Nawachukia "wageni" wa JF!

Nawachukia "wageni" wa JF!

Kigarama

JF-Expert Member
Joined
Apr 23, 2007
Posts
2,492
Reaction score
1,242
Kwanza kabisa naomba nisionekane mimi sina mila ya Kiafrika ya Kupenda wageni, kwa kweli mimi napenda sana wageni tena sana, lakini wageni wa JF wanaboa bwana. Utakuta mada iko juu mpaka inapitiliza lakini memba wako 200 wageni wako 500, sasa hawa wageni si watafute njia na wao wawe memba ili michango yao ijulikane? Huu ugeni unaozidi idadi ya wenyeji unanitia shaka!!
 
acha chuki binafsi wewe HUWEZI KUWA MWENYEJI BILA KUWA MGENI hata sisi nasisitiza sisi wenyeji tulikua wageni pia nasasa tumekua wenyeji
 
Akili ni nywele mwenzetu sijui umenyoa?wewe haukuanza kama mgeni!ubinafsi tu unakusumbua hauna maana jamii forum sio ya baba au mama yako.
 
Kuna 59,104 members lakini unakuta walio active each and everyday ni around 7,000 na 9,000. So ukiona guest wanahesitate kujiunga labda anaona atakuwa inactive so haitakua na maana. Kama vipi ungeanza kuchukia members ambao wako inactive!
 
acha chuki binafsi wewe HUWEZI KUWA MWENYEJI BILA KUWA MGENI hata sisi nasisitiza sisi wenyeji tulikua wageni pia nasasa tumekua wenyeji
Dada malaika sisemi kusiwe na wageni lakini wageni wanapokuwa wengi kuliko wenyeji huoni ni kama kuzavezana fulani hivi. Kuna mtu kasema baadhi ya "wageni" ni wenyeji ila wanakuwa anakula chabo kwanza kabla ya kuingia.lakini katika kundi hili wenye identity zaidi ya moja!!
 
Mkuu Kigarama.
Unadhani wageni ni wengi hakuna kitu wale "wageni" ni wenyeji..

JF kuna members zaidi 59.000.

Multiple ID's zipo zaidi ya 11.000 kwa mujibu wa Mtumishi.

Na kuna Maltiple ID's zingine azieleweki kutoka kwenye Internet Cafe za bongo.

Kwa hiyo wale ni wenyeji Mkuu wanatizama kwanza kuna mada gani kabla hawajavamia thread.
 
Mimi nimesoma maoni yooote kuanzia juu mpk chini lkn sijaelewa kama mgeni anawezaje kuchangia mada. Au huyu ndugu yetu anamaanisha nini?
 
Kwani wewe ukifungua JF unakimbilia kusaini in au unacheki upepo kwanza?
 
mkuu usiwe na hasira,wengi wa hao wageni ni real members lakini wanataka kusoma mada wakiwa nje'mimi nawaona wapo smart kuliko unavyofikiri kwa sababu wanaonekana ni watu wasio na haraka'wengine ndio hao wakina mkweree na serikali yake'wanataka kuona kuna nini kipya hapa jf
 
pia wengi wao ni wale ambao wameajiriwa na watu special tu kwakujua wotz in this forum,kuna skendo gani na lipi limejiri juu yao
 
Kwani wewe mleta mada ukiingia JF automatically huwa computer yako inaku log in instantly ama unachukua average ya 60 seconds hivi kulog in? Kwa muda huo si nawe unakuwa mgeni? Hata hivyo kwanini ulazimishe wote wawe memba? Interest yako ni nini?
 
Wengi huwa tunasoma kama guests, tukivutiwa na mada ndio tuna"log in". Kwa hiyo sio unapoona guests usidhani ni guests.....
 
Kwani wewe ukifungua JF unakimbilia kusaini in au unacheki upepo kwanza?
mimi huwa nikifungua naingia mazima, kazi yangu moja tu, kumtafuta pumpkin head leo kasema nini!!!
Wamjua Pumpkin head wewe??
 
Wa wale wasiochangi jf hata mwaka mmoja kama wewe unawaweka kundi gani.
 
sio kila mgeni sio memba wa jf ila kuna kipindi mtu unaogopa kulog in kutokana na mazingira uliyopo ndio maana unaingia kama guest.Nalog off
 
Kigarama umewaza nini dear? Mie naona ni vizuri kua there are people watching out there.... Kuna several members wameshawahi admit walijiunga baada ya kua guests, wakavutiwa na kujiunga.... Even a baby starts by crawling before standing and eventually walking.... Usiwachukie hivo bana.

Na kama members wengine walivokuambia... Mwingine aingia kama guest kusoma upepo then alog in.
 
Back
Top Bottom