Nchi inapokuwa na Waziri Mkuu mlalamikaji na mshangaaji bila kuchukua hatua zenye matokeo, shida iko wapi?

Criterion

JF-Expert Member
Jan 8, 2008
11,798
11,881
Ninaona waziri mkuu akianika madudu ya serikali kama raia asie na mamlaka. Anakuwa mtu wa kusoma uovu kwa kushangaa na kulalalmika, nikisha hakuna kinachoendelea juu ya maovu hayo. Tatizo ni kwamba hana uwezo?, si kazi yake?, hana nia thabiti zaidi ya propanganda za kisiasa? AU genge la uharibu linamzidi nguvu na hivyo kuishia kuguna na kuacha bora liende?

1. Mwaka jana aliongea wizi wa mabilioni ulifanyika hazina kwa muda mfupi baada ya kifo cha Mh. Magufuli. Baada yya hapo, hatukuona hatua yoyote ya kuonyesha uchungu wa uharifu huo hadi leo kimya. Hii inaashiria wizi wa kughushi malipo serikalini ni halali? Kama hazina ni wezi halali, report za CAG zian nguvu gani kama si matumizi mabaya ya fedha za umma?



Hii ni dalili kwamba hawa watu wamezoea na ni ilitakiwa overhauling ya hiyo ofisi. Lakine leo yako wapi?

2. Leo tena analalamika watu wamekaa china 60+days irrelevantly. Chunguzi hizi huchukua muda gani?



Inaonekana wanapomaliza kusema naye, yanaishia hapo.
Wizara ya fedha, haifai. Ifanyiwe mabadiliko.

3. Kuhusu matumizi ya balozi zetu, alipashwa hili aongee na mama ili aache kuzurura, badala yake atumie balozi zetu kuwasilisha na kusimamia agenda na maslahi ya taif ughaibuni badala ya kila mara barabarani.

Hii ni dhahiri kwamba baada ya mafisadi kushika hatamu, upigaji serkalini utakuwa umerudi pale pale. Watanzania wakakufa na maisha magumu, kdozi zikiwa katika viwango vya juu duniani, na atozo za matumizi juu!. My country Tanzania, nani atatuokoa?
 
Bila kusahau muongo. Huyu ndie alietuambia kaongea na raisi na ni mzima wa afya kumbe mwenzie keshakata moto kitambo.
Inawezekana kusema sema madudu bila hatua, ni namna ya kutaka kuwaaminisha watu kwamba mifumo yetu iko makini, kumbe chini a zuria kila kitu ni halali tu.
 
Viongozi wote wa serikali wanapaswa kujitathmini jinsi wanavyoendesha nchi kama ni sahihi ama la, hawajui wanamuumiza mtz kiasi gani kwa kusema madudu na hakuna hatua zinazochukuliwa
 
Ki ukweli inakatisha tamaa na kuuzunisha kama sio kustaajabisha.......nadhani viongozi wengi tuliowapa dhamana ya uongozi hawajui wajibu wao na majukumu yao........Sasa kiongozi mkubwa wa serikali kama waziri mkuu anapolalamika unategemea kiwango gani Cha weledi kiutendaji kutoka ngazi ya chini.............
 
Back
Top Bottom