Asante The Boss kwa mada hii muhimu. Nimepitia michango ya wenzangu waliotangulia, ni kweli kuwa ni wakati muafaka sasa tujadili na kushiriki kutengeneza nchi na taifa letu na historia itatuhukumu hivyo.
1. Kwa CCM suala la Urais kwao halina mjadala ni LAZIMA awe wa kwao hata kama italigharimu Taifa hili uhai wake wote. Hiyo ni siri iliyo wazi kwa miaka mingi tu.
2. Je ni mara ngapi tumewahi kusikia au kuona "viongozi wakuu" kama Rais, Waziri Mkuu, Wabunge na Mawaziri wakisema/kulalamika au kuonyesha "laiti kama ingekuwa ni uwezo/mamlaka yangu basi ninge......." Mifano iko mingi; mfano kauli ya Waziri Mkuu Pinda kuwa "wakiwashughulikia mafisadi nchi itayumba..." Hii inaonyesha kuwa kuna "nguvu" nyuma yao hao wanaonekana kwa macho kuwa "wakuu"; ambayo wao wenyewe wanaiogopa na kutumikia hiyo "nguvu" kwa hiari au shuruti, kwa kujua au kutokujua.
3. Kauli ya Kingunge ni nzito na ya ajabu sana kwa kuzingatia historia, uhusiano na hadhi yake CCM.
Kwangu mimi kauli ile ina vitu vikubwa vine (tofauti na watu waliojitokeza kusema kuwa mzee yule alikuwa anaitishia CCM nyau).
a) Kitengo ni kitu halisi "real"
b) Kitengo, pamoja na kuwa ni halisi, lakini sio kinachofikiwa na wengi (not accessible to all except for a selected few)
c) Kitengo ni fumbo pana na refu (codeword and terible mystery)
d) Kitengo hakina mipaka (kinaweza kuanzia ndani ya CCM lakini hakiishi huko na kinyume chake)
4. Matunda yake yako wazi katika historia ya nchi yetu. Ujinga umeendelea kutusumbua, umaskin umeendelea kuongozeka, maradhi, madawa ya kulevya, rushwa na ufisadi vimeongezeka kila siku na sasa vinatishia mustakabali wa nchi nzima.
5. Ugumu wa fumbo ni pale (kwa mujibu wa Kingunge) Kitengo ndio "kilipika/kilitengeneza" kashfa ya Richmond ili kumtoa Lowassa kutoka kuwa WM (hatujui hasa kwanini), lakini kwa jinsi kilivyo cha ajabu, nusura kiiangushe kabisa Serikali ya Kikwete mwaka 2006! Inaonesha kitengo kiko nje/juu ya mamlaka ya Mkulu. Ni kama vile duara (cycle) huoni mwisho na mwanzo ni mgumu pia kuuona!
HITIMISHO (kwa sasa)
i. TISS, Idara ya Ulinzi/Usalama/Ujasusi wa Chama, Ikulu, Bunge ni sehemu ya Kitengo lakini Kitengo sio Umma (Wananchi wa Tanzania.
ii. Kitengo kipo kiuhalisia ingawa hakipo kwa mujibu wa Katiba yetu ya JMT.
Fumbo bado linataka tuendele mbele zaidi kuchunguza, kudadisi na kuwa wajasiri zaidi ili tusimezwe na "Kitengo"