Nchi inaendeshwa na 'KITENGO'?

Nchi inaendeshwa na 'KITENGO'?

Waandishi wa tz...mostly ni wasaka na watoa taarifa za matukio...rais kaenda kufungua barabara, daraja, hospital etc...

Tz hatujafkia kuwa na waandishi wa habari za uchunguzi...ni safari ndefu sana kufika huko, kuiendea na kuifkia safari kwahitaji machozi, jasho na damu.

Historically nchi zilizopitia ujamaa wa kikomunisti wa urusi na china kama yetu, system (kitengo ) hupenya maeneo yote muhimu ya ki nchi kwa lengo la kudhibiti mambo na kuhakikisha nchi inakwenda kwa ajenda kusudiwa...kwa sababu hiyo kitengo huamua nani awe nani kwa muda gani...in the process kuna watu huumizwa albeit kwa maslahi mapana ya nchi...

am happy kitengo kutumika kumzuia mamvi kwani kwa ushahidi wa wazi wa namna mamvi amekuwa akitumia nguvu ya pesa katika safari ya matumaini...obviously alijipanga na namna ya kurudisha pesa zile....how?...waangalie wapambe wake wakubwa na utapata jibu....

wanasema democracy iliminywa....ni kweli, and am happy with that katika mazingira hayo special maana hata Hitler aliingia kwa democracy lkn kilichofatia...history ni shahidi.

Pats like yangu mkuu well said
 
Fikiria mtu na akili zake timamu anatetea hilo zimwi kitengo eti kina haki ya kuwachagulia wananchi viongozi kwa sababu wananchi wanaweza kumchagua mtu hatari. Swali ni hatari kwa nani?

Kuna dai kwamba chama tawala CCM kimetekwa na wenye nguvu lakini hatujiulizi hao wenye nguvu ndio akina nani? Zipo nyakati nyingi tu viongozi wetu wa kitaifa tuliowachagua tumesikia wakilalamika, hatujiulizi wanamlalamikia nani.

Kama Raisi analalamika, Waziri Mkuu analalamika, Katibu Mkuu wa chama tawala analalamikia utendaji wa serikali iliyoundwa na chama chake...wananchi tueleweje? Katiba yetu imempa nguvu ya kimungu Raisi wetu, kwa nini alalamike?

Oh mara wasaidizi wangu wananiangusha, anawabadilisha, Haijakaa muda na hao wapya anaanza kuwalalamikia eti wanamuangusha, anawabadilisha. Muda si muda mambo bado hayaendi anaanza tena kulalamika, kulikoni wananchi wenzangu?

Tunamchagua Raisi kwa imani kubwa kwamba sasa tumempata kiongozi mzuri lakini haichukui muda mambo yanarudi kule kule. Mifano ipo tangia Mwinyi, Mkapa na sasa Kikwete...ni nani huyo anawachezesha mchakamchaka, je ni kitengo?

Hayati Mwalimu alimpigia debe Mkapa, akatembea nchi nzima akimnadi kama mtu safi lakini haikuchukua muda, tukajikuta tunatoka kapa. Mwalimu akaahidi kumpinga uchaguzi utakaofuata...je ni kitengo kilichoamua asiuone huo uchaguzi?

Cha ajabu licha ya kuwa na kitengo tumewashuhudia wezi na matapeli makubwa ya dunia yakipata hifadhi nchini na kuzidi kuneemeka kupitia rasilimali zetu.

Licha ya kuwa na kitengo tumeshuhudia matapeli wa kimataifa wakiivamia nchi yetu na kuingia mikataba mibovu ya kupora mali asili zetu kuanzia wanyama, madini hadi mimea.

Imefikia mahali ni kama nchi haina serikali, nchi haina katiba, nchi haina utawala wa sheria na vyombo vya dola viko tu kulinda maslahi ya wageni na maslahi ya wahamiaji haramu.

Ni kama vile vyombo vya usalama vipo tu kupambana na wananchi na si kuwalinda wao na mali zao. Vyombo vya kutoa haki navyo vinalalamika havina nguvu ya kupambana na wahalifu.

Ni kama vile nchi imetekwa na nchi haiko tena mikononi mwa wananchi na matakwa ya wananchi hayapewi tena uzito wala kipaumbele na serikali ni kama haiwatumikii tena wananchi.

Ni kama vile serikali haikuwekwa madarakani na wananchi bali imewekwa na hao inaowatumikia...kitengo? Kama Mtanzania hawezi kumchagua kiongozi anayemtaka kwa sababu kitengo hakikubali, je kweli tuko huru?

