"Nawasalimu kwa Jina la Jamhuri - Kazi Iendelee" ifutwe tumrudie Mungu

Napendekeza hii salamu ifutwe tumurudie Mungu. Sababu nyingine ni hizi hapa.

1. Salamu ya Mungu inaliinua taifa. Mungu anakuwa karibu nasi siku zote hata kipindi cha Corona.

2. Salamu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kazi iendelee inakosa consistency. Tutajikuta kila awamu tunabadili salamu. Taifa lazima tuwe na salamu Moja kama alama yetu.

3. Hii salamu ya kazi iendelee haitikiwi na watu wote. Maana hii salamu inategemea na utendaji wa kazi wa serikali na jinsi mtu anaridhika na hiyo Kazi. Kama kazi hazitafanyika kiasi cha kuridhisha basi mtu hawezi kuitikia. Ila salamu ya Mungu wote twaitikia. Na wale wasio amini Mungu walishazoea.

Bwana Sifiwe, Asalamu Aleikumu
Kwani kusema Bwana Asifiwe nayo ni salamu?? Em tuweni serious kidogo jamani
 
Hapana lazima tuwe na salamu yenye kujenga uzalendo kwenye nchi yetu

Uzalendo umepotea sana tunaabudu nchi nyingine mfano maras watanzania wanavaa na kuitukuza bendera ya ethiopia, kuna wengine wanavaa bendera za marekani na cha ajabu siku za karibuni akina dada wana vaa bracelets zenye rangi na bendera ya kenya. Huo ni unyani (apedomia) kuacha kutukuza cha kwako unatukuza cha mtu mwingine. Hivyo salamu hii kwa sasa ni muhimu sana kwa taifa tulipokuwa rumefikia kila kiongozi au mtu alikuwa anaona salamu ya dini yake ni bora zaidi na kulazimisha kusalimia hata watu ambao imani hiyo hawaijui
Sisi wengine Mungu ni kwanza, vingine vinafuata...Kusalimiana kwa jina la Jamuhuri kiimani yangu ni kumweka Mungu chini ya Jamuhuri ambayo ni dhambi...Ndiyo sababu nikasema wapo ambao tunakwazwa!
 
Mimi nisingejali hata kama tungesema Asalamu aleykum ni sawa kwangu kuliko kwakua ndani yake kuna ibaada kwa Mungu wa ndugu zangu wa Tanzania.

Dhamira ya Mh. Mama na Rais wetu inaweza kuwa njema ila kwa bahati mbaya tafsiri yake kwa wengine kama sisi siyo nzuri. Ndiyo sababu tunali express hili waziwazi.
 
Napendekeza hii salamu ifutwe tumurudie Mungu. Sababu nyingine ni hizi hapa.

1. Salamu ya Mungu inaliinua taifa. Mungu anakuwa karibu nasi siku zote hata kipindi cha Corona.

2. Salamu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kazi iendelee inakosa consistency. Tutajikuta kila awamu tunabadili salamu. Taifa lazima tuwe na salamu Moja kama alama yetu.

3. Hii salamu ya kazi iendelee haitikiwi na watu wote. Maana hii salamu inategemea na utendaji wa kazi wa serikali na jinsi mtu anaridhika na hiyo Kazi. Kama kazi hazitafanyika kiasi cha kuridhisha basi mtu hawezi kuitikia. Ila salamu ya Mungu wote twaitikia. Na wale wasio amini Mungu walishazoea.

Bwana Sifiwe, Asalamu Aleikumu
Kumbuka kuwa kuna baadhi ya rais hawaamini mungu

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
 
Aseme tu ila itam cost maana watanzania wapiga kura zaidi ya 60% wanaamini katika Mungu na katu tusingependa kuongozwa na mtu asiyemwamini Mungu. Nchi yetu haina dini lakini watu wake ambao ndiyo waamuzi wana dini zao ambazo zinamtaja Mungu
 
Sisi wengine Mungu ni kwanza, vingine vinafuata...Kusalimiana kwa jina la Jamuhuri kiimani yangu ni kumweka Mungu chini ya Jamuhuri ambayo ni dhambi...Ndiyo sababu nikasema wapo ambao tunakwazwa!
Hakuna jinsi kama mtu unatumia akili na unaamini nchi yetu ina diversity kubwa ya kimila kiimani na kiitikadi. Ili kuondoa malalamiko kama hayo kwamba kpendelea.kumtaja Mungu wa dini yake ni bora ufanye hivyo. Kumbuka kila dini ina Mungu wake mwenye sifa tofauti na Mungu wa dini nyingine ndio maana tuna tofauti za kiibada.

