Mgombea urais kwa tiketi ya CCM mwaka huu John Maguli tayari amekuwa na ziara za kutembelea mikoa mbalimbali kabla na toka ateuliwe na CCM kuwa mgombea urais, kuna mambo kadhaa ambayo nimechunguza na kujiuliza kama kweli CCM ilifanya uamuzi sahihi kumteua Magufuli kuwa mgombea wake waburais.
Kwa mfano
1/Wakati wa uchukuaji fomu za kuomba kuteuliwa kugombea urais ndani ya CCM, Magufuli hakuonekana sana kama ni miongoni mwa watu wanaofaa kupeperusha bendera ya CCM, hakukuwa na mshtuko wala hamasa yoyote kutoka kwa wanaCCCM au wasio wanaCCM kuhusu ugombea wa Magufuli. Tofauti kabisa na wagombea wenzake kadhaa. Hakuna mwanasiasa asiyetaka kushangiliwa au kushabikiwa, na hatuamini kabisa kuwa Magufuli hakutaka kushangiliwa au kushabikiwa bali huenda ni mvuto duni wa kisiasa ndani ya CCM au vinginevyo.
2/Hata baada ya Magufuli kuteuliwa rasmi kuwa mgombea urais wa CCM na kufanya mikutano ya Hadhara mjini Dodoma, Dar, Zanzibar na Mwanza bado hatukuona mwangwi mzito wa mwitikio wa watu.
Kwa ujumla mikutano yote hiyo ilijaa makada wa CCM wakiwa na sare zao za kijani(wengi wao walikuwepo kwenye harakati za kumshabikia Lowassa wakati wakusaka wadhamini) wakiwa na sura zenye mashaka makubwa na tabasamu za kutengeneza. Wengi wetu tulitegemea makundi makubwa sana ya watu mbalimbali hususani wasiokuwa wanaCCM.
3/Mpaka sasa hatujaona kishindo cha mtikisiko wa kisiasa kwa upande wa upinzani katika kuhofia ujio wa Magufuli katika mbio za urais mwaka huu. Japokuwa UKAWA hawajatangaza rasmi mgombea wao lakini hatuoni Presha yoyote katika kuhofia nguvu za Magufuli kisiasa.
4/Mwitikio wa Makundi makubwa ya kijamii bado uko chini sana baada ya Magufuli kuteuliwa. Mpaka sasa wingu la kisiasa limegubikwa na kukatwa kwa jina la Lowassa tu, badala ya uteuzi wa Magufuli.
Kila mtu alishuhudia namna Lowassa alivyokuwa akitikisa kila mahali alipopita wakati tu, amechukua fomu kugombea urais.
Tukio la Lowassa kutangaza nia jijini Arusha lilikuwa ni tukio kubwa sana kiasi cha kusimamisha kabisa shughuli za watu katika Miji ya Arusha, Moshi na Manyara. Lakini huwezi amini Tukio la Magufuli kuteuliwa kugombea irais na CCM na kuja Dar na Mwanza halikushtua kitu chochote katika shughuli za watu za kila siku.