Nchi yetu inaitwa Tanganyika

Nchi yetu inaitwa Tanganyika

Aliyeizika Tanganyika si CCM. Ni Nyerere na ilikuwa kabla ya CCM kuzaliwa kwa miaka mingi sana, Tanzania ilianza mwaka 64. CCM ilianza lini?

Fikiri.

unawezaje kuitenganisha CCM na Nyerere? Yeye ndio aliizika Tanganyika lakini viongozi wa CCM waliofuatia walilijengea kaburi kwa zege nzito ili hata kama ikitokea imefufuka ikose pa kutokea huko kaburini.
Lakini saa imefika ya kulivunja kaburi na kuitoa Tanganyika yetu.
 
Yaani hii mada kwangu ni bora kuliko zote,we have to tell them (readers),that we need our country and we love it (TANGANYIKA).Kwa hiyo kuna haja ya kuanza kudai Tanganyika yetu kwa njia yoyote ile.Let us stand together and fight for that,our land, our origin is where we belong.Oooo my dear Tanganyika I love U, where u are?!!!!
 
Watanganyika ni waoga wa kila kitu. Kazi yao ni Domo reeeefu bila ya vitendo, maneno meeeengi vitendo vichache. Usishangae ndio maumbile yao, ndio maana wakaitwa Wadanganyika. Mtanganyika aliyebaki ni mmoja tu Mch. Mtikila. Wengine wote ni Nguvu mdomo tu. Eti waache wao wadai, itakayobaki ndio yetu. Pumbav. UMOJA NI NGUVU. Kila upande udai haki zake tuone kama haitorudi Tanganyika na Zanzibar. TUAMKE KUMEKUCHA HAKUNA KULALA. Wadanganyika.
hatuna haja ya kudai tanganyika yetu maana hatujabadilisha chochote,bendera,wimbo wa taifa vya tanzania vyote ni vya tanganyika,vazi la taifa kila kitu ni vya tanganyika ,kwa kifupi tanzania ni tanganyika,historia ya tanzania ni ya tanganyika ,labda nyie wa znz kama wanataka nchi yao maana ilivo sasa ni kama mkoa tu wa TZ.Watanganyika wenzangu wala msijishugulishe niaminini mimi hamna utamaduni wa tanganyika uliopotea eti kwa sababu ya kuwa Tanzania.
 
Ubaguzi utawamaliza! Hivi unajua Tanganyika ilikumuisha Rwanda na Burundi au Tanganyika ipi muitakayo?

nadhani unachanganya dhana ya Tanganyika na German East Africa. Tanganyika was there na GEA was there. Muda mfupi tuliokaa na jina letu ulikua mzuri na wa amani kuliko hii miaka arobaini na nane ya kuitwa kila neno baya na Wapemba.
Halafu mbona huu ubaguzi unaongelewaga pale tu Watanganyika wanaporaise? Au Wazanzibar wana nini hasa cha ziada?
 
muungano ni muhimu, ila muundo sio mzuri umatoa haki kwa upande mmoja zaidi..muundo wa serikali tatu ndio bora zaidi kama tunaupenda muungano na kuuhitahi..ila serikali moja ndio bora zaidi
 
Ingawa lengo sio kuvunja muungano lakini naomba tuwe na muuungano ulio na usawa kwa pande zote.UKISOMA KATIBA inasema kuwa rais wa Tanzania ndie atakaye simamia pia mambo ya bara, lakini sijawahi kuona bunge linalojadili mambo yasiyo ya muungano ya bara bila wazanzibari kuwepo. Je siku tukichagua Rais kutoka Zanzibar itakuwaje kwa mambo yasiyo ya muungano, Je Makamu wa Rais atapewa mamlaka ya kuunda serikali pamoja na bunge la bara lenye nguvu kisheria ya kusimamia mambo ya bara bila kuingiliwa na Rais wa Jamhuri ya muungano. Kama kweli tunaupenda muungano tuunde wa serikali Moja vinginevyo bila kumumunya mameno napenda kusema kuwa maoteo yangu yanaonesha kuvunjika kwa muungano hivi karibuni.
 
kwa tafsiri ya muungano,Tanganyika,ilipoteza autonomy yake baada ya muungano ila zanzibar haijapoteza
 
Jamani hakuna Muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar bali kuna ushirikiano tu wa baadhi ya nyanja tulizokubaliana. Muungano maanake mnashirikiana kwa kila kitu tena kwa usawa bila kujali huyu mkubwa na yule ni mdogo au huyu anacho yule hana.

Walioungana katika muungano huu ni TANU na ASP wakaja ni kitu yao ya magamba inayowatesa watanganyika na wazanzibari.