Kusema aanze kusalimia kwa salamu.za.kidini kuna wahindi wana mungu wao na salamu zao nao ni watanzania

Kuna wapagani wana miungu yao nao ni watanzania wanaabudu mawe.miti wanyama nk

Kuna Wakristu na kuna Waislam kila mmoja ana yake. Ukitumia busara tuu atataja miungu wangapi? Na hata akitaja ataanza kupata upinzani kwa nini ameanza na salamu ya dini fulani na kuitaja dini nyingine mwisho, kuna imani nyingine nyingi kama marastafari huwa wanasahaulika hawatajwi na wao watalalamika. Kumbuka kwenye utaifa kila mtu ana haki nafursa sawa. Suala la salamu za kidini zibaki kwenye nyumba za ibada na baina ya watu wenye imani moja. Tungekuwa nchi nzima tuna imani moja basi isingekuwa tatizo. Hata hivyo hakuna mtu anayekwenda mbinguni kwa kusalimia salamu ya kidini. Kwenda mbinguni ni mchakato mkubwa wa kutenda mema kwa viumbe vyote alivyoviumba
 
Ni ushamba tu unakusumbua na mazoea mabaya, mungu hatukuzwi kwa salamu bali mungu anatukuzwa kwa matendo mema

Kuamini uwepo wa mungu sio kwa kusalimia bwana yesu asifiwe tu jinga wewe bali unashi maisha gani ya kukili uwepo na utii kwa mungu kwa matendo

Huyo aliye kuwa anasalimia kwa salamu dini zote alifanya kipi zaid ya kuteka na kuua na matusi ya jukwaani pamoja na kudhulumu haki za wengine? Acheni kuishi kwa kukalili.
Neno linasema ukimkiri YEYE kwa kinywa chako..Mungu hukaa katika sifa, unaanzaje kumsifu Mungu kama si kwa kinywa (kutamka)..matendo mema si lazima yamfurahishe dhalimu, Magufuli alitenda jwa wema si kwa kumfurahisha binadamu bali Mungu kwanza, machoni kibinadamu unaona alitenda vibaya, lkn mbele za Mungu alipata kibali kwa hayo alitenda!
Unaanzaje kusema jamhuri as if ndyo inakupa uzima..? IT IS WRONG!!
 
Hakuna jinsi kama mtu unatumia akili na unaamini nchi yetu ina diversity kubwa ya kimila kiimani na kiitikadi. Ili kuondoa malalamiko kama hayo kwamba kpendelea.kumtaja Mungu wa dini yake ni bora ufanye hivyo. Kumbuka kila dini ina Mungu wake mwenye sifa tofauti na Mungu wa dini nyingine ndio maana tuna tofauti za kiibada.

Kusema aanze kusalimia kwa salamu.za.kidini kuna wahindi wana mungu wao na salamu zao nao ni watanzania

Kuna wapagani wana miungu yao nao ni watanzania wanaabudu mawe.miti wanyama nk

Kuna Wakristu na kuna Waislam kila mmoja ana yake. Ukitumia busara tuu atataja miungu wangapi? Na hata akitaja ataanza kupata upinzani kwa nini ameanza na salamu ya dini fulani na kuitaja dini nyingine mwisho, kuna imani nyingine nyingi kama marastafari huwa wanasahaulika hawatajwi na wao watalalamika. Kumbuka kwenye utaifa kila mtu ana haki nafursa sawa. Suala la salamu za kidini zibaki kwenye nyumba za ibada na baina ya watu wenye imani moja. Tungekuwa nchi nzima tuna imani moja basi isingekuwa tatizo. Hata hivyo hakuna mtu anayekwenda mbinguni kwa kusalimia salamu ya kidini. Kwenda mbinguni ni mchakato mkubwa wa kutenda mema kwa viumbe vyote alivyoviumba
Wimbo wa taifa unapomtaja Mungu huwa ni Mungu yupi? wapi anatajwa mungu wa wapagani au hao wahindi? Kwako wewe ni muhimu sana kumfurahisha binadamu kuliko aliyekuumba wewe na huyo unayetaka kumfurahisha? akikunyima hewa ya bure inayokupa uhai kwa dk 10 huyo jamhuri atakupa? tusitetee mambo ya upotofu!
 
  • Thanks
Reactions: Ame

Kwahiyo Mungu tunayemtaja tukiimba wimbo wa taifa ni wa akina nani? Kuna common denominator hapo...Watanzania wame evolve na wana culture yao, miaka 60 uje utuambie kila mtu ana Mungu wake hiyo siyo fair kabisa....Narudia dhamira ilikuwa njema ila is against the common understanding of most of us
 
Umewaza kama mimi. Kuna vitu havina utetezi maana vinazuiwa na historia kuwa jinsi mtu apendavyo
 
Kwahiyo Mungu tunayemtaja tukiimba wimbo wa taifa ni wa akina nani? Kuna common denominator hapo...Watanzania wame evolve na wana culture yao, miaka 60 uje utuambie kila mtu ana Mungu wake hiyo siyo fair kabisa....Narudia dhamira ilikuwa njema ila is against the common understanding of most of us
Mimi nakubaliana na wewe na mpaka ameweka hivyo kuna tafakari ya kina ameifanya. Umeongea wimbo wa Taifa unataja neno Mungu ibariki hilo halina utata maana kila mmoja atatohoa kwa Mungu wake

Linapo kuja kwenye salamu kila dini ina mfumo wake ambao ni kikwazo au haukubaliki kwenye upande mwingine hata utatafsiri maana ya maneno yanayotumika kuwa ni mazuri kiasi gani lkn kwa kuwa yanatumiwa na imani fulani basi mtu wa imani nyingine anakwazika inapotumika kwenye halaiki

Togauti na hapo utumie kama nusu saa kuanza kusalimia kwa dini tofauti tofauti na hata ukifanya hivyo kuna zile dini ndogondogo huwa hawazitaji na kwao kuona kuwa wanabaguliwa.Hata ukiweza kukumbuka zote bado utakutana na changamoto ya kuwa kwa nini katika kutaja salamu za kidini kaanza na salamu fulani na nyingine kaiweka ya mwisho.

Nadhani, kama una busara za kutosha utaielewa nia yake ya dhati akiwa kama kiongozi mkuu wa nchi tofauti kabisa yenye diversity tofauti za kiimani na kimila na kila moja anatakiwa aheshimiwe bila kujali udogo wake au ukubwa wake
 
Wewe kwako kumheshimu binadamu ni bora kuliko kumheshimu Mungu?
Kuanza na salamu..Amani iwe kwenu au tumsifu Yesu Kristu kwa kutuweka hapa leo..au kusema Bwana Yesu asifiwe..huo ni mfumo??? Mfumo ni nn..au tunaandika tu maneno bila hata kujua maana yake! Mungu anayetajwa kwenye wimbo wa taifa ni wa watu gani tofauti na anayetajwa kwenye salamu..!
Maana ya salamu hizo ni kukiri kwamba tupo hapo kwa sababu ya rehema tu za huyo aliye Mkuu kupita vyote!!!!
Unapotanguliza jamhuri, yeye ndiye anakuweka hapo?
 
Kwa hiyo unaamini watanzania tupo katika hayo makundi mawili ya ASSALAM ALAYKUM na BWANA YESU ASIFIWE/ TUMSIFU YESU KRISTU? kama kuna makundi mengine ( najua Tanzania yapo mengi sana tofauti na hayo) Hata kama machache kwa kutowatambua tayari umeleta matabaka na manunguniko

Unaweza kulazimisha kulitaja jina l Mungu sehemu ambayo wana imani tofauti badala ya jina hilo kutukuzwa watu wakawa wanalalamika na wengine kuongea vibaya

Kitu sahihi na kutumia salamu isiyokuwa na itikadi yoyote ambayo kila mmoja inamgusa sawa. Mungu anaijua nia ya dhatinya mtu hivyo hakuna baya lolote cha msingi tenda mema kwa binadamu mwenzako bila kujali itikadi yake basi hapo utahesabiwa haki haitoshi tuu kulitaja jina lakn tukifanya mambo yasiyofaa
 
Mimi nakubaliana na wewe na mpaka ameweka hivyo kuna tafakari ya kina ameifanya.
Una uhakika ya tafakari kufanyika! Mbona hili wala halihitaji tafakari..jina la jamhuri ndyo kitu gani zaidi ya kumtaja aliyekuumba na anakupa hewa ya bure 24 hrs..
Mbona mambo mengine hiyo hofu ya kutokwaza wengine haionekani?? watu wmelalamikia tozo tena kwa sauti kubwa lkn bado zipo..hofu ya kutomtaja Mungu kuogopa kukwaza wapagani kwenye tozo hofu imeenda wapi..
 
Kwa hiyo unaamini watanzania tupo katika hayo makundi mawili ya ASSALAM ALAYKUM na BWANA YESU ASIFIWE/ TUMSIFU YESU KRISTU? kama kuna makundi mengine ( najua Tanzania yapo mengi sana tofauti na hayo) Hata kama machache kwa kutowatambua tayari umeleta matabaka na manunguniko

Unaweza kulazimisha kulitaja jina l Mungu sehemu ambayo wana imani tofauti badala ya jina hilo kutukuzwa watu wakawa wanalalamika na wengine kuongea vibaya

Kitu sahihi na kutumia salamu isiyokuwa na itikadi yoyote ambayo kila mmoja inamgusa sawa. Mungu anaijua nia ya dhatinya mtu hivyo hakuna baya lolote cha msingi tenda mema kwa binadamu mwenzako bila kujali itikadi yake basi hapo utahesabiwa haki haitoshi tuu kulitaja jina lakn tukifanya mambo yasiyofaa
Mungu wa kwenye wimbo wa taifa ni wa kundi gani?
Wewe unaogopa matabaka kuliko aliyekuumba?
 
Tungekuwa na salamu moja inayotaja Mungu tu ambaye ni common kwa wote asingekuwa shida.

Mathalani unapoimbwa wimbo wa taifa kila mmoja anatafsiri Mungu wa Imani yake. Kwa mfano huu wimbo ungekuwa unatamka Jina la Yesu aliyepo kwenye salamu yao ungekuwa unaimbika kwa waislam, na Je! Ungekuwa unatumia maneno ya kiarabu yanaoonekana kwenye salamu ya waislam hata kama yanatafsiri nzuri vipi yangeeleweka kwa wakristu?

Kama ni mtu aliyesoma diversity na kujua namna nzuri ya kuishi kwenye harmony na watu wenye itikadi tofauti utanielewa lakini kama ni mtu bold unayeamini kuwa unachokiamini wewe kipo sahihi sana na yafaa watu wote wakifuate hatutakubalianza na wewe

Zaidi ya hapo nchi yetu ina mchanganyiko mkubwa wa kiimani na jibu la pamoj halitkuwepo maana kila mtu chake ni bora hata kama wewe unakiona kibaya zaidi

Kwa msaada zaidi waweza kusoma Sura Al - kafirun 109 , 1-6 jibu lilishatolewa na imetumika busara kubwa kwenye hili ili kuepuka mkangajiko maana kwenye nchi yetu huwezi kusalimia salamu yoyoyote ya Kumtaja Mungu bila kutumia salamu za dini hizi mbili. Nukta
 
Napendekeza hii salamu ifutwe tumurudie Mungu. Sababu nyingine ni hizi hapa.

1. Salamu ya Mungu inaliinua taifa. Mungu anakuwa karibu nasi siku zote hata kipindi cha Corona.

2. Salamu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kazi iendelee inakosa consistency. Tutajikuta kila awamu tunabadili salamu. Taifa lazima tuwe na salamu Moja kama alama yetu.

3. Hii salamu ya kazi iendelee haitikiwi na watu wote. Maana hii salamu inategemea na utendaji wa kazi wa serikali na jinsi mtu anaridhika na hiyo Kazi. Kama kazi hazitafanyika kiasi cha kuridhisha basi mtu hawezi kuitikia. Ila salamu ya Mungu wote twaitikia. Na wale wasio amini Mungu walishazoea.

Bwana Sifiwe, Asalamu Aleikumu
Mungu hana salam period.

Bali kuna salam za Amani.

Else tupatie dalili kuwa hizo ni salami za mungu.
 
Kinachompa tabu mama yenu ni kusema Bwana Asifiwe. Anaona atageuka mkristo
Bwana asifiwe ndiyo salamu ya wapi? Hata Wakatoliki wa Tanzania ambao ndiyo dhehebu RASMI la kikristo hawaitambui!!

Muacheni Rais SSH na salamu ambayo ni secular
 
Napendekeza hii salamu ifutwe tumurudie Mungu. Sababu nyingine ni hizi hapa.

1. Salamu ya Mungu inaliinua taifa. Mungu anakuwa karibu nasi siku zote hata kipindi cha Corona.

2. Salamu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kazi iendelee inakosa consistency. Tutajikuta kila awamu tunabadili salamu. Taifa lazima tuwe na salamu Moja kama alama yetu.

3. Hii salamu ya kazi iendelee haitikiwi na watu wote. Maana hii salamu inategemea na utendaji wa kazi wa serikali na jinsi mtu anaridhika na hiyo Kazi. Kama kazi hazitafanyika kiasi cha kuridhisha basi mtu hawezi kuitikia. Ila salamu ya Mungu wote twaitikia. Na wale wasio amini Mungu walishazoea.

Bwana Sifiwe, Asalamu Aleikumu
Nongwa tupu 😝😝
 
Tungekuwa na salamu moja inayotaja Mungu tu ambaye ni common kwa wote asingekuwa shida.

Mathalani unapoimbwa wimbo wa taifa kila mmoja anatafsiri Mungu wa Imani yake. Kwa mfano huu wimbo ungekuwa unatamka Jina la Yesu aliyepo kwenye salamu yao ungekuwa unaimbika kwa waislam, na Je! Ungekuwa unatumia maneno ya kiarabu yanaoonekana kwenye salamu ya waislam hata kama yanatafsiri nzuri vipi yangeeleweka kwa wakristu?

Kama ni mtu aliyesoma diversity na kujua namna nzuri ya kuishi kwenye harmony na watu wenye itikadi tofauti utanielewa lakini kama ni mtu bold unayeamini kuwa unachokiamini wewe kipo sahihi sana na yafaa watu wote wakifuate hatutakubalianza na wewe

Zaidi ya hapo nchi yetu ina mchanganyiko mkubwa wa kiimani na jibu la pamoj halitkuwepo maana kila mtu chake ni bora hata kama wewe unakiona kibaya zaidi

Kwa msaada zaidi waweza kusoma Sura Al - kafirun 109 , 1-6 jibu lilishatolewa na imetumika busara kubwa kwenye hili ili kuepuka mkangajiko maana kwenye nchi yetu huwezi kusalimia salamu yoyoyote ya Kumtaja Mungu bila kutumia salamu za dini hizi mbili. Nukta
Salamu hizo tatu ni za kawaida zinatumiwa kila siku kwa makundi yote mchanganyiko, sababu ya kuzitumia kwenye mikutano ni vile waliopo kwenye mkutano wengi ni wale wanatumia salamu hizi wao kwa wao kila siku, si jambo geni kwao, kama salamu ya Tumsifu Yesu Kristu haikuhusu itatajwa inayokuhusu...Lakini ZOTE zinaonyesha kutambua uwezo wa MMOJA mwenye nguvu na mamlaka kuliko vitu vyote iwe juu iwe chini hapa tulipo. Si kila unachosoma kina mantiki kwa jamii, shule nzr ya kuishi kwa amani na jamii inayokuzunguka ni malezi anayopata mtu na hasa kati ya miaka 0-18 Kiongozi anapaswa kuvuka kiwango cha kudhani anawajibika kuwapendeza binadamu wote..sifa kuu ya siyo tu kiongozi mtu yeyote ni kuwa na hofu na yule aliyetuumba wote including hao wasiomjua kama yupo, wewe unayefahamu kuwa yupo onyesha kwa kauli na matendo kuwa yupo, ni faida kwa wanaodhani walijikuta tu wapo duniani pengine kupitia maneno unayotamka itawasaidia kufahamu kama wewe..uongozi ni kielelezo hasa cha mazuri!
 
Back
Top Bottom