Nchi inaendeshwa na 'KITENGO'?

Nchi inaendeshwa na 'KITENGO'?

Kuna vitu vinajitokeza kipindi hiki cha uchaguzi
ambavyo vinapaswa kuulizwa
je nikweli wananchi wa Tanzania ndio wasemaji wa mwisho wa masuala ya nchi hii?
au kuna watu kwa aakili zao na utashi wao wamejipa 'jukumu' hilo?

Kingunge alisema 'KITENGO' ndio kiliamua nani awe mgombea wa CCM na sio
wanachama......na Ukisoma gazeti la Raia Mwema wanasema watu wa 'usalama'
walimwambia Ngeleja awaambie wazanzibar kumchagua 'mgombea wa kitengo'
ndio akashinda....maswali yanajitokeza
1.kitengo kinaendeshwa na nani hasa?
2.Ni watu wangapi wanaofanya hayo maamuzi?
3.Ni kweli maamuzi yao yote ni kwa faidaya Taifa?
4.Wananchi wakipishana maamuzi na 'kitengo' maamuzi ya wananchi yataheshimiwa?
5.Nguvu ya 'kitengo' kwa tume ya uchaguzi ni halali?
6.kuna faida ya kushiriki uchaguzi huku 'kitengo' kimeshafanya maamuzi?
7.Je tuna demokrasia kweli au tunaruka ruka ttu na maigizo?

Mleta mada pamoja na mjinga mwenzako kingunge mwanzo mlitarajia kitengo kimteue lowassa leo mnasema kitengo hakifai! acheni uchangu doa wenu wa kula hela za lowassa
 
Hiko kitengo kipo CCM tu!?
Kitengo hakiwezi kuchagua wapinzani?
Double standards hizi.

1. Inawezekana kipo zaid ya CCM inawezekana kipo kila unapodhani hakipo. . . .
2. Wapinzani kwani hawako karibu na mboni ya kitengo??!!!! Kama wako mbali inawezekana jicho halioni sawa lakini hata simu na barua havifikishi ujumbe??!??
3. Mwezi wa saba unaisha huu jina tu la mgombea ni mivutano na walisema wanajua wanalofanya na kila kitu kiko sawa wananchi wasitaharuki. . . . . .kiko wapi??!!! Hata wewe ungekuwa mkuu wa kitengo ungekaa usubiri au ungetangulia na watu wanaoonesha utayari wa kufanya hivyo??!!!. . . . .

Ni sahihi na wakati muafaka wananchi kuhisi na kuona nchi ina watu wanafikiria, taasisi na mifumo pia ipo. . . . .Hata kama kuna mapungufu
 
Waandishi wa kuaminika kama wa Raia Mwema wana ripoti tu hili bila kuuliza maswali

Hawa walikuwa wakimsujudi yule jamaa aliotakiwa na hao wanaojidai wakitengo kwa kuwahidiwa vyeo na pia wengine wale wale walioshiriki wizi wa ESCROW walishiriki wizi wa Mali za wananchi! Hawa kazi yao kubwa ni kutuletea ripoti ambayo hajakuwa doctored kuhusu wagombea.

Hapa Kama taifa tutadanganyana na ujinga huu utatupeleka pabaya.
 
Kitengo lazima kifanye kazi zake kuangalia maslahi ya nchi kuacha sanduku LA kura itafikia tukachaguliwa kichaa
 
Kingunge alisema 'KITENGO' ndio kiliamua nani awe mgombea wa CCM na sio
wanachama......na Ukisoma gazeti la Raia Mwema wanasema watu wa 'usalama'
walimwambia Ngeleja awaambie wazanzibar kumchagua 'mgombea wa kitengo'
ndio akashinda....maswali yanajitokeza
1.kitengo kinaendeshwa na nani hasa?
2.Ni watu wangapi wanaofanya hayo maamuzi?
3.Ni kweli maamuzi yao yote ni kwa faidaya Taifa?
4.Wananchi wakipishana maamuzi na 'kitengo' maamuzi ya wananchi yataheshimiwa?
5.Nguvu ya 'kitengo' kwa tume ya uchaguzi ni halali?
6.kuna faida ya kushiriki uchaguzi huku 'kitengo' kimeshafanya maamuzi?
7.Je tuna demokrasia kweli au tunaruka ruka ttu na maigizo?
Mkuu, kwa wataalam wa saikolojia, mtu anapokuwa katika maruwe ruwe kuna nyakati husema yanayoonekana kama maruwe ruwe, ukweli ni kuwa anachosema ndicho alicho nacho moyoni.

