"Nawasalimu kwa Jina la Jamhuri - Kazi Iendelee" ifutwe tumrudie Mungu

Napendekeza hii salamu ifutwe tumurudie Mungu. Sababu nyingine ni hizi hapa.

1. Salamu ya Mungu inaliinua taifa. Mungu anakuwa karibu nasi siku zote hata kipindi cha Corona.

2. Salamu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kazi iendelee inakosa consistency. Tutajikuta kila awamu tunabadili salamu. Taifa lazima tuwe na salamu Moja kama alama yetu.

3. Hii salamu ya kazi iendelee haitikiwi na watu wote. Maana hii salamu inategemea na utendaji wa kazi wa serikali na jinsi mtu anaridhika na hiyo Kazi. Kama kazi hazitafanyika kiasi cha kuridhisha basi mtu hawezi kuitikia. Ila salamu ya Mungu wote twaitikia. Na wale wasio amini Mungu walishazoea.

Bwana Sifiwe, Asalamu Aleikumu
Ukusoma andiko la ,"usilitaje jina la bwana mungu wako ovyo" , unajua hekima ya andiko hilo
 
Muache adanganywe na Askofu Kakobe na wa aina yake. Wajasiria Neno la Mungu ambao wanalipindisha kwa faida yao.

Rais anayetaka kuombewa kwa Mungu lakini hataki kuhimiza anaowaongoza wamtegemee Mungu. Bali anawaongoza yeye akiwa mfano kuvaa barakoa na kuitegemea huku akifanya kila juhudi kuleta chanjo ya kuharibu uumbaji wa Mungu. Amewakwaza hata wasaidizi wake maana kama unataka ugali mezani hunabudi na wewe uivae hiyo barakoa na hivyo hivyo itakuwa kwa chanjo ikifika.
 
Sal
Ni ushamba tu unakusumbua na mazoea mabaya, mungu hatukuzwi kwa salamu bali mungu anatukuzwa kwa matendo mema

Kuamini uwepo wa mungu sio kwa kusalimia bwana yesu asifiwe tu jinga wewe bali unashi maisha gani ya kukili uwepo na utii kwa mungu kwa matendo

Huyo aliye kuwa anasalimia kwa salamu dini zote alifanya kipi zaid ya kuteka na kuua na matusi ya jukwaani pamoja na kudhulumu haki za wengine? Acheni kuishi kwa kukalili.

Ama nayo ni tendo.
 
Kuchukua salaam za kidini na kuzifanya salaam za kisiasa ni utapeli. Lini umeingia Msikitini ukamsikia Shehe/Imamu akisalimia Asalaam aleikum-Bwana Yesu asifiwe kwa pamoja, au vivyo hivyo kwa mapadri na Wachungaji? Sasa hili la kuchanganya salaam za madhehebu tofauti tena likifanywa kisiasa lina baraka gani?

Leo tumlazimishe Rais mwenye imani ya Kiislamu atoe salaam ya Kikristo hata kama imani yake binafsi haitambui kusifiwa kwa Yesu Kristo? Au tumwambie Makamu wa Rais aanze kusalimia kwa salaam iliyoasisiwa kiislamu wakati dhehebu lake haliitambui?

Kama ni hivyo itungwe sheria viongozi wote wa dini na waamini wao waswalipo/wasalipo wazitaje salaam zote kama mnavyotaka Viongozi wafanye majukwaani. Tusiwaache viongozi wabebe dhambi tusiyoitaka sisi kama ipo.
Wala hawezi mtu kusema , Yesu ni Bwana, isipokuwa katika Roho Mtakatifu (1 Cor 3)
 
Kwanza kusema nawasalimu kwa jina la Jamhuri maanake hatuamini uwepo wa MUNGU, ni dhihaka kubwa sn mbele za MUNGU.
Ujinga tu unataka kulazimsisha wote waamini mungu kwani ni sheria ya nchi? Nchi hii haina dini na katiba inatambua hilo

Mungu hatukuzwi kwa salamu bali matendo mema

Vipi yule aliye kuwa anasalimulia kwa salamu za kidini halafu anateka na kupoteza wapinzani wake?
 
Binadamu wote sio wakamilifu .ukiona unashindwa kutaja salamu ya dini ya mwenzako jua una tatizo na uongozi wako unatia mashaka.
 
Napendekeza hii salamu ifutwe tumurudie Mungu. Sababu nyingine ni hizi hapa.

1. Salamu ya Mungu inaliinua taifa. Mungu anakuwa karibu nasi siku zote hata kipindi cha Corona.

2. Salamu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kazi iendelee inakosa consistency. Tutajikuta kila awamu tunabadili salamu. Taifa lazima tuwe na salamu Moja kama alama yetu.

3. Hii salamu ya kazi iendelee haitikiwi na watu wote. Maana hii salamu inategemea na utendaji wa kazi wa serikali na jinsi mtu anaridhika na hiyo Kazi. Kama kazi hazitafanyika kiasi cha kuridhisha basi mtu hawezi kuitikia. Ila salamu ya Mungu wote twaitikia. Na wale wasio amini Mungu walishazoea.

Bwana Sifiwe, Asalamu Aleikumu
1. Tungekuwa tunaamini wote kwenye Mungu mmoja mwenye sifa sawa ingewezekana lakini kila dini wanamwabudu Mungu mwenye sifa tofauti na mwingine.
 
Siajajua nia ilikuwa ipi, lakini salam hii inatukwaza wengi...
 
1. Tungekuwa tunaamini wote kwenye Mungu mmoja mwenye sifa sawa ingewezekana lakini kila dini wanamwabudu Mungu mwenye sifa tofauti na mwingine.
Basi tusalimiane tu habari za siku au hamjambo? Basi
 
Hapana lazima tuwe na salamu yenye kujenga uzalendo kwenye nchi yetu

Uzalendo umepotea sana tunaabudu nchi nyingine mfano maras watanzania wanavaa na kuitukuza bendera ya ethiopia, kuna wengine wanavaa bendera za marekani na cha ajabu siku za karibuni akina dada wana vaa bracelets zenye rangi na bendera ya kenya. Huo ni unyani (apedomia) kuacha kutukuza cha kwako unatukuza cha mtu mwingine. Hivyo salamu hii kwa sasa ni muhimu sana kwa taifa tulipokuwa rumefikia kila kiongozi au mtu alikuwa anaona salamu ya dini yake ni bora zaidi na kulazimisha kusalimia hata watu ambao imani hiyo hawaijui
 
Salamu hii "nawasalimu kwa jina la jamhuri ya muungano wa Tanzania" ni salamu bora kabisa na iendelee! Tuache unafiki kujifanya kama taifa ili la kidini! Kwanza peleka salamu kwa wachungaji wako waambie:-
1) waache sala/maombi marefu kipindi cha hafla, zinachosha!
2)waache tabia ya kuwasimamisha watu, eti "simameni tuombe"
3) waache tabia ya kuwaambia watu wafumbe macho tuombe!
Wajitambue wapewapo nafasi, pale pana mkuu wa Nchi nani afumbe macho? Unataka kufanya nini?
NB; ikibidi ni mkristo mmoja na mwisilamu mmoja, suala la madhehebu watajiwakilisha!
 
Ujinga tu unataka kulazimsisha wote waamini mungu kwani ni sheria ya nchi? Nchi hii haina dini na katiba inatambua hilo

Mungu hatukuzwi kwa salamu bali matendo mema

Vipi yule aliye kuwa anasalimulia kwa salamu za kidini halafu anateka na kupoteza wapinzani wake?
Kasafishe kwanza njia yako kuu ya kupumulia ndiyo urudi hapa
 
Ujinga tu unataka kulazimsisha wote waamini mungu kwani ni sheria ya nchi? Nchi hii haina dini na katiba inatambua hilo

Mungu hatukuzwi kwa salamu bali matendo mema

Vipi yule aliye kuwa anasalimulia kwa salamu za kidini halafu anateka na kupoteza wapinzani wake?

Ila chanjo ikiwa kitanda kwa kitanda sio tatizo. Na wenye hekima walitumia salamu hizi kwenye hadhara maana walio wengi kati ya wahudhuriaji ni waunini wa Kikiristo ima wa Kiislamu, wengi wape.

Unakataa kutumia hizi salamu lakini unasema kwenye hotuba yako nianze kwa kumshukuru 'Mnyezi Mungu.' Unafiki haujawahi kulipa hata mara moja.
 
Kuchukua salaam za kidini na kuzifanya salaam za kisiasa ni utapeli. Lini umeingia Msikitini ukamsikia Shehe/Imamu akisalimia Asalaam aleikum-Bwana Yesu asifiwe kwa pamoja, au vivyo hivyo kwa mapadri na Wachungaji? Sasa hili la kuchanganya salaam za madhehebu tofauti tena likifanywa kisiasa lina baraka gani?

Leo tumlazimishe Rais mwenye imani ya Kiislamu atoe salaam ya Kikristo hata kama imani yake binafsi haitambui kusifiwa kwa Yesu Kristo? Au tumwambie Makamu wa Rais aanze kusalimia kwa salaam iliyoasisiwa kiislamu wakati dhehebu lake haliitambui?

Kama ni hivyo itungwe sheria viongozi wote wa dini na waamini wao waswalipo/wasalipo wazitaje salaam zote kama mnavyotaka Viongozi wafanye majukwaani. Tusiwaache viongozi wabebe dhambi tusiyoitaka sisi kama ipo.
Umenena mkuu.., yaonesha mleta mada ameubaka ufahamu wake
 
Napendekeza hii salamu ifutwe tumurudie Mungu. Sababu nyingine ni hizi hapa.

1. Salamu ya Mungu inaliinua taifa. Mungu anakuwa karibu nasi siku zote hata kipindi cha Corona.

2. Salamu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kazi iendelee inakosa consistency. Tutajikuta kila awamu tunabadili salamu. Taifa lazima tuwe na salamu Moja kama alama yetu.

3. Hii salamu ya kazi iendelee haitikiwi na watu wote. Maana hii salamu inategemea na utendaji wa kazi wa serikali na jinsi mtu anaridhika na hiyo Kazi. Kama kazi hazitafanyika kiasi cha kuridhisha basi mtu hawezi kuitikia. Ila salamu ya Mungu wote twaitikia. Na wale wasio amini Mungu walishazoea.

Bwana Sifiwe, Asalamu Aleikumu
Kwani kusema Bwana Asifiwe nayo ni salamu?? Em tuweni serious kidogo jamani
 
Back
Top Bottom