Nchi imekauka, mambo hayaendi...

Nchi imekauka, mambo hayaendi...

Fanyeni kazi acheni blah blah
Wanaotoa kauli hii ni waajiriwa ambao mwisho wa mwezi anasubiria mshahara. Siku akifukuzwa kazi anakuwa kama chizi vile. Acha hiyo kazi halafu ingia kitaani ufanye kazi kwa sbb huku kuna kazi nyingi sana tena zinazilipa. Wengi wanaosema kauli kauli km yako wanamtindio wa ubongo.
HAKUNA BINADAMU ASIYEPENDA KUFANYA KAZI. PESA TAMU.
 
ok sawa kwa ujumbe wako kama vipi tupe na mrejesho wa hali ya maisha kule Venezuela amabako watu wananyang'anyana makombo na mbwa kwenye majalala
Pole sana. Kwahiyo ww unafurahia kuona Tanzania inakuwa km Venezuela, Shida ya wafrika wengi wamezoea shida umasikini. Ukiona ww unalala njaa na tajiri jirani yako analala njaa roho yako inaridhika.
Sikulaumu ila una roho ya kimasikini na umezoea shida
 
Hii ni dalili ya watu waliokuwa wamedeka katika mfumo wa utawala wa kifisadi... kama ulikuwa unanyongewa kila siku sasa unaambiwa chinja... hujui kisu kinashikwa vipi.. Jiji la Dar lina matatizo yake na hayaishi leo.. mojawapo ni kuwa watu wake wamezoea uchafu kiasi kwamba kuishi bila uchafu kunaonekana ni kama kuwa "mzungu" au kuwa majuu!

Mzee Mwanakijiji; with due respect to you. Ninaelewa mtu kama stroke au jingalao kuandika ulichokiandika. You may have changed your views -for that you commanded respect and admiration- rightly and I dare say deservedly.

But I never thought you would stoop so low that you would insult so many Tanzanians that way! Kuna mkulima gani (na tunaambiwa 70% ya Watanzania ni small-hold farmers) aliezoea vya kunyonga? Ina maana workforce yote kabisa nchi hii (waalimu, field agronomists, manesi na lower cadres wote) walikuwa "wapiga dili". Am sorry Sir, but I thought you were more intelligent than that!!
 
Ok hali ni ngumu, je umechukua hatua gani kujikwamua? Kulalamika pekee sio suluhu, chukua hatua, jikwamue.
 
Wanaotoa kauli hii ni waajiriwa ambao mwisho wa mwezi anasubiria mshahara. Siku akifukuzwa kazi anakuwa kama chizi vile. Acha hiyo kazi halafu ingia kitaani ufanye kazi kwa sbb huku kuna kazi nyingi sana tena zinazilipa. Wengi wanaosema kauli kauli km yako wanamtindio wa ubongo.
HAKUNA BINADAMU ASIYEPENDA KUFANYA KAZI. PESA TAMU.
Mkuu na heshimu mawazo yako..Njoo Bukoba tulime vanilla na Kahawa
 
Aaahh shogaangu hayo si maneno sasa,.nikiuza nyumba ina maana narudi kwetu ikwiriri,maana hela ya kupanga tena ntatoa wapi??
Ukiuza nyumba, pesa unayoipata unatatulia shida iliyokufanya uuze nyumba, pesa inayobaki unalipa kodi ya nyumba ya mwaka mzima na kufungua genge mtaani. Maisha yanasonga.

Sikuombei yakukute mwanakwetu..
Ndugu yangu anakusabahi, anadai hali halali kwaajili yako
 
Nani huyo hali halali😄😄...lol
 
Hii ni dalili ya watu waliokuwa wamedeka katika mfumo wa utawala wa kifisadi... kama ulikuwa unanyongewa kila siku sasa unaambiwa chinja... hujui kisu kinashikwa vipi.. Jiji la Dar lina matatizo yake na hayaishi leo.. mojawapo ni kuwa watu wake wamezoea uchafu kiasi kwamba kuishi bila uchafu kunaonekana ni kama kuwa "mzungu" au kuwa majuu!

Yaani wananchi wa kipato cha chini walie na hali ngumu ya maisha halafu wewe useme walikuwa wanadeka?
Sijawahi kuona ukitoa kauli insensitive kama hii!.

Hali ngumu ya Maisha mtaani ni result ya sera za uchumi zilizofeli na uendeshaji wa mambo vibaya wa mheshimiwa na si kudeka kwa watu!.

1. Kutokuongeza mishahara na nyongeza za kila mwaka ambazo ni stahiki za wafanyakazi kwa mujibu wa sheria

2. Kumismanage ishu ya korosho, kawatia umasikini wakulima

3. Kutokulipa wafanyabiashara kwa huduma zao walizotoa kwa serikali/taasisi zake

4. Kuhamisha serikali Dodoma bila kujipanga, matokeo yake makusanyo dar yameshuka na Dodoma haijajipanga kuweza kuaaccomodate hospitality business kwa hiyo overall makusanyo kushindwa kufikia malengo

5. Sera zake alipoingia tu mara ya kwanza ziliiyumbisha bandari naona sasa ndo wanakumbuka kuondoa tozo mbalimbali kwa mizigo ya congo, wacongo walishatuhama , wakagamia mombasa

6. Sera zake za kuminya uhuru na demokrasia matokeo yake wahisani kuacha kutoa hela

7. Kutumia pesa bila kuwa na malengo yaliyofanyiwa tafiti vya kutosha, ukijisikia mradi huu unapeleka hela bila hata kufanya money for value analysis ya kutosha, kuipitisha bungeni na kupata mawazo na kuwa allocated budget, matokeo yake baadhi ya miradi kama ndege imepeleka nje mihela yetu mingi tu ya kigeni

Sasa katika hali kama hiyo utamlaumu vipi raia anayeshindia karanga za mia mbili kutwa kuwa alikuwa anadeka?

Acha dharau mkuu, unaweza kuitetea serikali ya CCM kwa mambo mengine lakini siyo at the expense ya well being ya watu!
 
Back
Top Bottom