Muungano wa kweli ni kuwa na serikali Moja. Shirikisho la kweli ni kuwa na Serikali TATU. kinyume na hapo hakuna muungano wala ushirikiano.
 
historia, nimesoma japo si sana inaonekana hukunielewa vizuri kwa vile post imekaakaa kaa shairi fulani hivi, laki my point is:

1. Tanganyika ni nchi iliyobuniwa na kubatizwa jina hilo na wakoloni

2. Tanzania ni nchi iliyobuniwa na kubatizwa jina hilo na wazalendo

3. mimi na wingine wenye umri usiofikia miaka 47, tumezaliwa Tanzania na sio Tanganyika

4. muungano ni kielelezo cha umoja wetu na licha ya mapungufu yake, ni bora kuliko kutengana

5. changamoto tuliyonayo ni kuondoa mapungufu yake, iwe ni kwa kuunda serikali moja, tatu au kubaki na mbili za sasa, vyovyote vile, muhimu tuondoe kero zinazohusiana na muungano

kilichotufanya tusindwe kuijenga Tanzania si muungano uliopo, bali masuala mengi tu tunayojadili hapa kila siku kama ufisadi nk. kwa hiyo hata tukiuvunja muungano, tutashindwa kuijenga Tanganyika pia kama hatutapambana na matatizo haya (ufisadi nk)

haupo sahihi katika hayo maandishi niliyoyawekea rangi nyekundu
Tanga na Nyika ni aina ya samaki waliokua wakipatikana Ziwa Tanganyika(sina uhakika kama bado wanapatikana) na ndio jina Tanganyika lilipotokea na sio kweli kwamba wakoloni ndio walitoa jina la Tanganyika.
 
Vipi vizazi vitakavyokuja baadaye, navyo viwe na jina lake?? Nani, wapi jina lilikotoka is immaterial! cha msingi, je linaleta sense??
 
historia, nimesoma japo si sana inaonekana hukunielewa vizuri kwa vile post imekaakaa kaa shairi fulani hivi, laki my point is:

1. Tanganyika ni nchi iliyobuniwa na kubatizwa jina hilo na wakoloni

2. Tanzania ni nchi iliyobuniwa na kubatizwa jina hilo na wazalendo

3. mimi na wingine wenye umri usiofikia miaka 47, tumezaliwa Tanzania na sio Tanganyika

4. muungano ni kielelezo cha umoja wetu na licha ya mapungufu yake, ni bora kuliko kutengana

5. changamoto tuliyonayo ni kuondoa mapungufu yake, iwe ni kwa kuunda serikali moja, tatu au kubaki na mbili za sasa, vyovyote vile, muhimu tuondoe kero zinazohusiana na muungano

kilichotufanya tusindwe kuijenga Tanzania si muungano uliopo, bali masuala mengi tu tunayojadili hapa kila siku kama ufisadi nk. kwa hiyo hata tukiuvunja muungano, tutashindwa kuijenga Tanganyika pia kama hatutapambana na matatizo haya (ufisadi nk)

Swali kwako Ms Judith,kama kuna Tanzania ambayo ni Muunganiko wa Tanganyika na Zanzibar,kwa nini leo Zanzibar ipo na Tanganyika haipo? Mimi ni Mtanganyika piga ua!
 
haupo sahihi katika hayo maandishi niliyoyawekea rangi nyekundu
Tanga na Nyika ni aina ya samaki waliokua wakipatikana Ziwa Tanganyika(sina uhakika kama bado wanapatikana) na ndio jina Tanganyika lilipotokea na sio kweli kwamba wakoloni ndio walitoa jina la Tanganyika.

Tanga = sail, Nyika = wilderness, it is a natural name
 
Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alitabiri yote haya! Alisema kitu kama hiki:-

Baadaye watajitenga wakisema "sisi ni watanganyika, wao wazanzibari. Lakini mgawanyiko wao hautaishia hapo bali vile vile wazanzibari tena watasema, "sisi ni waunguja na wao ni wapemba". huku Bara/Watanganyika nao watasema, "Sisi ni wa kusini, wao ni wa kaskazini". Wataendelea mpaka watasema sisi ni wa moshi, wao ni wa Arusha.......
Itafika hatua watu watagawanyika mpaka kwenye ngazi ya familia. Mtaanza kusema sisi ni wazawa wa kwanza na wao wa pili. Sisi wa Baba na wao wa Mama. Tunapoelekea huku tutaanza "Sisi ni JF Premium Member, wao ni Junior Member na hawalipii.Yanayotuunganisha ni makubwa kuliko yanayotutenganisha.
 
historia, nimesoma japo si sana inaonekana hukunielewa vizuri kwa vile post imekaakaa kaa shairi fulani hivi, laki my point is:

1. Tanganyika ni nchi iliyobuniwa na kubatizwa jina hilo na wakoloni

2. Tanzania ni nchi iliyobuniwa na kubatizwa jina hilo na wazalendo

3. mimi na wingine wenye umri usiofikia miaka 47, tumezaliwa Tanzania na sio Tanganyika