Kama Mzee Ngombale Mwiru, kada maarufu wa CCM aliyeitetea CCM wakati wa kiangazi na mvua, usiku na mchana leo yamemkuta na analalama kuhusu kitengo, lazima tujiulize maswali kadhaa!

Viko vifo vingi tu vya kutisha vimetokea nchini visivyo na maelezo, je ni kitengo kinanyamazisha wakosoaji?
Tumeshuhudia kila kunapotokea mtafaruku, kiongozi mkuu wa nchi anakuwa hayupo nchini, je nani huyo anaachiwa utekelezaji?


Hapana Watanzania, hii ni karne ya 21 na teknolojia inatupa fursa ya kutoka gizani. Mambo ya gizani tusiyape nafasi hivyo tujiulize. Kwa nini tuchague kiongozi tukiamini ni msafi halafu baada ya kitambo kidogo tu anaanza kucheza ngoma ya wengine?
 
The Boss,

Huoni kwamba kwa wao kupendekeza taarifa za kukatwa kwa Lowassa walikuwa loyal subject to the Republic?. Umewahi kujiuliza nini kingetokea endapo wangeruhusu Lowassa apitishwe?

Ndiyo 2005 walishindwa kutimiza wajibu wao, lakini mwaka huu wameweza. Isitoshe wao wako better placed kujua nyendo za ndani kabisa za wagombea wote.

By the way, hivi kwani vyama vingine wamezuiwa kutumia huduma za "kitengo" kupata taarifa sahihi za wagombea wao? Au ni muendelezo wa malalamio ya watanzania kama ilivyozoeleka?


Mkuu na wengine wengi
nimejaribu sana kueleza hapa main issue sio Lowassa lakini naona hamuelewi kabisa

Hebu tu assume 'kitengo' walimkata Lowassa na tu assume kuwa ni uamuzi sahihi..

swali bado linabaki pale pale....Kitengo walitumia vigezo gani kumchagua Magufuli
na kuwakata Pinda,Bilali,Mahiga,Mwele,Mwandosya,Sitta,Mwigulu,Kigwangala,na wengi wengine wote?

Hivi unafikiri wanachama wangechagua kwa uswa kati ya majina yote hayo Magufuli angepita?
na Usiseme Kitengo hakihusiki sababu nimetaja gazeti la RaiaMwema limeripoti Kitengo kumfanyia kampeni
Magufuli...na hata kura alizopata Asha kutoka Nec kura 280 kufika mkutano mkuu zimepunguzwa hadi 50...

Hilo ndo swali.....Kitengo kawapa nanimamlaka ya kuwachagulia watu Rais?
 
The Boss,

Huoni kwamba kwa wao kupendekeza taarifa za kukatwa kwa Lowassa walikuwa loyal subject to the Republic?. Umewahi kujiuliza nini kingetokea endapo wangeruhusu Lowassa apitishwe?

Ndiyo 2005 walishindwa kutimiza wajibu wao, lakini mwaka huu wameweza. Isitoshe wao wako better placed kujua nyendo za ndani kabisa za wagombea wote.

By the way, hivi kwani vyama vingine wamezuiwa kutumia huduma za "kitengo" kupata taarifa sahihi za wagombea wao? Au ni muendelezo wa malalamio ya watanzania kama ilivyozoeleka?

Huduma ya kitengo nje ya ccm ni kuzuia mikutano, kupandikiza na kuwalipa mamluki ndani ya vyama kuvuruga ustawi wa vyama (ZZK) kushauri kitengo jinsi ya kuiba kura, kununua wapinzani n.k.
 
Hilo pia ni tatizo, waandishi wetu wa tanzania hawajui kwenda deep na kufanya investigation ya habari, wanachofanya wao ni kukimbilia kuandika habari nusu nusu bila ya kwenda deep wakaja na habari kamili. Kwa kweli sasa hivi ccm imeshikilia kila sehemu muhimu ya hii nchi. Jeshini, usalama wa taifa Polisi na Magereza, hao wote wakistaafu wanapewa ukuu wa wilaya na mikoa, kama sio nafasi za ubalozi. walewale walioshindwa wana wa-recycle na kuwarudisha kwa njia nyingine. I know lots of Top military who think this country belong to ccm, wanajisahau kuwa nchi ni ya watanzania.

Wengi wananyemelea vyeo ccm


CCM ni chama dola ukisikia wanasema sisi wajamaa, ujue ndiyo ktk mambo kama haya huu ndiyo mfumo wa Kikomunist nasikitika hata Mzee Kingunge kasahau.

CCM walishikwa woga sana ktk Katiba mpya pale walikua wameshikwa bara bara, lakini bahati haikua yetu tulitaka kupata kila kitu na Wahenga walisema mtaka yote kwa pupa..............

Lazima tujiulize kwa nini kuna Kamati ndogo ya maadili na Kamati ya Usalama na Maadili ambayo Mwenyekiti wake ni Mwenyekiti wa Chama ambaye ni Rais wa nchi, lakini pia hatujawahi kujenga hoja ya kupinga vikao vya CC kukutana Magogoni!

Kwa mtazamo wangu kama CCM watashinda uchaguzi wakapata Wabunge wengi, tuwashinikize Katiba pendekezwa ipigiwe Kura ya ndiyo hivyo hivyo ilivyo kwa sababu hakuna njia nyingine.

Najua tutakua tumerudi nyuma miaka 5 lakini ndiyo gharama hakuna njia ya mkato, kwani uwezekano ni mdogo upinzani kushinda kwa Katiba hii ya 1977

Swala la waandishi pia ni tatizo hawana uthubutu wakumtaka Waziri au Mkuu wa Nchi ili kufanya nae mahojiano, mpaka anajipangia mwenyewe kuongea mwisho wa mwezi akitaka.

Tujitahidi tukishindwa tusikate tamaa lakini kasoro kubwa kwetu ni MATUSI, KEJELI, UDINI, UKANDA na UJUAJI ukiangalia wengi wa wachangiaji uelewa wao ni mdogo kila mtu aheshimiwe au akikosea aelimishwe tutasonga mbele vinginevyo naiona miaka mingi ya CCM kuendelea kutawala.
Ole wetu kama tutamucha Comred Kinana aanze kufanya kile alichoahidi Mwanza.
 
I just don't get it. I just don't.

The opposition will never win the presidency under the current conditions. Never.

And that fact is as audible to the deaf as it is visible to the blind.

That's how obvious it is.

Tuliingia kwenye mfumo wa vyama vingi bila kubadili katiba. Iliyokuwepo iliwekewa viraka tu.

Mbona Afrika Kusini walipotoka kwenye Apartheid na kuingia kwenye demokrasia ya kweli walibadili na katiba?

Imagine serikali ya ANC ingekuwa inatawala kwa kufuata katiba ya Makaburu....

Tulipaswa kuingia kwenye mfumo wa vyama vingi na a brand new set of rules that is apropos for the new system.

Siyo kuja kuanza kuhangaika na katiba mpya miaka 20 na kitu baadaye.

Mimi nina imani kama tungeaza afresh hiyo 1992 basi huenda sasa hivi tungekuwa hata tushapata rais kutoka nje ya CCM.
Duh!

Kutoka 2015!

Zaidi ya miaka 5 ilopita.
 
I just don't get it. I just don't.

The opposition will never win the presidency under the current conditions. Never.

And that fact is as audible to the deaf as it is visible to the blind.

That's how obvious it is.

Tuliingia kwenye mfumo wa vyama vingi bila kubadili katiba. Iliyokuwepo iliwekewa viraka tu.

Mbona Afrika Kusini walipotoka kwenye Apartheid na kuingia kwenye demokrasia ya kweli walibadili na katiba?

Imagine serikali ya ANC ingekuwa inatawala kwa kufuata katiba ya Makaburu....

Tulipaswa kuingia kwenye mfumo wa vyama vingi na a brand new set of rules that is apropos for the new system.

Siyo kuja kuanza kuhangaika na katiba mpya miaka 20 na kitu baadaye.

Mimi nina imani kama tungeaza afresh hiyo 1992 basi huenda sasa hivi tungekuwa hata tushapata rais kutoka nje ya CCM.
Apatikane mtu ayachapishe vizuri maoni haya na kuya-laminate vizuri halafu yakagawiwe (hata kama ni kwa lazima) kwa viongozi wote wa upinzani. Na walazimishwe kuyasoma na kuyaelewa vizuri.

Bila kuwa na katiba mpya (mf. ile ya Warioba), tume huru ya uchaguzi na taasisi zingine huru kama mahakama, haki ya nani urais wataishia kuwa wanausikia kwenye TV tu na kila mwaka yatakuwa yale yale...."wanashindwa", wanalalamika kuwa wameibiwa kura, wanatukana na hata kupuyanga kwenda kushtaki huko kwa akina Amsterdam lakini hakuna kitakachobadilika.

Kuanzia sasa nguvu zote zielekezwe kwenye kupata katiba mpya...na mengine yote yatafuatia. Kama siyo hofu ya kupoteza hela za ruzuku, kusema kweli hata haja ya kushiriki chaguzi hizi hakuna...
 
Back
Top Bottom