Resilience
JF-Expert Member
- Jan 4, 2023
- 876
- 4,101
Hatua za ukusanyaji taarifa, uchakataji, uandaaji na uwasilishaji wa ripoti ya CAG NI hizi zifuatazo;
1. CAG kila mwaka wa Fedha kupitia mpango kazi wake ufanya ukaguzi WA kawaida na ukaguzi maalumu katika taasisi za umma pamoja na mashirika ya umma.
2. Katika ukaguzi wa kawaida na hata ukaguzi maalum CAG uwasilisha Kwa taasisi husika barua yakuomba kufanyika Kwa ukaguzi na kisha barua hiyo ufuatiwa na kikao kazi baina ya wakaguzi na wakaguliwa. Lengo la kikao hiki nikuwatambulisha wakaguzi Kwa menejimenti inayokaguliwa, kueleza scope ya ukaguzi, taarifa wanazohitaji pamoja na muda au kipindi cha ukaguzi.
3. Baada ya kujadiliana na menejimenti wakaguzi uingia kazini na kuibua hoja mbalimbali. Hoja zinazoibuliwa uwasilishwa Kwa wakaguliwa waweze kuzitolea ufafanuzi na majibu ikiwemo kuwasilisha nyaraka mbalimbali kutatua changamoto zinazoibuka. NI katika kipindi hiki Ndipo hoja zisizo na majibu uibuka na zile zenye majibu kufutwa.
4. Baada ya ukaguzi ufanyika exit meeting ambayo lengo lake nikuieleza menejiment wapi wamefanya vyema na wapi panapoonekana Pana dosari.. katika kikao hiki ufunguliwa majadiliano kinzani ya hoja ambapo menejimenti serious ufanya KAZI usiku na mchana kuzifuta hoja kuepusha hoja hizo kuongizwa kwenye vitabu.
5. Hatua ambayo ufuata NI CAG kuandaa draft ya hoja na kuziwasilisha Kwa menejimenti kutaka majibu na hoja hizi ujibiwa Kwa kipindi flani; zile zinazokosa majibu Ndizo uingia kwenye kitabu cha mwisho zikionyesha madhara yatokanayo na hoja husika... Kwa maneno wayapendayo wapiga Kura uita ubadhirifu.
6. Ripoti husika uwasilishwa na kukabidhiwa Kwa Mhe Rais
7. Kwa kuwa Bunge Ndilo jicho la wananchi basi ripoti husika ufika bungeni na Mawaziri WA sekta husika uwajibika kuandaa majibu na ufafanuzi kuzima baadhi ya hoja.
8. Jukumu kubwa la serikali (Mawaziri wakisaidiwa na makatibu wakuu na viongozi waandamizi WA sekta) nikupangua hoja zote kwakuzipatia majibu.
9. Bunge linaweza kutoa maazimio Kwa Yale yote watakayobaini kuwa Mawaziri wameshindwa kuyapatia majibu; kamati za Bunge pia utumia hoja hizi kusisulubu sekta wakati wakifanya vikao kuzipitia hoja.
10. Mchakato WA kufuta hoja uendelea na hivyo kwenye taarifa ya CAG inayofuata hoja zote zilizojibiwa uondolewa na kubaki zile ambazo bado hazijibiki.
Kwa mchakato huu, kwanini Mhe. Rais amerejesha hoja Kwa Katibu Mkuu kiongozi na safu yake?
Majibu.
Kama mlimsikiliza Mhe. Rais kwenye hotuba yake akielekeza serikali au watendaji kufuta hoja ambazo zinafutika au hazina majibu.....hii nikutokana na ukweli kwamba kwenye ripoti ya CAG lazima aeleze hoja zote ambazo aliziwasilisha kipindi cha nyuma na azijapatiwa majibu.
Lengo la Mhe. Rais kumwelekeza Katibu Mkuu kiongozi wazifanyie KAZI hoja hizi nikwakuwa Mhe. Rais anaelewa kwamba ripoti ya CAG ikifika kwake haimaanishi kila ubadhirifu unaotajwa basi ni ubadhirifu.
Lakini pia anaelewa kwamba hoja hizi wanakwenda kukutana nazo Mawaziri bungeni ambapo Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri niyeye...kama Mawaziri wakikosa majibu ikaonekana hoja zote za CAG zipo kama zinavyosomeka basi Baraza la mawaziri litakuwa na shida na hivyo hata Mwenyekiti naye amtaonekana ameshindwa kusimamia.
Wakati huo huo Mhe. Rais anaelewa kwamba kwenye baadhi ya hoja lazima wapo watu wamekiuka maadili ikiwemo wizi; moja ya jukumu la serikali anayoingoza nikuadhibu Tabia zilizopo ndani ya binadamu. Anatambua kwamba anaowaongoza wapo wezi na waadilifu...hivyo ametoa fursa Kwa viongozi na watendaji waliokiuka maadili wawajibishwe na apewe taarifa....Ikumbukwe Mhe. Rais siyo hakimu na wala siyo mpelelezi, yeye anatekeleza sheria. Aidha ripoti ya CAG siyo documenti inayoweza kutumika mahakamani kama ushahidi, ripoti ya CAG inaonyesha maeneo yenye viashiria vya rushwa, uvunjifu WA sheria na ubadhirifu Kwa ajili ya taasisi zenye dhamana ya uchunguzi kuingia kazini. Hello Kwa Mhe. Rais kuwa mstahimilivu kusubiri wasaidizi wake wafanye KAZI na kumpa matokeo.
Tunajifunza nini; ninajifunza kwamba Mhe. Rais anatambua kwamba akihukumu yeye hakuna wakupinga hukumu yake. Hivyo kuliko atoe hukumu Bila kuwa na ushahidi na kuepuka kuingilia mfumo wa mahakama amewapa jukumu wanaomsaidia na aliowapa dhamana.
Swali la mwisho; Je aliowapa dhamana watachukua hatua? Wasipochukua hatua atafanya nini? Awafanye nini?