambako mizania ya faida ina uzito zaidi kuliko hasara....lakini faida ya mtu mmoja isiwe kipimo cha faida ya nchi au umma wote.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom