3.Ni kweli maamuzi yao yote ni kwa faidaya Taifa?
Ah wapi! Ukibahatika kutembelea sehemu mbalimbali za nchi ndo utagundua kwamba maamuzi 'yao' mengi wala si kwa manufaa ya taifa.
Sina uhakika sana na hili la kiinua mgongo cha wabunge na sijalisikia tena tokea karibu wiki mbili zilizopita lakini kama kweli hicho kitengo dhima yake kuu ni kulinda maslahi ya taifa basi kingeingilia kati ili hayo mabilioni ambayo yanadaiwa wabunge watalipwa yaende sehemu ambazo zina uhitaji mkubwa zaidi.
4.Wananchi wakipishana maamuzi na 'kitengo' maamuzi ya wananchi yataheshimiwa?
Thubutu! Watanzania wa kizazi hiki hawana ujasiri wala uthubutu wa kupishana na maamuzi ya 'kitengo'. Majuzi tu hapa tumeona jinsi ambavyo rafu imechezwa hadi Magufuli akawa railroaded kuwa mteule wa chama na yule ambaye iliaminika ndiye aliyekuwa chaguo la wengi kutoselewa mbali tena kwa udhalilishaji wa hali ya juu. Walipojitokeza watu wawili watatu kujaribu kupinga kilichotokea walizimwa haraka sana na wakarudishwa mstarini.
5.Nguvu ya 'kitengo' kwa tume ya uchaguzi ni halali?
Sisi hatuna tume huru ya uchaguzi. Hiyo ambayo tunayo sasa ni extension ya 'kitengo' tu. Hebu tumia tu hata busara zako za kawaida [common sense]. Ni nani ambaye huiunda hiyo tume? Mwenyekiti wa hiyo tume na hao wenzake huwa wanapatikanaje?
6.kuna faida ya kushiriki uchaguzi huku 'kitengo' kimeshafanya maamuzi?
Kwa ujumla mimi sioni faida yoyote ile hususan kwenye urais. Kwa jinsi ambavyo mambo yalivyo hivi sasa CCM kuja kushindwa na wapinzani haiwezekani hata kidogo. Kutegemea mwenyekiti wa tume ya uchaguzi aliyeteuliwa na rais/ mwenyekiti wa CCM kumtangaza mshindi wa kiti cha urais mgombea wa upinzani ni sawa na kutegemea ngamia apite kwenye tundu la sindano.
Kama kuna anayedhani hiyo tume ya uchaguzi siyo extension ya kitengo namsihi arudi kumwangalia mmoja wa watangaza nia wa CCM - Jaji Agustino Ramadhani. Huyu bwana nadhani alikuwa ni makamu mwenyekiti wa tume ya uchaguzi kuanzia mwaka 1993 hadi 2002 na kuanzia 2002 hadi 2007 alikuwa makamu mwenyekiti wa tume ya uchaguzi ya Zanzibar [eti hawa watu nao wana tume yao ya uchaguzi!!].
Hiyo inatueleza nini kuhusu hiyo inayoitwa tume ya uchaguzi? Je, ina maana tume nzima imejaa makada wa CCM? Mimi nadhani ni hivyo.
7.Je tuna demokrasia kweli au tunaruka ruka ttu na maigizo?
Ni maigizo tu. Demokrasia gani hiyo isiyotoa fursa sawa kwa washindani wote? Hata katiba ya nchi inayoendana na misingi mikuu ya kidemokrasia hatuna. Eti juzi juzi tu hapa ndo tumestuka na kuona umuhimu wa kuandika katiba mpya.
Kwa nini hilo halikufanyika hapo awali kabisa mwaka 1992 tulipoingia kwenye siasa za vyama vingi?
Na kusema ukweli Tanzania wala hatuna siasa za vyama vingi. Siasa zetu ni za chama kimoja ila kuna mazingaombwe yanayofanya watu wadhani kwamba tuna siasa za vyama vingi. Hatuna.
Wiki ilopita tumeshuhudia jinsi ambavyo nadhari karibu ya Watanzania wote ilivyoelekezwa huko Dodoma katika shauku ya kutaka kujua rais ajaye atakuwa nani.
Hakuna ubishi wowote ule kuwa rais wa 5 wa Tanzania ni John Magufuli.
Hata kupatikana kwake hakukuwa kwa demokrasia. Kinachosubiriwa sasa ni kukamilishwa tu kwa taratibu [igizo la uchaguzi mkuu hapo Oktoba] na yeye kuapishwa, basi.