Mchambuzi,
Naona unakwepa ukweli uliosimama wazi kabisa.. AFYA ni biashara hivyo yote uloandika hapo juu ni matokeo ya kunedesha biashara huduma muhimu kama AFYA wakati wananchi wake hawana uwezo. Kwa nini Kiogoma hakuna Madaktari au Hospital za kutosha?.. Kwa sababu hakuna biashara nzuri kuliko Moshi, Arusha na Dar..
Swala la AFYA kwa nchi kama yetu halikutakiwa kabisa kuwa ktk mfumo uliopo ambao una jenga maradhi zaidi ili wananchi waende kutibiwa Hospital. Mtu anaumwa malaria atafanyiwa vipimo vya kila aina ikiwa hakuomba yeye afanyiwe kipimo cha Malaria. Leo hii Tanzania unatakiwa kwenda Hospital unajua unaumwa nini, laa sivyo utatozwa maelfu na mwisho wa siku utaambiwa na Dakatari huyo huyo Jioni au kesho njoo katika zahanati yangu iko Buguruni.
This is reality mkuu wangu mnajaribu sana kuficha madhambi ya mchezo mzima wanaofanyiwa wananchi kwa kuilaumu serikali wakati UFISADI umekuwa sehemu ya maisha yetu. Kweli serikali imeshindwa tena sehemu zote za uongozi na ndio maana imefilisika.. au hamjaambiwa hilo?.
Hakuna daktari mwenye hali mbaya Dar au Tanzania naomba nionyesheni hata mmoja ambaye hana hata nyumba na gari la kifahari!..Na kama yupo basi huyo ndio kamaliza tu masomo na kaanza kazi lakini within next 5 yrs sii mwenzako tena.
Ni wizi mtupu toka mashuleni hadi Hospital tunafuga maradhi kama mbegu ya kuzaa wagonjwa.
Mkuu Mkandara,
Ukinisoma between the lines, utabaini kwamba mimi na wewe tunaongea kitu hicho hicho. Kwa mtazamo wangu, lugha zetu sawa, inawezekana tunachopishana ni 'lafudhi' tu. Vinginevyo, nia yangu ilikuwa sio zaidi ya ile iliyolenga to 'stimulate' a debate juu ya jambo hili, tuweze kuliangalia tatizo hili kwa undani zaidi. In that line, nikawasilisha takwimu za sekta ya afya kama zilivyo, ili kwa pamoja tusaidiane kubaini tatizo lipo wapi, na kupendekeza suluhisho la kudumu. Kwa kweli, sijawa as subjective katika maelezo yangu ya awali kwani - sijatetea sekta binafsi, sijatetea sekta ya umma, na wala sijatetea sekta ya NGO, zaidi ya kuelezea hali halisi kama ilivyo, na kumalizia kwa maswali.
Lakini kuna vitu viwili tu ambavyo ningependa kuvijadili, kama majibu yangu kwa hoja zako.
1. Kwanza ni kuhusu hoja yako kwamba "Afya ni Biashara." Nimeipenda hoja hii, kwani katika thread yangu nyingine, nilizungumzia kwa kirefu vacuum ya ideology inayolikabili taifa letu, especially in practicalities za vyama vyetu vya siasa ambavyo malengo yake ni kushinda chaguzi, kuunda serikali, na kuja na sera zenye lengo la kuboresha maisha ya watanzania, sera zitokanazo na itikadi, sio sera zitokanazo na leo waziri au katibu mkuu ameamkaje.Sasa, kuhusu
Afya ni Biashara, hii ni itikadi ya kihafidhiana (Conservatism), unlike mtazamo kwamba Afya ni Huduma msingi katika Jamii ni itikadi ya mrengo wa kati kwa kiasi fulani, lakini zaidi mirengo ya kushoto. Kwahiyo iwapo wewe imani yako kuhusu Afya ndio hiyo, basi tofauti yangu na ewe ni ya ki-itikadi tu, na tofauti hii inajadilika, hakuna wa kukosea au wa kupatia, kama ulivyojaribu pendekeza. Ni suala la kujenga tu hoja.
Iwapo huo ndio mtazamo wako juu ya Afya i.e. kwamba ni biashara, ningependa tuendeleze mjadala huu, na naomba unielezee zaidi biashara hiyo itaendaje katika Tanzania ambapo suala la kuiachia sekta ya afya iendeshwe na nguvu za soko tayari ilishapelekea market failure, na ndio maana hao hao waliokuwa na mtazamo wa afya ni biashara (WorldBank na IMF), wakairudisha serikali katika kutoa huduma hiyo - again, kutokana na market failure in that sector.
Lakini Mkuu, katika mijadala mingi sana humu, kama vile nimekuwa nakuelewa wewe na mimi tupo katika mrengo mmoja ki-hoja yani, mrengo wa kushoto. Sikutegemea ungekuwa mrengo wa kihafidhiana juu ya suala hili la afya. Lakini inawezekana kwamba nilikuwa sikusomi vizuri awali, au sijakusoma vizuri katika hoja yako ya leo.
2. Kuna suala la pili ambalo ningependa pia kulizungumza. Linahusu kauli yako ifuatayo:
Kweli serikali imeshindwa tena sehemu zote za uongozi na ndio maana imefilisika.. au hamjaambiwa hilo?.
Mkuu Mkandara, Je, maana yako hapo ni kwamba Mimi Mchambuzi ni Sehemu ya Utawala wa Serikali ya Jakaya Mrisho Kikwete? au nimekuelewa sivyo? Kama ulimaanisha hivyo, naomba tu uelewe kwamba, ingawa nimevaa shati la Chama Cha Mapinduzi, Mchambuzi ni mtu aliyejiajiri mwenyewe kujitafuita riziki yake ili mradi siku ziende, kwahiyo nipo kwenye sekta binafsi, sehemu ndogo ikiwa kwenye sekta isiyo rasmi, lakini kubwa zaidi kwenye sekta iliyo rasmi na inayolipa kodi. Mimi sina madaraka ya aina yoyote katika chama cha mapinduzi, kuanzia shina hadi taifa; Na pia sina madaraka yoyote katika Serikali ya CCM, kuanzia serikali ya kijiji, serikali ya mtaa, serikali kuu, na wala utumishi wowote wa umma. Mimi sina cha zaidi ya uanachama wa CCM niliyelipia ada zangu zote kama wanachama wengine wote huko mijini na vijijini.
Naomba Kuwasilisha Mkuu.