Ndio usome somo la siasa ya kwamba Urais unaandaliwa na hivyo vyama vyenu ni vumbi la macho tu kutekeleza agizo la nchi za magharibi lakini hakuna Upinzani pale ni ushindani kaa klabu za mpira..Hebu jiongeze kidogo basi
kama kitengo kiko sahihi leo kumuondoa Lowasa
kitengo kinaaweza kesho kumuondoa mwingine kwa sababu ambazo sio sahihi
je wao kitengo nani kawapa mamlaka?
wao ni wasafi kiasi gani?
mbona Ngeleja hana tofauti na Lowassa na kitengo wamemtumia?
Ikiwa leo wewe unashangaa KITENGO kumuondoa mtu wakati vyama vinaondoa watu na wengine kupokea watu pasipo kujali historia zao, iweje ufikirie kwamba KITENGO kinaweza kumuondoa mtu asiyekuwa sahihi? sahihi kwa nani? maana usahihi wenyewe lazima utokane na interest za nchi sio za chama.
Na inapotokea mtu kuanzisha Cartel ndani ya Chama huoni kama ndivyo mlivyowadhania kina Kitila na Zitto na mkawafukuza. Huyu kapewa heshima na kaachwa hadi dakika ya mwisho..Kwanza ilitakiwa wagombea wote wa Urais wafanyiwe screen chack na Usalama, kehso wakija kuuza nchi je!
Leo mmekuwa na Ujasiri gani kufanya yale yale mloyakataa kwa kina Zitto kwa tuhuma tu leo ukatae utafiti wa KITENGO juu ya Lowassa!.. halafu maajabu yenyewe wanaopinga ni Chadema ambao wanasema Chama kina KANUNI zake unafikiri nchi haina KANUNI zake? Hao KITENGO unadhani wamejifunza nini kama sio kulinda Katiba na Kanuni za nchi hii... hata huko Marekani CIA lazima wampitishe mgombea Urais, UK lazima M16 wampitishe mgombea Urais sio swala la chama na wananchi pekee.