Anna Makinda: Magufuli ni Siri ya Mungu na atakayempinga atashindwa Uchaguzi ndio sababu Rais Samia anasema " Kazi Iendelee"

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
84,035
142,141
Spika mstaafu mama Makinda amesema Ujio wa Hayati Magufuli kama Rais wa JMT ni Siri ya Mungu na hata sasa ameungana na Hayati baba wa taifa Mwalimu Nyerere huko Peponi.

Makinda amesema Magufuli amekamilisha miradi yote Kuanzia ile ya 1960 ambayo ilimshinda hata Mwalimu Nyerere

Makinda amesema Mgombea yoyote atakayempinga Magufuli atashindwa Uchaguzi na ndio sababu hata Kauli mbiu ya Rais Samia inasema Kazi Iendelee alimaanisha Kazi iliyoanzishwa na Hayati Magufuli

Mama Makinda amesema hayo jijini Mwanza Katika Misa ya kumkumbuka Magufuli ambapo akihudhuria kama muumini wa kawaida

Source: Ayo tv
 
Hivi hawa wanasiasa hawajuagi kutudanganya ni mwisho duniani?hayo mambo ya kuwatabiria pepo watu ni magumu sana.

Wako waliotabiliwa pepo na wakaitwa watu wa peponi huku wangali hai, lakini sio kizazi cha sasa kilichojaa wizi,uporaji,uuaji utekaji na dhuruma kama kina Magufuri
 
Huo ndo ukweli, hata chadema walipokuja mwanza hawakuthubutu kumuongelea vibaya JPM,

Amini nawaambieni chama chochote chenye mpango wa kupata wabunge wengi hakitamuongelea vibaya Jpm kwenye uchaguzi, Jpm yupo kwenye mioyo ya wapiga kura sio wapiga kelele.
 
Umuongelee vibaya mtu wao wakati hawajasoma wengi wa watu wa Kanda hiyo
 
Acha utoto wewe, walimkosoa sana tu JPM Kwa kuendeleza chato na kuisahau maeneo mengine ya Kanda ya ziwa!!

Unadai hakuna chama kitashinda wabunge kikimtukana JPM? Sasa CCM ya Samia Inamkashifu Kila siku JPM, Chadema pia Inamkashifu!! ACT pia nj hivyo hivyo!! Sasa unataka kusema wabunge watatokea CHAUMMA na NCCR?

Magufuli angekua na chama chake hapo ungekua na hoja ila Kwa Sasa vyama vikubwa ni viwili na vyote havimtaki JPM so sielewi unaposema havitopata wabunge je nani atapata?
 
Mi nikajua hawa wajinga ambao hawajasoma ndo rahisi kuwadanganya habari za Udikteta na wizi, kama hao wamewashinda basi muungane na Honey Badger asali bado ipo ya kutosha.
 
Hakuna chama chenye uwezo wa kupambana na marehemu JPM. Miaka miwili sasa ila bado wanatapatapa kuwaingia wapiga kura.

Sio ccm wala cdm wote 2025 wataufyata. JPM ndiye kipimo cha uongozi ndani ya miaka 20-30 ijayo
 
Wizi ni kwel ndo maana alimtoa assad .kuelezea mambo complex ya kihasibu kwa watu wavuvi wa sangara ni kaz
 
Hakuna chama chenye uwezo wa kupambana na marehemu JPM. Miaka miwili sasa ila bado wanatapatapa kuwaingia wapiga kura.

Sio ccm wala cdm wote 2025 wataufyata. JPM ndiye kipimo cha uongozi ndani ya miaka 20-30 ijayo
Jibu swali Samia na Mbowe wote wanamtukana JPM je unataka kusema Chadema na CCM hawatopata wabunge 2025?? Mnachekesha.
 
Back
Top Bottom