Gily Gru
JF-Expert Member
- Jul 4, 2016
- 7,798
- 20,743
ATHARI ZILIZOLETWA NA UKOLONI JUU YA DAMU, VICHWA VYA WAZEE WETU
MZUNGU (Mkoloni) ni mtu mbaya sana na utawala wa kitumwa ulikuwa mbaya na kwani familia nyingi zilitengwa na wenzao na kupelekwa wasipokujua. Watoto walitengwa na wazazi wao, mume na mkewe kwa kweli inaonyesha ni uchungu kiasi gani babu zetu walipitia. Wanaume waliochukuliwa kwenda kufanywa watumwa ughaibuni, walichukuliwa na KUHANISIWA ili wasiwazalishe wanawake wa huko. Ndugu zetu wakiwa huko nchi za ugenini walipigwa MNADA na KUNUNULIWA kama bidhaa. Mambo haya waliyoyapitia ni ya uchungu mkubwa mno kuyaelezea, hakuna atakayefurahia kumkuta
MWARABU (Mkoloni) ni mtu mbaya sana kwani ni moja yapo ya watu wabaya kuleta utumwa, nakumbuka nilisimuliwa na bibi, waliwagawanya watu katika matabaka. Ilifika kipindi watu wakawa wanauza watoto wao kwa fitina za waarabu. Mfano pwani (Tanga mpaka Tabora maeneo haya yalijulikana kama pwani kipindi cha ukoloni) mtoto alikuwa ni mali ya mjomba, ikimaanisha bba hakuwa nanguvu zaidi ya mjoimba. Wajomba wengi waliuza watoto wao kwa waarabu ili wapate ujira. Kwa watoto waliokuwa na damu ya kiarabu wao na waarabu wenyewe walikuwa wezi wakubwa, tena waliiba watu wengi hususani watoto. Usipomchunga mwanao basi atanyakuliwa na hawa waarabu na mamluki yake na kwenda kuuzwa kama bidhaa.
Wazee wetu walijazwa hofu ndani ya mioyo yao ili wauone mzungu kama mungu, wengine waliwazania ni mungu. Wakoloni waliwafanya mababu na mabibi zetu wajione wako chini yao, kuwafanya kutekeleza mambo ya kikoloni (watu kuuza watoto wao wenyewe kwa Waarabu) na kumwabudu mkoloni kama miungu dunia. Bibi zetu WALIBAKWA sana tena sio mbele ya kadamnasi, walifanywa kama chombo cha starehe, wanawake walizalilishwa na kuzalishwa na watawala hawa wa mabavu. Ilipelekea wengine kutengwa na familia zao na kuteseka sana kwa uchungu mkubwa pale walipozalishwa na wakoloni.
Walipigwa fimbo kama wanyama, na kushurutishwa kufanya shughuli mbali mbali zenye kuwazalishia makoloni zikiwemo kulima mashamba ya wazungu. Mbali na hayo walinyimwa haki zao za kibinadamu mfano walishindishwa njaa bila kupewa chakula chochote, walifanyishwa kazi kupita uwezo wao wa kibinadamu, walitiwa chapa za alama kama wanyama n.k. Mababu zetu walitia sahihi mikataba ya kilaghai kwa shuruti na wengine kwa kupenda kuwauza wa-Tanganyika wenzao. Hapo unaona jinsi walivyotugawanya sisi wenyewe kwa wenyewe.
Hata baada ya kupata uhuru, dhambi ya utumwa haikukoma, ikaendelea kuwatafuna jamaa zetu kupitia UKOLONI MAMBOLEO. Nchi nyingi barani Africa hata baada ya uhuru bado ziliathirika na ukoloni mamboleo unaoendelezwa na watawala wenyeji. Tumeona wazungu wakipora utajiri wa nchi nyingi barani Afrika hata baada ya utumwai, hasa mafuta na madini. Ukoloni umeathiri FIKRA za ngozi nyeusi, ndo maana unaona watu wamekuwa wavivu kujiajiri, fitina, uvivu wa kufikiri nk. Je, kitu gani unaona tufanye kufuta ukoloni mamboleo jwa vizazi vyetu vinavyokuja?
Kuna watu wanajiona juhudi zao binafsi zilitupa uhuru, lakini harakati za uhuru zilianza toka kwa wote walipigana kutetea haki zao na familia zao (UHURU HAUKULETWA NA JUHUDI TANU PEKE YAKE). Shukrani zatu za dhati zinaenda kwa Chifu Mkwawa (1891 and 1894), Kinjekitile Ngwale kuwaunganisha watu katika vita vya Maji Maji (1905 – 1907), ma chifu wengi, taasisi za dini (WAKRISTU, WAISLAMU, DINI ZA KIJADI), na watu wote waliopigania uhuru kwa namna moja au nyingine. SHUKRANI ZA KIPEKEE zimwendee HAYATI MWALIMU NYERERE, kwa kuunganisha Tanganyika kuwa nchi moja yenye ushikamano mmoja pasipo UDINI, UKABILA, UKANDA, UBAGUZI WA RANGI N.K. Nawapongeza Maraisi wote waliopita na wa sasa kwa kufata nyayo hizi na kupiga kabisa chembe chembe hizi za chuki na kudumisha umoja wetu.
Kuna baadhi ya viongozi wa kipindi kile walitaka kudai uhuru wa maeneo yao binafsi na mfano mzuri ni Mangi Thomas Marealle. Kazi kubwa ilifanywa na Mwalimu J K Nyerere kuwaunganisha viongozi wa mikoa mbali mbali nchini Tanganyika na kuwaweka chini ya utawala mmoja. Isingekuwa juhudi na fikra za Mwalimu Nyerere basi kungekuwa na ushindani mkubwa sana kila mtu angevutia kwake. Kwa yeyote anayebeza kuwa yeye si MUASISI halali, mbona babu zao hawakupewa nchi watawale wao? Mbona babu zao hawakuunganisha Tanganyika? Kuna watu wengi walidai uhuru, kuna watu ndugu zao walidai uhuru kwa kiasi kikubwa leo hawako kutafuta ujiko. Mwalimu Nyerere hakudai uhuru wa wakatoliki, alidai uhuru wa wa-Tanganyika, hakupewa uraisi kwa sababu ya ukatoliki wake. Kwanza idadi ya WAKRISTU na WAISILAMU haikuzidi hata nusu ya WATANGANYIKA (wengi hawakuwa na dini za kuletewa).
Tahadhari: Naomba sana wana Tanzania wenzangu tupinge kwa sauti moja dhambi za kibaguzi; na yeyote anayepinga dhambi hizi aweke neno lake. Mimi siko hapa kubishana, kutukanana na mtu yeyote, ukoloni mamboleo umetawala fikra za watu wengi. Kupinga ukoloni mamboleo tena wanasiasa, kwa wasomi wanaojitafutia majina, wanaopayuka tu kuuharibu umoja wetu WAPE NENO LA KUJENGA. Swali, sio unakaa chini kila siku unawaza Tanzania imekufanyia nini, wewe umeifanyia nini Tanzania?