Ni maruwe ruwe'delirium' ndiyo humusukama kusema bila kukusudia

Baada ya kufanikiwa kumtengeneza mfalme,mzee alijisahau au alijivika kofi ya ubaba wa Taifa.

Akawekeza sana , mwisho wa siku tunajua yaliyomkuta. Hapa namnukuu JK akisema 'naomba yaliyomkuta mzee X yasije yakanikuta''

Mzee alikuwa ndani ya 'Kitengo' tulichokuwa hatukijui hadi alipoapatwa na mkasa.

Hivi leo analalamikaje, ikiwa sisi wananchi wenye nchi hatukujua kitengo isipokuwa yeye na wana kitengo? Thanks to CCM

Kuhusu hoja zako

Kwanza, mzee anatueleza hatuna demokrasia. Hata hivyo, hatuwezi kukaa tukilalamika bila kufanya jambo.

Oktoba 25 tubadili mwenendo ili tuwape watu wa nje nafasi ya kutueleza kitengo kinafanyaje kazi

Pili, ninashangaa usalama wa taifa wanaingia katika kitengo cha CCM. Hapa napo pana jambo

Tatu, tume ya uchaguzi ni sehemu ya 'kitengo' nikupe mfano. CCM waliosema kura ya maoni ipo, tume ikashikilia msimamo huo.

CCM wakasema kura ya maoni ni pamoja na uchaguzi, tume ikashikilia msimamo.

CCM wakasema wameagiza BVR na kazi itamalizika kwa wakati, tume wakasema hayo.

Rais akarudia kule Washington kuwa kura ya maoni ipo pale pale, mwenyekiti wa tume akarudia maneno hayo hayo.

CCM wakasema wameshauri serikali iharishe kura yao ya maoni, tume wakasema nao wanaahirisha.

Yaani tume iliyopaswa kuongozwa kitaalumu, imekuwa inapokea maagizo ya ''kitengo''

Ndiyo maana tunasema, kama tutalalamika bila kuleta mabadiliko, 2020 tutakuwa hapa tunazungumzia hicho hicho

Tatu,kitengo kinaendeshwa na nani? Hapa mzee atusaidie maana hatukujua uwepo wa kitengo

Nne,Watu wangapi wanafanya maamuzi? Mzee anajua kitengo kimeundwaje na kina watu wangapi

Tano,maamuzi ya kitengo ni ya kitengo, na huwa ya kitaifa kupitia vyombo husika.
Kimoja ni hicho tulichoambiwa, kingine ni Bunge. Hivi watu hawajui mswada wa gesi na mafuta ni kazi ya kitengo?

Uliletwa haraka na serikali, ukapigwa mhuri haraka haraka na bunge ili watu waende kwenye kampeni, tumeondoa mafuta na gesi tupeni kura wazanzibar. Hili nalo linajibu hoja ya maamuzi kwa manufaa ya taifa

Sita,kuna fiada gani kushiriki uchaguzi? Tukikaa pembeni kitengo kinaimarika.

Tumekaa miaka 50 na kitengo, hatuwezi kuendelea kukaa mingine 50 tukisubiri kitengo kitatuhurumia.

Lazima lifanyike jambo, kazi hiyo ipo kwetu na si kwa kitengo. Oktoba 25 tukiendelea na ugonjwa wa kusahau, hewalaa!

Mwisho mzee wetu kasoma Urusi. Anajua vema falasafa za vanguard party na Polituburo.
Sina uhakika nani ameanzisha kitengo, ninachojua kitengo ni mfumo uliopo unaondeana na anachokieleza mzee
 
Km kuna pahala TISS walicheza kwa ufanisi na busara ni pale walipohakikisha jina la Lowasa linakatwa.Ingekuwa enzi zile,Edo angelikwisha pata ajali siku nyngi.Hyo iko pote duniani hata Us.Hata opp. Kunyimwa ushndı ni kazi ya TISS, to be fair hauwezi kukabidhi nchi kwa watu km Mbowe.TISS ndo inasaidia kuwajengea uwezo opp na baada ya muda nadhani watawapa nafasi wakishnda.Wanaimprove kila siku na watu wenye akili wanawajoin, tutafika.
 
Hebu fikiria kama CIA au M16 kama wangekuwa wanafanya siasa kwenye taasisi zao hizo nchi zao zingekuweje? Leo hii hapa kwetu Tanzania wageni wanakuja kuiba mchana kweupe wanachukuwa wanyama huko kwenye mbuga zetu na kuwapakiza kwenye ndege, madini yetu yanaibiwa kila siku na vijidege vidogodogo vinavyotuwa kwenye migodi.
Eti usalama wa taifa wapo busy kwenye ofisi za ccm kuhakikisha ccm haitoki madarakani. Usalama wa taifa unatumikia CCM badala ya taifa na rasilimali zake. This is shamefully and disgusting to us Tanzanian. Politics is everywhere, this is too dangerous to our nation playing politics in serious matter
kila sehemu kuna watu wa kitengo hata hizo ndege zinazoiba raslimali zinasimamiwa na kitengo
 
ha ha ha...naona sasa vijana wamelipwa kuja mitandaoni kutuletea porojo.
ACHENI POROJO NA KUTUMIKA...
Lowasa mwenyewe ni hatari kwa afya yake binafsi...sembuse familia yake na watanzania.

Mgombea urais kwa tiketi ya CCM mwaka huu John Maguli tayari amekuwa na ziara za kutembelea mikoa mbalimbali kabla na toka ateuliwe na CCM kuwa mgombea urais, kuna mambo kadhaa ambayo nimechunguza na kujiuliza kama kweli CCM ilifanya uamuzi sahihi kumteua Magufuli kuwa mgombea wake waburais.

Kwa mfano
1/Wakati wa uchukuaji fomu za kuomba kuteuliwa kugombea urais ndani ya CCM, Magufuli hakuonekana sana kama ni miongoni mwa watu wanaofaa kupeperusha bendera ya CCM, hakukuwa na mshtuko wala hamasa yoyote kutoka kwa wanaCCCM au wasio wanaCCM kuhusu ugombea wa Magufuli. Tofauti kabisa na wagombea wenzake kadhaa. Hakuna mwanasiasa asiyetaka kushangiliwa au kushabikiwa, na hatuamini kabisa kuwa Magufuli hakutaka kushangiliwa au kushabikiwa bali huenda ni mvuto duni wa kisiasa ndani ya CCM au vinginevyo.

2/Hata baada ya Magufuli kuteuliwa rasmi kuwa mgombea urais wa CCM na kufanya mikutano ya Hadhara mjini Dodoma, Dar, Zanzibar na Mwanza bado hatukuona mwangwi mzito wa mwitikio wa watu.
Kwa ujumla mikutano yote hiyo ilijaa makada wa CCM wakiwa na sare zao za kijani(wengi wao walikuwepo kwenye harakati za kumshabikia Lowassa wakati wakusaka wadhamini) wakiwa na sura zenye mashaka makubwa na tabasamu za kutengeneza. Wengi wetu tulitegemea makundi makubwa sana ya watu mbalimbali hususani wasiokuwa wanaCCM.

3/Mpaka sasa hatujaona kishindo cha mtikisiko wa kisiasa kwa upande wa upinzani katika kuhofia ujio wa Magufuli katika mbio za urais mwaka huu. Japokuwa UKAWA hawajatangaza rasmi mgombea wao lakini hatuoni Presha yoyote katika kuhofia nguvu za Magufuli kisiasa.

4/Mwitikio wa Makundi makubwa ya kijamii bado uko chini sana baada ya Magufuli kuteuliwa. Mpaka sasa wingu la kisiasa limegubikwa na kukatwa kwa jina la Lowassa tu, badala ya uteuzi wa Magufuli.
Kila mtu alishuhudia namna Lowassa alivyokuwa akitikisa kila mahali alipopita wakati tu, amechukua fomu kugombea urais.
Tukio la Lowassa kutangaza nia jijini Arusha lilikuwa ni tukio kubwa sana kiasi cha kusimamisha kabisa shughuli za watu katika Miji ya Arusha, Moshi na Manyara. Lakini huwezi amini Tukio la Magufuli kuteuliwa kugombea irais na CCM na kuja Dar na Mwanza halikushtua kitu chochote katika shughuli za watu za kila siku.
 
Mgombea urais kwa tiketi ya CCM mwaka huu John Maguli tayari amekuwa na ziara za kutembelea mikoa mbalimbali kabla na toka ateuliwe na CCM kuwa mgombea urais, kuna mambo kadhaa ambayo nimechunguza na kujiuliza kama kweli CCM ilifanya uamuzi sahihi kumteua Magufuli kuwa mgombea wake waburais.

Kwa mfano
1/Wakati wa uchukuaji fomu za kuomba kuteuliwa kugombea urais ndani ya CCM, Magufuli hakuonekana sana kama ni miongoni mwa watu wanaofaa kupeperusha bendera ya CCM, hakukuwa na mshtuko wala hamasa yoyote kutoka kwa wanaCCCM au wasio wanaCCM kuhusu ugombea wa Magufuli. Tofauti kabisa na wagombea wenzake kadhaa. Hakuna mwanasiasa asiyetaka kushangiliwa au kushabikiwa, na hatuamini kabisa kuwa Magufuli hakutaka kushangiliwa au kushabikiwa bali huenda ni mvuto duni wa kisiasa ndani ya CCM au vinginevyo.

2/Hata baada ya Magufuli kuteuliwa rasmi kuwa mgombea urais wa CCM na kufanya mikutano ya Hadhara mjini Dodoma, Dar, Zanzibar na Mwanza bado hatukuona mwangwi mzito wa mwitikio wa watu.
Kwa ujumla mikutano yote hiyo ilijaa makada wa CCM wakiwa na sare zao za kijani(wengi wao walikuwepo kwenye harakati za kumshabikia Lowassa wakati wakusaka wadhamini) wakiwa na sura zenye mashaka makubwa na tabasamu za kutengeneza. Wengi wetu tulitegemea makundi makubwa sana ya watu mbalimbali hususani wasiokuwa wanaCCM.

3/Mpaka sasa hatujaona kishindo cha mtikisiko wa kisiasa kwa upande wa upinzani katika kuhofia ujio wa Magufuli katika mbio za urais mwaka huu. Japokuwa UKAWA hawajatangaza rasmi mgombea wao lakini hatuoni Presha yoyote katika kuhofia nguvu za Magufuli kisiasa.

4/Mwitikio wa Makundi makubwa ya kijamii bado uko chini sana baada ya Magufuli kuteuliwa. Mpaka sasa wingu la kisiasa limegubikwa na kukatwa kwa jina la Lowassa tu, badala ya uteuzi wa Magufuli.
Kila mtu alishuhudia namna Lowassa alivyokuwa akitikisa kila mahali alipopita wakati tu, amechukua fomu kugombea urais.
Tukio la Lowassa kutangaza nia jijini Arusha lilikuwa ni tukio kubwa sana kiasi cha kusimamisha kabisa shughuli za watu katika Miji ya Arusha, Moshi na Manyara. Lakini huwezi amini Tukio la Magufuli kuteuliwa kugombea irais na CCM na kuja Dar na Mwanza halikushtua kitu chochote katika shughuli za watu za kila siku.

Km kuna pahala TISS walicheza kwa ufanisi na busara ni pale walipohakikisha jina la Lowasa linakatwa.Ingekuwa enzi zile,Edo angelikwisha pata ajali siku nyngi.Hyo iko pote duniani hata Us.Hata opp. Kunyimwa ushndı ni kazi ya TISS, to be fair hauwezi kukabidhi nchi kwa watu km Mbowe.TISS ndo inasaidia kuwajengea uwezo opp na baada ya muda nadhani watawapa nafasi wakishnda.Wanaimprove kila siku na watu wenye akili wanawajoin, tutafika.
 
ha ha ha...naona sasa vijana wamelipwa kuja mitandaoni kutuletea porojo.
ACHENI POROJO NA KUTUMIKA...
Lowasa mwenyewe ni hatari kwa afya yake binafsi...sembuse familia yake na watanzania.

Sikujua kabla kumbe jama ni hatari hata kwa afya yake mwenyewe! ngoja nimwombe mbowe asimpokee ukawa maana ataharisha maisha ya wengi nchini.
 
Sasa ulitaka kitengo waruhusu nchi iende kwa mafisadi , ili kina Rostam na Karamagi watambe kila Kona kila tenda wangechukua wao mpaka mabilioni yao yangerudi tungekuwa Hoi.

Kwa kifupi kitengo Walikuwa sahihi kukata jina, huwezi kukabidhi nchi kwa baba wa ufisadi.
 
Kabisa nakubali kupingana nayo, sio kipindi chote inakuwa sahihi. . .Nchi changa kidemokrasia elimu iko chini, purchasing power iko chini, inflation ya ajabu, rate of unemployement is acrueing. . . . . Hawa watu hawawezi kuwa na maamuzi sahihi asilani, wanakuwa influenced na vitu vingi ambavyo kama wangekuwa "free" hali isingekuwa hivyo. . .

Demokrasia gani kwa katiba hii ya sasa??!! Demokrasia gani kwa tume hii ya uchaguzi??!! Demokrasia gani kwa undugunization uliojaa katika vyama???!

Demokrasia inatumika na few eiltes na middle class kufanya maamuzi yao kwa mgongo wa wengi. . . .. .
.
hasante sana mkuu, "eti wamiliki wa vyombo vya habari waliweza kuishawishi selekali ikaondoa mswada wa dharula wa habari lkn kwa miswada mingie ilishindikana kuiondoa!"
 
Kuna vitu vinajitokeza kipindi hiki cha uchaguzi
ambavyo vinapaswa kuulizwa
je nikweli wananchi wa Tanzania ndio wasemaji wa mwisho wa masuala ya nchi hii?
au kuna watu kwa aakili zao na utashi wao wamejipa 'jukumu' hilo?

Kingunge alisema 'KITENGO' ndio kiliamua nani awe mgombea wa CCM na sio
wanachama......na Ukisoma gazeti la Raia Mwema wanasema watu wa 'usalama'
walimwambia Ngeleja awaambie wazanzibar kumchagua 'mgombea wa kitengo'
ndio akashinda....maswali yanajitokeza
1.kitengo kinaendeshwa na nani hasa?
2.Ni watu wangapi wanaofanya hayo maamuzi?
3.Ni kweli maamuzi yao yote ni kwa faidaya Taifa?
4.Wananchi wakipishana maamuzi na 'kitengo' maamuzi ya wananchi yataheshimiwa?
5.Nguvu ya 'kitengo' kwa tume ya uchaguzi ni halali?
6.kuna faida ya kushiriki uchaguzi huku 'kitengo' kimeshafanya maamuzi?
7.Je tuna demokrasia kweli au tunaruka ruka ttu na maigizo?
Amri ya Mkapa ilivyozima vurugu NEC - Kitaifa | Mwananchi
 
hapa inazungumziwa TISS kuegemea chama kimoja, ww unaleta mambo ya CIA kupanga nani aongoze nchi, democratic na republican wanabadilishana uongozi bila matatizo nyie mnakumbatia chama kimoja. maendeleo mtasubir miaka 1000

Usichokijua ni kwamba wote wawili Republican na Democrat wanamtumikia bwana mmoja,The Big Corporation/Corporate America. Marais,Maseneta na Makongresimani wanawekwa huko na hawa mabwana wakubwa.
 
Back
Top Bottom