Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 13,504
- 51,099
Nimetembelea jiji la Dar es salaam, kwa kweli hali niliyokutana nayo inasikitisha sana. Mpaka ikabidi nijiulize hii wizara inayohusika na mazingira iko wapi na inafanya nini?
1. Mifuko ya Plastic mitaani imekuwa mingi sana.
Miaka michache iliyopita wakati wa Utawala wa Hayati Magufuli serikali ilijaribu kupunguza kiwango cha mifuko ya plastic nchini, kwa kweli hilo lilisaidia sana. Lakini hivi sasa mifuko ya plastic imerudi tena, na inazagaa mitaani.
Kuna mifuko ya aina fulani ya plastic inauzwa kati ya sh 300 na 500, iliyoletwa kureplace mifuko ya nailoni nayo imekuwa kero sana. Imezagaa tele mitaani.
Aina nyingine za mifuko ya plastic niliyoiona ni mifuko ya sabuni ya unga, vifungashio mbalimbali
2. Chupa za Plastic zimekuwa nyingi sana.
Sasa hivi kuna chupa za energy drinks, Vikombe vya plastic vya juice, chupa za plastic za soda, hizi zimezagaa mitaani kama njugu. Kwa kweli kila mtaa unaopita hivi sasa unakuta chupa za namna hiyo zimezagaa
3. Foil za chakula za takeaway
Hili nalo ni tatizo kubwa mno. Siku hizi mtu akiagiza chakula anafungiwa kwenye take away au foil. Hizi taka nazo ni ngumu sana kuoza. Leo hii ukizunguuka mitaani, kumejazana hizi foil
4. Chupa za pombe
Leo hii wauza pombe zikiwemo pubs hawajisumbui kutafuta mahali sahihi pa kutupa chupa zao baada ya wateja kunywa pombe. miongoni mwa chupa hizo ni zile za Wine, Pombe kali kama vile K-Vant na nyinginezo. Matokeo yake wanavizia usiku wanaenda kutupa katika mitaa ya jirani
4. Uchomaji taka usio salama kwa afya wakithiri.
Leo hii ukipita katika mitaa, kwa sababu ya accumulation ya taka, basi raia wanajichomea taka kila mtu kadri anavyotaka. Lakini kitendo hicho ni hatari sana,baadhi ya taka kama vile plastic na foils zinatoa kemikali ambazo ni hatari sana kwa mapafu na inaweza kupelekea magonjwa ya kutopumua vizuri au kansa. Japo kufanya hivyo ni kinyume cha sheria za serikali za mitaa,lakini serikali insonekana imelala, watu wanachoma taka na kuhatarisha afya ya jamii kwa kiwango cha kutisha sana.
5. Upikaji chakula usiozingatia afya ya walaji.
Leo hii ukizunguuka mitaani kuna staili ya mapishi ambayo ni hatari sana kwa afya. Mama lishe wanapika wali huku wakiufunikia manailoni. Wao wanaamini wakifanya hivyo ndo unaiva haraka.Lakini athari ya hayo ni makemikali ya plastic baasa ya kupata joto kuvujia ktk chakula na kupelekea maradhi mengi ikiwemo kansa. Sasa hivi nchini kuna ongezeko kubwa la ugonjwa wa kansa, huenda miongoni mwa sababu ni lifestyle ya namna hii.
Huu ni wakati wa serikali kuamka. Nchi kwa kasi sana inageuka jalala. Waziri wa Mazingira uko wapi, timiza wajibu wako!