4. muungano ni kielelezo cha umoja wetu na licha ya mapungufu yake, ni bora kuliko kutengana

5. changamoto tuliyonayo ni kuondoa mapungufu yake, iwe ni kwa kuunda serikali moja, tatu au kubaki na mbili za sasa, vyovyote vile, muhimu tuondoe kero zinazohusiana na muungano

kilichotufanya tusindwe kuijenga Tanzania si muungano uliopo, bali masuala mengi tu tunayojadili hapa kila siku kama ufisadi nk. kwa hiyo hata tukiuvunja muungano, tutashindwa kuijenga Tanganyika pia kama hatutapambana na matatizo haya (ufisadi nk)

Hiyo point yako namba 2 naona jaupo sahihi, japokuwa nyingi haupo sawa ila hii ndo kabisaaaaa. Wazalendo gani unaowazungumzia hapa kuwa wametoa jina hilo la Tanganyika? unadhani hao watu( Kama sikosei ni Julius na Karume tu) fikra zao hata kama ni uchwara zilikuwa zinatosha kuwakilisha mawazo na matakwa ya wananchi wengi?

Kumbuka kuwa kipindi hicho ni kwamba fikra za mwenyekiti wa CCM zilikuwa hazipingwi hata zikiwa ni mbovu kutokana na utaratibu mzima wa mfumo wa chama kimoja. Kwa sasa hivi tupo ktk mfumo wa vyama vingi ambao tunajisifia kuwa demokrasia inafuata mkondo (japo kinafiki nafik)i, kwanini tusiwape wananchi nafasi ya kutumia demokrasia na kujiamulia kama Muungano uendelee kuwepo au tuwe na Tanganyika yetu??

Kusema kweli NAIPENDA SANA TANGANYIKA KULIKO TANZANIA YENYE MIGOGORO ISIYOISHA JUU YA HUU MUUNGANO WA KINYONYAJI.
 
Tutabaki kuimba na kujinasibu na kujivunia kitu ambacho hakipo, Watanganyika tuchangamkeni tuitafute nchi yetu kwa nguvu zote wachana na idea za magamba.

Kweli sisi wanatushinda walaurojo(Wazenji), sasa hvi wao wanafanya kila hali kujipatia uhuru wao sisi tuko kimya.

(Na tarehe 26April watakuwa na mkutano mkubwa pale Lumumba school.
sorce: mzalendo.net)
 
nani mkeo ?
hii ndio sababu tunavunja huu unaoitwa muungano nia yenu mbaya watanganyika
 
mimi sio mtanganyika,
sikuzaliwa Tanganyika,
maana ya neno Tanganyika, siijui,
Tanganyikailitoka wapi, sijui,
ilibatizwa jina na nani, sijui

nilizaliwa Tanzania,
nilizaliwa Afrika
nilizaliwa duniani
nlizaliwa na mwanadamu

kwa hiyo;

mimi ni mtanzania
mimi ni mwafrika
mimi ni mwanadamu

maana ya Tanzania, najua
maana ya Afrika, najua
maana ya Dunia, najua
maana ya mwandamu, najua

nawauliza wazanzibari,
nini maana ya Zanzibari,
nani aliipa jina Zanzibari,
kwa nini wajivunie uzanzibari?
kwa nini wasijivunie utanzania?
Well said! Tujivunie Utanzania kwa vile unatokana na sisi wenyewe kwa hiari yetu wenyewe, na kwa malengo yetu wenyewe hata km kutokana na kasumba yao baadhi yetu wanataka kuukana na kujinasibisha na ukoloni, kwa kushupalia majina ya mapokeo ambayo hata maana yake hatujui
 
waziri mkuu alisema zanzibar si NCHI
WAZANZIBAR tunajua maana ya maneno yale. pinda anafahamu kuwa NCHI ya tanganyika Imeungana na NCHI ya zanzibar. lakini kwa makusudi kaamua kuwaeleza wazanzibar dhamira ya kuimeza NCHI yao.
bila ya kutafuna maneno karibuni hivi tanganyika itafungua balozi wake zanzibar na tutabakia majirani TU. BAADA YA KURA YA MAONI KUHUSU MUUNGANO amboyo kwa sasa tunaandaa matokeo yake. TANZANIA itakua hesemu katika historia ya nchi hizi mbili....tunavunja muungano and in this matter we are serious
''TANGANYIKA NI NDUGU ZETU WA DAMU SIO KISIASA WALA KIUCHUMI''
 
Baada ya miaka kadhaa ijayo kuna dhoruba kali lajatokea baharin kuna vsiwa vdogodogo vitafutika kabisa, watafiti wamethibitisha. Tufanye mpango wa ndg zetu wa zenj wapate eneo la kuwatosha maeneo ya shinyanga wakachunge.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom