Nchi yetu inaitwa Tanganyika

Nchi yetu inaitwa Tanganyika

hapo kweli mnaleta topics ambazo 'zinahatarisha' muungano lakini inaonekana ndiyo dawa, japo ni chungu! Kama kweli Mwalimu aliashindwa kupata jina Tanganyika lilipotoka, alihita to consult others also! Kama ni makosa ya kihiostoria, ni budi kuyarekebisha kabla hayajaturekebisha.
Tatizo lenu watanganyika mumelala sana,yule nyerere alikuwa na uzee wake unamsumbua sumbua,na nyie mukamsikiliza sana mzee yule,uzee ule ndio ulokukandamizeni,alizeekea vibaya,iweje awavunjie utaifa wenu ? Hilo ni jukumu lenu,kifo cha tanganyika ni cha kujitakia wenyewe.
 
Inapendeza mtu kuwa great thinker. Nyerere hakuhitaji consultant kwa ajili ya jina la nchi, maana jina Tanganyika bila shaka linatokana na ziwa Tanganyika. Kwa nchi za jirani jina Kenya linatokana na mlima Kenya na Kongo linatokana na mto Kongo na kuna waliochakachua jina la ziwa Nyasa kuliita Malawi ili wahalalishe jina la nchi yao. Sina imani kuwa jina la ziwa lilitoka kwa wajerumani bali ni imani yangu kuwa walitafuta jina litakalokidhi maeneo ya nchi yetu pamoja na Rwanda-Urundi kwa pamoja ndipo wakaamua kutumia jina la ziwa lile. Hata ukanda wa ziwa kuna wazee wasiojua ziwa victoria bali 'Nyanza' kama linavyosomeka katika ramani ya wajerumani. Maadam palikuwepo na muungano kutoka Kagera hadi Ruvuma hapakuwa na taabu kutumia jina Tanganyika baada ya uhuru ambalo awali lilitumiwa na wakoloni. Na tukihitaji kulitumia sasa hatuhatarishi muungano kwa sababu wapo wanaotumia jina zanzibar na hakuna hatari yoyote kwa muungano.
 
Nafikiri kwa wakati huu kama utanikazania niiitwe mtanganyika nitakukatalia mimi ni Mtanzania, so baki na uzanzibar wako sisi tutaendelea na utanzania wetu usitutie ujinga. hamkawii kubadilika mara mtakapoona mtanzania anaendelea mtaomba turudiane so mimi nilizaliwa wakati wa Tanzania na nitaendelea kuwa mtanzania,
 
Mis judith weye utakua ni ccm. Maana hutamki wazi serikali 3 unababaisha tu eti ikiwa moja mbili au tatu wee nini wee?
 
Sikukazanii uitwe Mtanganyika, kwani hata mimi ni Mtanzania mwenzako. Tatizo linakuja pale unapokutana na Mzanzibari na ukataka kujipambanua. Kwa sababu ninyi wote ni watanzania, yeye akijiita mzanzibari wewe utajiita nani?
 
Mkuumara nyingi kisiasa huwa nakupinga lakini kwa hili tuko pamoja na nimekugonga senks na kukulike!
 
Tatizo lenu watanganyika mumelala sana,yule nyerere alikuwa na uzee wake unamsumbua sumbua,na nyie mukamsikiliza sana mzee yule,uzee ule ndio ulokukandamizeni,alizeekea vibaya,iweje awavunjie utaifa wenu ? Hilo ni jukumu lenu,kifo cha tanganyika ni cha kujitakia wenyewe.

Wewe umetokea wapi tena? Nyerere alikuwa mzee 1964?
 
watu wa dunia ya leo wanatazama mbele sio nyuma.

watu wanajiuliza juu ya uraia wa nchi mbili au zaidi, sisi tunajiuliza uraia wa nusu nchi!

watu wanazungumza namna ya kuvutia uwekezaji wa kimataifa, uondoshwaji wa masharti ya visa, sisi tunazungumzia kichefuchefu cha neno "bara" kwenye utambulisho wetu, tunataka turejee kwenye nchi mbili na kurudisha masharti ya passport na visa

watu wanahangaika na mazungumzo ya ushirikiano/uundwaji wa shirikisho, soko la pamoja, ushirikiano katika masuala ya sayansi na tekinolojia, umoja wa forodha, sarafu moja nk sisi tunazungumza namna ya kuvunja muungano!.

jambo la msingi la kujiuliza ni je, tunapiga hatua kimaendeleo au tunarudi nyuma? tunakwammishwa na jina hili tanzania, au ni kitu gani kinatukwamisha tusiendelee kwa kasi tuliyotazamia? kama hatupati maendeleo tunayohitaji kwa kasi tunayotazamia, je, tatizo ni nini, ni jina la Tanzania?

Miss Judith.

Umesema mengi mazuri katika mchango wako.
Lakini mengine umeyatoa nje ya "context"

Zaire imerudi katika jina lake la zamani...sijui wamerudi nyuma?

Lakini hapa wengi hawasemi turudi kwenye nchi mbili kwa maana ya utengano, nilivyowaelewa mimi.
Watanganyika wanataka jina Tanganyika litumike kwa sehemu ya iliyokuwa nchi ya Tanganyika kabla na sio Tanzania bara na pia yale mambo ambayo si ya muungano, yaitwe mambo ya Tanganyika badala ya kuitwa mambo ya Tanzania bara au wizara za mambo ya Tanzania bara. na wazanzibari wanahoji kupotea kwa Tanganyika. wao wanauliza wajadiliane na nani?

Kumbuka muungano huu si muungano wa kila kitu au jambo. Jikumbushe historia ya muungano.

Kwa hiyo malalamiko hasa yapo kwa sababu mbia mmoja wa muungano kapotea au kajipoteza. Inapotokea upande uliobaki unataka kuzungumza au kujadiliana tena kuhusu jambo lolote ajadiliane na nani?

Umetoa mfano wa nchi kuungana na kuondosha visa. kweli hili ni jambo zuri lakini pia wao wameweka utaratibu mzuri. kama mfano wa EU hawa wote ni europeans lakini kila european ana utambulisho mwengine kama ni mjerumani,mfaransa ,mgiriki au mbelgiji.
Majina ya nchi zao au utaifa wao haukufa na bado wamepiga hatua hizo unazosema.

Tatizo la kwetu ni usanii mwingi na utaratibu mbovu au misingi mibovu ya muungano tulionao. na kwa sababu "viongozi" hawataki kusikiliza vilio vya wananchi ndio wengine wanafikia kusema muungano uvunjwe lakini wengi wanataka iwekwe misingi ya muungano wa haki na usawa. na vilio hivi viko Tanganyika na Zanzibar.

Au wewe unaelewa muungano ulioua wanachama wake?
Au sisi kwa kuliua jina Tanganyika ndio tumepiga hatua za kwenda mbele zaidi ya hao unaoona wamepiga hatua kubwa kimaendeleo na ushirikiano?
 
Wewe ni mmoja kati ya wale walionielewa kwa nini nimeleta thread hii. Nia si kukataa muungano, bali kuturejesha utambulisho wetu halisi.
 
Mkuumara nyingi kisiasa huwa nakupinga lakini kwa hili tuko pamoja na nimekugonga senks na kukulike!

Huwa unanipinga kwa kudhani hakuna mwana CCM mwenye fikra za kimapinduzi ya ukweli.
 
Mis judith weye utakua ni ccm. Maana hutamki wazi serikali 3 unababaisha tu eti ikiwa moja mbili au tatu wee nini wee?

Wana msemo wao ati 1+1=2, haiwezi kuwa 3 wala 1!
 
Tanganyika haijawahi kufa kwani hata neno TANZANIA ni kifupisho cha maneno TANganyikaZANzibar(IA). Hayo maneno ya mwisho waliyaongeza tu kufanya jina litamkwe ki-pan african zaidi. Hivyo kimsingi huwezi kuongelea Tanzania bila kuzitaja Tanganyika na Zanzibar.

