Mkutano mkuu wa chama cha walimu Tanga na sakata la rushwa

HaMachiach

JF-Expert Member
Dec 15, 2015
3,399
6,077
Chama cha walimu Tanzania kinafanya mkutano wake mkuu tarehe 17 Machi 2023 Jijini Tanga haya yakiwa ni maamuzi ya mkutano mkuu wa kikatiba uliofanyika Disemba 2022. Pamoja na mambo mengine lengo ni kumchagua naibu katibu mkuu baada ya aliyekuwa naibu katibu mkuu Japhet Maganga kupandishwa ngazi kuwa katibu mkuu kwa mujibu wa katiba ya CWT kwa kuwa aliyekuwa katibu mkuu Deus Gracewell Seif alihukumiwa kifungo gerezani 28 Juni 2022 kwa kosa la uchepushaji wa fedha za chama na matumizi mabaya ya madaraka. Nafasi nyingine ni ya mweka hazina wa taifa ambapo Abubakari Alawi alihukumiwa kama alivyohukumiwa katibu mkuu kwa kosa lile lile(fedha zilizochepushwa baadhi ya matumizi ilikuwa ni kwenda kuangalia mechi kati ya Taifa Stars na Cape Verde, yaani walikwenda Cape Verde kwa fedha ambazo ni ada za walimu). Nafasi nyingine ni ya makamu wa rais ambapo aliyekuwa makamu wa rais Dina Mathamani aliondolewa nafasi yake kikatiba na sasa ni mkuu wa wilaya ya Uvinza.

Deus Seif na Abubakari Alawi wanaishi kwa falsafa ya kwamba hakuna mkate mgumu mbele ya chai. Walipohukumiwa kifungo gerezani mwaka jana na Hakimu Mhe. Richard Kabate wa mahakama ya Kisutu walikaa gerezani muda wa chini ya juma moja. Mkate ukawa laini mbele ya chai. Sio mahakama ya Kisutu wala gereza la ukonga aliyeeleza ni kwa nini wafungwa hawa walikaa nje ya gereza wakati wa kifungo hicho.

Jamhuri ilikata rufaa dhidi ya kifungo laini na cha utatanishi hata hivyo kwa kuthibitisha kwamba hakuna mkate mgumu mbele ya chai, mwezi huu mahakama kuu kanda ya Dar es salaam chini ya Jaji Ephery Kisanya na kama tulivyokwisha tahadharisha hapo awali, walifutiwa kesi na kwamba eti kifungo walichopewa kilikuwa batili. Baada ya hapo mafisadi hawa wakafungua kesi nyingine mahakama kuu Dodoma ikisimamiwa na Jaji Dkt. Mambi kwanza kwa kuweka zuio la mahakama kuzuia mkutano mkuu wa CWT kutojadili hoja za mafisadi hawa Disemba 2022 kwa kuwa walikuwa na kesi mahakamani kwa sababu ya fault in technical grounds za waleta maombi mkutano mkuu ulijadili hoja zao na kuwafutia uwanachama. Juma lililopita mafisadi hawa kupitia Jaji Mambi waliweka zuio la mkutano mkuu kujaza nafasi zilizojazwa hapo juu. CWT ikaamua kumkataa Jaji Mambi kwa sababu zifuatazo.
  1. Jaji Mambi ana uswahiba mkubwa na Deus na Alawi, Akiwa Mbeya aliisaidia CWT chini ya Deus kuwakandamiza Chama kingine cha walimu (CHAKAMWATA) na fedha za rushwa kutoka kwa Deus zilikua zikipitia kwa katibu wa CWT Mbeya Ms. Sekela.
  2. Jaji Mambi alipohamia Dodoma alimnyanyasa Mwalimu Clement Mahemba aliyekuwa mwenyekiti wa CWT mkoa wa Dodoma kwa maelekezo ya Deus kesi yake ilipotea.
  3. Jaji Mambi huyo huyo kwa maelekezo ya Deus alimnyanyasa mwalimu Ndabazi Kasebo kesi yake nayo ikapotea. Huu ulikua ni utekelezaji wa hakuna mkate mgumu mbele ya chai.
Shinikizo kubwa kutoka kwa wanasiasa waandamizi na viongozi wa serikali wenye maslahi binafsi na fedha za CWT lilikua ni kuhakikisha kwamba rais wa CWT na katibu mkuu wake wa sasa wanakwenda kuripoti na kuapishwa kuwa wakuu wa wilaya ili viongozi hao wahakikishe kuwa viongozi watakaochaguliwa kwenye mkutano mkuu wa Tanga ni watu wao na hii ni ili waendeleze wizi na ufisadi wao dhidi ya fedha za walimu. Kwa hiyo basi wakaamua kuwafadhili baadhi ya wagombea wa nafasi hizo. Kwa Hekima ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan alijua namna ya kulichukulia jambo hili na wateuliwa waliendelea kwenye nafasi zao ndani ya chama jambo ambalo liliwakera wanasiasa na viongozi hao waliokuwa na dhidi ya CWT.

Deus Seif na Abubakari Alawi baada ya kushindwa kwenye hila yao wakaamua kuwatumia baadhi ya mabosi wa TAKUKURU ili kufanikisha zoezi la kupitisha rushwa kwa wajumbe na hata wizi wa kura katika mkutano mkuu Tanga wa Tarehe 17 Machi 2023. Moja ya watu ambao Deus Seif amekuwa akiwatumia kwa muda mrefu ni Bw. Victor Swella ambaye kwa sasa ni kaimu Mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Tanga ambaye hapo awali alikuwa akimhujumu Mkurugenzi wa TAKUKURU akiwa Dodoma kwa kutotekeleza maagizo ya bosi wake au kwa kutoa taarifa kwa Deus ili achukue tahadhari kwa mambo yanayotakiwa kufanyiwa kazi na TAKUKURU kipindi akiwa Naibu Mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Dodoma chini ya kamanda mwadilifu Sosthenes Kibwengo. Bw. Swella tangu juma lililopita akiwa Tanga amekuwa akiwapigia simu wajumbe kadhaa wa mkutano mkuu kwa namba yake ya 0754803882 eti kwamba vikionekana viashiria vyovyote vya rushwa afahamishwe huku vyanzo vyetu vya kuaminika vikitahadharisha kwamba lengo lake lilikiwa ni kuwataarifu watoa rushwa kuchukua tahadhari kwani taarifa alizonazo mpaka sasa zingetosha kuwawajibisha baadhi ya watoa rushwa hao.

Kinachotokea kwa sasa kuelekea mkutano mkuu ni nini?
  1. Vyumba karibu vyote vya hoteli Jijini Tanga vimekuwa vikilipiwa fedha na Katibu wa CWT wa Tanga, mwalimu Kombo mwenye namba ya Simu 0716397849 hii ni fedha nyingi sana na mwalimu anapataje fedha za kulipia hoteli nyingi kiasi hicho wakati walimu wanateswa na vicoba, mikopo kausha damu na ile ya mabenki? Hawa wanaomwaga fedha hizi ili kupata uongozi watazirejeshaje? Wajumbe wanapofika kwenye hoteli hizo huambiwa wasajili taarifa zao na kuelekeza kura zao kwa Joseph Misalaba kwenye nafasi ya Unaibu katibu mkuu na Protas Magesa kwa nafasi ya uweka hazina. Hapo mjumbe atalala na hatapaswa kulipa gharama ya malazi na chakula. Tarehe 15/3/2023 wajumbe wa Shinyanga walifika Tanga kwa usafiri wa Coaster yao saa 10 alfajiri wakazunguka jiji la Tanga hadi saa 3 asubuhi bila kupata pa kulala lakini baadae walipata, ni kwa namna gani walipata waulizeni wenyewe kupitia Katibu wao wa Mkoa Kizito Shuli.
  2. Baadhi ya wajumbe walipewa usafiri kutoka kituo cha mabasi mpaka sehemu ya malazi bure, wajumbe kutoka mkoa wa Ruvuma ni mfano mzuri.
  3. Joseph Misalaba na Protas Magesa, pesa wanapata wapi? Watajwa hapo juu wamezunguka mikoa yote ya Tanzania Bara wakihonga wajumbe kama wanagawa karanga na Joseph Misalaba mwenye namba 0752569398 ndiye aliyempatia mwalimu Kombo Katibu wa CWT Tanga fedha za kulipia hoteli zote. Lakini Joseph Misalaba Katibu wa CWT Geita amefadhiliwa na Katibu wa Geita Football Club Mwalimu Shija mwenye namba 0755561944. Papo hapo wameungana na Protas Magesa mwenye namba 0769863274. Anayewaunga mkono kwa kiwango kikubwa ni Bw. Deus Seif na Abubakari Alawi ambao pia kwa sasa wapo jijini Tanga wakisimamia zoezi zima la kuhakikisha kwamba Protas Magesa na Joseph Misalaba wanakaa kwenye nafasi zao.
Tunaiasa Serikali na mamlaka zake kuona kwamba uchaguzi mkuu wa chama cha walimu unaofanyika kesho jijini Tanga unafanyika kwa haki hii ni kwa ajili ya maslahi ya walimu wa nchi hii ambao makato ya asilimia 2 ya mishahara yao ya kila mwezi ndiyo yanayoendeshea chama. Tunaomba pia kuwaonya viongozi na wanasiasa waliokuwa wakifaidika na ambao wanataka kuendelea kufaidika na fedha za walimu kuacha hujuma dhidi ya walimu. Wakifanikisha hili tunaahidi tutafichua taarifa zao zote kwa kuwataja kwa majina, wamefaidikaje na fedha za walimu na kwa sasa wanafanya nini. Jambo hili wasilichukulie poa. We are determined. We will never ever give up.
 
Ukila hiyo takrima na ukampigia kura mtu mwingine unaye mkubali utapatwa na jambo Yani baya? Watu mnadhalilika kifala sana.Yani hongo ya malazi kwa siku tu ndiyo ikufanye umpe mtu kura kirahisi hivyo?
 
Kuna taarifa za chinichini wa zuio la mkutano huu. Mkuu hebu fukunyua huko utujuze ukweli wake
 
Ikumbukwe pia Maganga Japhet alikataa uteuzi ili abaki kula pesa za chama ambapo anasubiri kula pesa za tishet za meimosi Kwani hata mkataba wa tishet ulisainiwa na mwanasheria wa nje ambaye siyo mwanasheria wa chama na hii ni baada ya aliyekuwa mkuu wa Idara ya utetezi Queen Augustino kukataa kusain mkataba ule kwa sababu ulikuwa haujakidhi vigezo vya zabuni na hivyo aliamua kumtafuta mwanasheria wa nje ili Asaini mkataba huo waweze kupiga hela.

Lakini pia, Maganga mpaka sasa amewahamisha makatibu na hajawalipa pesa za uhamisho, watumishi makao makuu nao wanalalamika hawjapata haki zao, pesa zote alikuwa anapeleka kwenye uchaguzi ili watu wake washinde.

Hela yote ya pet cash , pesa za marejesho za mikoani zote zimeishia kwenye uchaguzi. Anawatesa watumishi wote ambao hawako upande wake na wale walioko upande wake anawapa feva kibao mfano amewapa watu walioko upande wake mikopo ya ndani isiyo na riba na ambao wamepewa hiyo mikopo ni Paschal Msafiri ( huyu ni mwanasheria ambaye alikuwa amefukuzwa kazi ila Maganga akamrudisha ili amsaidie kwenye kupiga hela), Paul Mdachi, Pasian Siay, Mathew Martin, consolatha kadikilo, Mohammed Mustafa, Nelea Nyang’uye .

Hawa wote ndo watu wake wanaomsaidia katika ishu zake za kupiga hela na kunyanyasa watumishi ambao anadhan hawako upande wake . Kwa kifupi chama Cha walimu kwa sasa kinakngozwa na Mtu ambaye hana hata uelewa wa uongozi, ameingia tu ili kupiga hela. Mpaka sasa watumishi wengi hawajalipwa haki zao Kwani pesa zote zinatumika kuhonga, ipo taarifa ya kwamba Japhet Mganga ilikutwa milion 400 kwenye akaunt yake ya bank.

Mtu amekuwa katibu mkuu kwa miezi 3 tayari ana milion 400. Walimu kuweni macho na huyu Japhet Maganga. Maana ameingia katika uongozi kwa slogan ya kwamba “ acha na yeye afaidi pesa ya chama kwa muda mfupi ili akitoka atoke akiwa amefaidi “ na ndicho chanzo Cha yeye kukataa uteuzi Kwani ulikuwa ni muda mfupi tangu athibitishwe na alikuwa bado hajapiga hela ya kutosha akaona agomee uteuzi. Anachokifanya sasa ivi ni kupiga tu hela na watu wake.
 
Back
Top Bottom