Maonesho ya Uagizaji na Mauzo ya Nje ya China ni mfano wa kunufaishana kati ya China na dunia

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,032
1,051
1713938839297.png


Maonyesho ya 135 ya Uagizaji na Uuzaji wa Bidhaa ya China, maarufu kama ‘Canton Fair,’ yameanza tarehe 15 mwezi April mjini Guangzhou, mkoa wa Guandong, hapa China. Katika maonyesho ya mwaka jana, idadi kubwa ya kampuni zilishiriki, na mwaka huu, idadi hiyo imeongezeka tena kwa kiasi kikubwa, ikiwa na jumla ya kampuni 29,000 zinazoshiriki, na kufanya maonesho hayo kuendelea kuwa maarufu mwaka hadi mwaka.

Kwa mujibu wa takwimu za vyombo vya habari, saa moja kabla ya maonyesho hayo kuanza rasmi, Zaidi ya wanunuzi 20,000 waliwasili, na asilimia 40 kati yao ni wateja wapya. Licha ya mvutano unaoendelea katika Mashariki ya Kati na kusababisha wasiwasi katika soko la dunia, ufunguzi mkubwa na wa mafanikio wa Canton Fair hakika unaleta uhakika katika biashara duniani.

Maonyesho ya mwaka huu yenye kaulimbiu ya “Maendeleo ya Ubora wa Juu, Kuimarisha Ngazi ya Juu ya Ufunguaji Mlango,” yanafanyika kwa awamu tatu nje ya mtandao. Kama kipimo na ramani ya biashara ya nje ya China, jamii ya kimataifa kwanza inachukulia nguvu na dhamira ya maendeleo ya China kupitia maonyesho hayo. Tangu mwaka 1957, maonyesho hayo yamekuwa yakifanyika mara mbili kwa mwaka bila kukosa, tukio ambalo ni la kipelee kati ya nchi kubwa duniani.

Hivi sasa, maonyesho haya yamekua kutoka dirisha la sekta ya uzalishaji ya China na kuwa jukwaa la uzalishaji duniani. Awamu ya kwanza ya maonyesho haya, yenye kaulimbiu ya “Uzalishaji wa Kisasa,” inaunga mkono maendeleo ya teknolojia na uzalishaji, na kuonyesha nguvu bora mpya za uzalishaji.

Kwa baadhi ya nchi za Magharibi, China imekuwa ikishutumiwa kwa kuuza bidhaa za ziada za ubora wa chini duniani, kuzuia eneo la ukuaji kwa nchi nyingine, na kufaidika na kitendo hicho. Lakini, kila anayetembelea maonyesho ya Canton na kuangalia kwa makini anaweza kuelewa kwa urahisi kwa nini watu wengi wanapenda kufanya biashara na China.

Tukichukulia Maonyesho ya mwaka huu kwa mfano, idadi ya wafanyabiashara wakubwa na kampuni kutoka nchi na sehemu mbalimbali duniani imeongezeka kidhahiri, miongoni mwao ni kampuni kama Walmart, Best Buy, na Amazon kutoka Marekani, Auchan, Carrefout na Shneider kutoka Ufaransa, na Tesco kutoka Uingereza. Kama kampuni hizi zikishirikiana na China na kutoa taswira ya China, itakuwa ni tofauti kabisa na ile inayotolewa na “washambuliaji wa mtandaoni” ambao hawajahi hata kufika China. Ikilinganishwa na matarajio yao, makubaliano yanayofikiwa katika Maonyesho ya Canton yanapaswa kuwa ni ishara ya kuaminika ya uchumi wa China.

Maonyesho ya Canton yamefungua mlango wa mafanikio ya pamoja kati ya dunia na China, na bila shaka yamefanikiwa sana katika nyanja zote. Inatarajiwa kuwa thamani ya biashara katika maonyesho ya mwaka huu itaongezeka kidhahiri, na huu si tu ni mtazamo wa ndani, lakini pia ni matokeo yasiyopingika ya hali ya sasa ya siasa na uchumi wa dunia.

Katika mageuzi ya mfumo wa kiviwanda duniani, ni rahisi kuona kuwa China ina nguvu kubwa ya uongozi katika kuboresha na kubadili uchumi wake. Kwa dunia, hususan katika hali ya sasa ya migogoro na mivutano, maonyesho kama haya ya kimataifa yenye fursa nyingi, matokeo mazuri ya biashara, na hadhi kubwa, pua ni bidhaa muhimu ya umma inayotolewa na China.

Kwa jinsi hali ya sintofahamu inavyoendelea duniani kwa sasa, ndivyo umaalum na thamani ya maonyesho haya ya biashara inavyokuwa.

Tunayatakia maonyesho haya kila la heri!
 
Back
Top Bottom