[TANganyika+ZANzIbAr
Na ikiwa wengine watalalamika kuwa kwa nini IA itoke katika jina Zanzibar, suluhisho hili hapa
TANg(A)ny(I)ka+ZANzibar
 
................ Mimi nina asili, na asli yangu ni Tanganyika

mi utanzania wangu ni wa kuzaliwa. wewe huo utanganyika wako uliutoa wapi? unaweza kuniambia maana ya neno tanganyika? unaweza kuiambia neno hilo tanganyika lilitokana na nini? na nani aliibatiza ardhi hiyo iitwayo tanganyika jina lake?

asante
 
REFER POST NO 62
Kisha na mimi nina swali kwako ambalo ukinijibu nitakujumuisha kwa ma-great thinkers miss Judith. Kama kunatokea kutokuelewana baina ya nchi zilizoungana inabidi pande mbili zikutane kujadiliana. Hizo pande mbili ni serikali au uwakilishi wa nchi hizo 2. Naomba unitajie hizo nchi mbili zinazopaswa kukaa na kuongea endapo kuna tatizo la muungano wa Tanzania. Natanguliza shukrani maana nakuaminia miss J kuwa utanijibu.
 
mi utanzania wangu ni wa kuzaliwa. wewe huo utanganyika wako uliutoa wapi? unaweza kuniambia maana ya neno tanganyika? unaweza kuiambia neno hilo tanganyika lilitokana na nini? na nani aliibatiza ardhi hiyo iitwayo tanganyika jina lake?

asante

Mara nyingi nilisoma coment za MISS JUDITH naona anaukataa utanganyika kwa hoja kua jina hilo lilibatizwa na wakoloni.

Hivyo nataka nikuulize Miss Judith unajua kua hata jina TANZANIA lilitolewa na mfaransa mmoja baada ya kusikia nchi mbili simeungana! sijui na hilo kwa tafsiri yako kama halitakua la kikoloni pia.

Kwa taarifa zaidi fuatilia nani alibatiza jina Tanzania,ukiachia kusikia tu kua limetokana na Muungano wa znz na T.nyka.

Ukishinwda niambie nikutafutie kwa ukamilifu mbatizaji wa jina hilo ambae pia ni mkoloni.
 
historia, nimesoma japo si sana inaonekana hukunielewa vizuri kwa vile post imekaakaa kaa shairi fulani hivi, laki my point is:

1. Tanganyika ni nchi iliyobuniwa na kubatizwa jina hilo na wakoloni

2. Tanzania ni nchi iliyobuniwa na kubatizwa jina hilo na wazalendo

3. mimi na wingine wenye umri usiofikia miaka 47, tumezaliwa Tanzania na sio Tanganyika

4. muungano ni kielelezo cha umoja wetu na licha ya mapungufu yake, ni bora kuliko kutengana

5. changamoto tuliyonayo ni kuondoa mapungufu yake, iwe ni kwa kuunda serikali moja, tatu au kubaki na mbili za sasa, vyovyote vile, muhimu tuondoe kero zinazohusiana na muungano

kilichotufanya tusindwe kuijenga Tanzania si muungano uliopo, bali masuala mengi tu tunayojadili hapa kila siku kama ufisadi nk. kwa hiyo hata tukiuvunja muungano, tutashindwa kuijenga Tanganyika pia kama hatutapambana na matatizo haya (ufisadi nk)

Unaweza kufumba macho, ukadhani Tanganyika haipo. Tanganyika haijafa. Hata mkiziba masikio. Kama si leo, kesho yaja, tutaidai nchi yetu.

Soma historia, Urusi ya zamani (USSR) iko wapi? Soviet Union - Wikipedia, the free encyclopedia
 
Mis judith weye utakua ni ccm. Maana hutamki wazi serikali 3 unababaisha tu eti ikiwa moja mbili au tatu wee nini wee?

KUWA CHE CHE MEA(C.C.M) SIO NDO KUTOTAKA SERIKALI 3. MI NI MCHECHEMEA LAKINI NATAKA HATA LEO KUWE NA SERKL 3 KWANI NAHISI UCHUNGU WA AJABU PALE MAMA YANGU ANAPO PATA TABU KUSEMA YEYE NI MTZ wakati si kweli YEYE NI MTANGANYIKA na MIMI NDIO MTANZANIA na BABA YANGU NI MZANZIBAR.
 
hata wamasai ,wanyamwezi, wasukuma na wengineo wanatanua tu zanzibar...usimuonee choyo mtu anadai haki yake just do the same dai haki yako ...taka kuwepo kwa katiba ya tanganyika na rais wa tanganyika na bunge la tanganyika na baadae ndio tuanze mambo ya muungano

lakini hawamiliki Ardhi..?!! hata hivo swala zima la kumiliki Ardhi serikali ya znz imetumia akili kweli.. la sivyo mngejengewa mabanda ya kitimoto kule ..tehehehe!!!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom