"Nawasalimu kwa Jina la Jamhuri - Kazi Iendelee" ifutwe tumrudie Mungu

JF Member

JF-Expert Member
Dec 14, 2014
4,674
2,000
Napendekeza hii salamu ifutwe tumurudie Mungu. Sababu nyingine ni hizi hapa.

1. Salamu ya Mungu inaliinua taifa. Mungu anakuwa karibu nasi siku zote hata kipindi cha Corona.

2. Salamu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kazi iendelee inakosa consistency. Tutajikuta kila awamu tunabadili salamu. Taifa lazima tuwe na salamu Moja kama alama yetu.

3. Hii salamu ya kazi iendelee haitikiwi na watu wote. Maana hii salamu inategemea na utendaji wa kazi wa serikali na jinsi mtu anaridhika na hiyo Kazi. Kama kazi hazitafanyika kiasi cha kuridhisha basi mtu hawezi kuitikia. Ila salamu ya Mungu wote twaitikia. Na wale wasio amini Mungu walishazoea.

Bwana Sifiwe, Asalamu Aleikumu
 

Bila bila

JF-Expert Member
Dec 20, 2016
15,232
2,000
Kuchukua salaam za kidini na kuzifanya salaam za kisiasa ni utapeli. Lini umeingia Msikitini ukamsikia Shehe/Imamu akisalimia Asalaam aleikum-Bwana Yesu asifiwe kwa pamoja, au vivyo hivyo kwa mapadri na Wachungaji? Sasa hili la kuchanganya salaam za madhehebu tofauti tena likifanywa kisiasa lina baraka gani?

Leo tumlazimishe Rais mwenye imani ya Kiislamu atoe salaam ya Kikristo hata kama imani yake binafsi haitambui kusifiwa kwa Yesu Kristo? Au tumwambie Makamu wa Rais aanze kusalimia kwa salaam iliyoasisiwa kiislamu wakati dhehebu lake haliitambui?

Kama ni hivyo itungwe sheria viongozi wote wa dini na waamini wao waswalipo/wasalipo wazitaje salaam zote kama mnavyotaka Viongozi wafanye majukwaani. Tusiwaache viongozi wabebe dhambi tusiyoitaka sisi kama ipo.
 

Bufa

JF-Expert Member
Mar 31, 2012
6,890
2,000
Hii nchi ni ya watu wote sio waamini Mungu tu. Hivyo kunasibisha kila kitu na Mungu ni kuwakosea wasioamini uwepo wake.

Kazi iendelee ni slogan ya Mama akija Rais mwingine atakuja na slogan yake. Hakuna tatizo. Hatuwezi kuwa na salamu moja awazo tofauti.

Mfano US; Obama - Yes, we can/Change we need. Trump - MAGA. Biden - Build back better/Restore The Soul of The Nation.
 

Huihui2

JF-Expert Member
Jan 5, 2012
1,684
2,000
Itakuwaje kwa wasioamini dini na wenye miungu tofauti na Mungu wako?
 

_KINGO_

JF-Expert Member
Apr 17, 2021
215
1,000
Hapana. Tusiweke dini kwenye siasa. 'Bwana Asifiwe' na 'Tumsifu Yesu...' kiuhalisia hata siyo salamu (yaani mtu kutaka kumjulia hali mwemzie kama ilivyo 'habari yake?') na sielewi ilikuwaje kuwaje mpaka tunaziona hizi kauli ni salamu. Pia huwa sipendi vile 'Salam Aleikum' inaonekana kutumiwa na dini ya Kiislam wakati mimi naona ni lugha tu ya kIARABU. Hata Wakristo wanaoongea lugha ya Kiarabu husalimiana hivyo.
 

polokwane

JF-Expert Member
Dec 16, 2018
1,843
2,000
Kwanza kusema nawasalimu kwa jina la Jamhuri maanake hatuamini uwepo wa MUNGU, ni dhihaka kubwa sn mbele za MUNGU.
Ni ushamba tu unakusumbua na mazoea mabaya, mungu hatukuzwi kwa salamu bali mungu anatukuzwa kwa matendo mema

Kuamini uwepo wa mungu sio kwa kusalimia bwana yesu asifiwe tu jinga wewe bali unashi maisha gani ya kukili uwepo na utii kwa mungu kwa matendo

Huyo aliye kuwa anasalimia kwa salamu dini zote alifanya kipi zaid ya kuteka na kuua na matusi ya jukwaani pamoja na kudhulumu haki za wengine? Acheni kuishi kwa kukalili.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom