Natoa wito Agosti 23 tujitokeze kwa wingi kuhesabiwa

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,498
113,605
National Bureau of Statistics

Tanzania Census 2022
Maandalizi ya Sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 Yamekamilika, Kazi Iliyobaki ni Moja Tuu, Tujitokeze kwa Wingi kwa Kujituliza, Tuhesabiwe!

Utangulizi

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imepanga kufanya Sensa ya Watu na Makazi ifikapo tarehe 23, mwezi Agosti 2022. Wizara ya Fedha na Mipango kupitia Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) kwa kushirikiana na Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali Zanzibar (OCGS), ambapo sasa maandalizi yote ya kufanya Sensa hiyo. Sensa ya Watu na Makazi yamekamilika Kwa asilimia 💯% Kwa 💯% kwa zoezi hili la kitaifa linalofanyika kila baada ya miaka 10 ambapo Sensa ya mwisho kufanyika nchini ni ile ya mwaka 2012. Hivyo Sensa ya mwaka 2022 itakuwa ni sensa ya Sita kufanyika nchini baada ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar mwaka 1964. Sensa nyingine zilifanyika mwaka 1967, 1978, 1988, 2002 na 2012.

Maana ya Sensa ya Watu na Makazi
Sensa ya watu na makazi ni utaratibu wa kukusanya, kuchambua, kutathimini na kuchapisha na kusambaza takwimu za kidemographia, kiuchumi na kijamii kuhusiana na watu wote na makazi yao katika nchi kwa kipindi maalum. Kwa maana nyingine, sensa ni zoezi maalum lenye lengo la kupata idadi ya watu wote katika nchi, kwa umri na jinsia, mahali wanapoishi na hali yao ya elimu, hali ya ajira, hali ya vizazi na vifo na hali ya makazi. Takwimu hizi za msingi ndiyo zinazoweza kuanisha mahitaji halisi ya wananchi yakiwemo makundi maalum yenye uhitaji maalum kwa mfano, watu wenye ulemavu, wanawake, watoto, vijana na wazee hivyo kurahisisha uandaaji wa sera na mipango ya maendeleo kulingana na uhitaji na mazingira yaliyopo.

Umuhimu wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022
Umuhimu wa kipekee wa Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 ni pamoja na:-
  1. Kuisadia Serikali kupata taarifa za msingi zitakazosaidia mchakato wa utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya mwaka 2025, mageuzi ya masuala ya afya na jamii, pamoja na ufuatiliaji wa ajenda za maendeleo za kimataifa;
  2. Taarifa za idadi ya watu husaidia katika mamlaka za wilaya katika utekelezaji wa mipango ya maendeleo ambayo huakisi matakwa ya watu katika ngazi husika na kusaidia kwenye uwiano wa mgawanyo wa rasilimali;
  3. Taarifa za msingi za hali ya kidemografia, kijamii na kiuchumi za idadi ya watu na makazi za mipango katika ngazi zote;
  4. Kigawio katika kukokotoa viashiria vingine mfano Pato la mtu mmoja mmoja, Pato la Taifa, Ajira na ukosefu wa Ajira na kiwango cha uandikishaji wa wanafunzi;
  5. Taarifa itakayowezesha serikali kujua ongezeko la idadi ya watu, kwa mgawanyo na viashiria vingine, ambavyo ni muhimu kwa usimamizi wa mazingira; na
  6. Msingi wa utawala bora na ujumuishaji wa demokrasia. Takwimu sahihi za Sensa zinahitajika kwa ajili ya ugawaji wa majimbo ya uchaguzi kwa ufanisi, kurekebisha mipaka ya kiutawala katika serikali za mitaa.
Madodoso ya Sensa
Sensa ya mwaka 2022 kama zilivyo sensa zilizopita itatumia aina mbili kuu za madodoso. Dodoso refu litakalotumika kuhoji asilimia 30 ya maeneo yote ya kuhesabia watu na Dodoso fupi litakalotumika kuhoji kwenye asilimia 70 ya maeneo yote ya kuhesabia watu.
Madodoso Mengine ni:-
  • Dodoso la Taasisi ambalo ni mahsusi kwa ajili ya wasafiri, waliolala mahotelini/nyumba za wageni, na waliolazwa hospitalini; na
  • Dodoso la Wasio na Makazi maalum ambalo ni mahsusi kwa watu wote wanaolala maeneo yasiyo rasmi, kwenye baraza za majengo mbalimbali, kwenye madaraja na maeneo mengine.
Maandalizi yote ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 yamekamilika Kwa asilimia 💯%
Kwa 💯%

Utekelezaji wa sensa ya watu na makazi hufanyika katika awamu kuu tatu kuu ambazo ni Kipindi Kabla ya Kuhesabu Watu, Wakati wa Kuhesabu Watu na Kipindi Baada ya Kuhesabu Watu.

Kipindi Kabla ya Kuhesabu Watu
Kipindi kabla ya kuhesabu watu kinajumuisha Uandaaji wa Kitabu cha Mkakati wa Usimamizi na Utekelezaji wa Sensa na nyaraka nyingine, Utengaji wa Maeneo ya Kuhesabia Watu na Uzalishaji wa Ramani, Uandaaji wa Nyenzo (Madodoso na Miongozo mbalimbali); Uhamasishaji, Sensa ya Majaribio ifikapo tarehe 29 Agosti 2021 ikiwa ni mwaka mmoja kamili kabla ya Sensa yenyewe; Kuunda kamati za sensa; kufanya mikutano na wadau wa takwimu; kufanya manunuzi, kufanya uchaguzi wa aina ya teknolojia itakayotumika, kuajiri wadadisi na wasimamizi, usambazaji wa vifaa; na kufanya maandalizi ya Tathmini ya Sensa.

Kipindi cha Kuhesabu Watu
Kipindi cha kuhesabu watu kinajumuisha kazi kuu na ya muhimu katika zoezi hili ya kuhesabu watu.

Kipindi Baada ya Kuhesabu Watu
Kipindi baada ya kuhesabu watu kinajumuisha Uchakataji wa Taarifa za Sensa, Uchambuzi, Utoaji wa Matokeo ya Awali, Usambazaji wa matokeo ya mwisho, uhamasishaji wa matumizi ya takwimu kwa watumishi wa Wizara, Idara na Taasisi za Serikali.

Maandalizi ya sensa ya watu na makazi 2022 yalianza 2018, ikiwa ni kutenga maeneo ya kuhesabia watu, kutayarisha nyaraka muhimu za sensa kama vile madodoso, miongozo, fomu za kudhibiti ubora na kufanya sensa ya majaribio.

Kwa sasa maandalizi ya sensa yamekamilika, imebaki kazi moja tuu, ya watu kujitokeza kwa wingi hiyo tarehe 23 Agosti kwa Kujituliza katika makazi yao na kumsubiria karani wa sensa atapita na kuhesabiwa.
  1. Kitabu cha Mkakati wa Usimamizi na Utekelezaji wa Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 kimekamilika.
  2. Kutenga Maeneo ya sensa Kwa wilaya zote za mkoa yote Tanzania nzima zimekamilika
  3. Ziara za kimafunzo nchini na nje ya nchi kwa ufadhili wa UNFPA kwa ambao wamefanya sensa ya kidigitali hivi karibuni na kujifunza matumizi ya teknolojia ya kisasa katika kufanya sensa kwa mafanikio. Matumizi ya teknolojia hii itasaidia kupunguza gharama za kufanya sensa na kupunguza muda wa kutoa matokeo ya sensa, zimekamilika
  4. Dodoso la Sensa na nyaraka nyingine muhimu kama vile miongozo ya kufundishia, miongozo ya makarani wa sensa, miongozo ya wasimamizi wa sensa na miongozo ya waratibu wa sensa mkoa na wilaya, imekamilika, semina za mafunzo kwa mikutano, warsha na makongamano, zimefanyika na kukamilika.
Maswali Yatakayoulizwa katika Sensa ya mwaka 2022
Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022 ina moduli kumi na nne ambazo zitatumika kukusanya taarifa za watu na makazi yao nchi nzima.

Maswali yatakayoulizwa yatahusu:-
  1. Taarifa za kidemografia (umri, jinsi, uhusiano, hali ya ndoa, uraia, n.k.);
  2. Maswali yanayohusu ulemavu;
  3. Taarifa za Elimu;
  4. Maswali ya uhamaji, pamoja na taarifa za Watanzania wanaoishi nje ya nchi
  5. Maswali kuhusu umiliki wa nyaraka za kitaifa (vitambulisho vya NIDA, Mzanzibari mkazi, cheti cha kuzaliwa, hati ya kusafiria, na leseni ya udereva)
  6. Shughuli za kiuchumi
  7. Umiliki wa ardhi na taarifa za TEHAMA
  8. Taarifa za Uzazi na Vifo vilivyotokea ndani ya kaya
  9. Vifo vitokanavyo na uzazi
  10. Hali ya nyumba za kuishi na umiliki wa rasilimali mbalimbali
  11. Maswali ya kilimo na mifugo
  12. Mifuko ya hifadhi ya jamii.
Tofauti ya Sensa ya Mwaka 2022 na Sensa zilizopita:-
Katika sensa ya mwaka 2022 inatarajiwa kuwa na vitu vipya kama vile;
  • Kutenga maeneo ya kijiografia ya kuhesabia watu katika ngazi za kitongoji/mtaa na upatikanaji wa taarifa za kitakwimu katika ngazi za kitongoji/mtaa pamoja na kuwa na mipaka ya kudumu katika ngazi hizo;
  • Matumizi ya Vishikwambi (tablets) katika hatua zote za utekelezaji wa sensa kwa lengo la kupunguza gharama;
  • Nyongeza ya maswali yatakayowezesha upatikanaji wa taarifa zaidi za kitakwimu ikilinganishwa na Sensa ya Mwaka 2012:-
  1. Taarifa za kidemografia (umri wakati wa ndoa ya kwanza);
  2. Maswali yanayohusu ulemavu (Kichwa kikubwa, Mgongo wazi, Kifafa/Epilepsy, Mbalanga/storiasis na Usonji/autism);
  3. Maswali ya uhamaji kulingana na mapendekezo ya IOM (International Organization of Migration);
  4. Maswali kuhusu umiliki wa nyaraka za kitaifa (vitambulisho NIDA, vitambulisho vya wafanyabiashara wadogo wadogo, Mzanzibari mkazi, hati ya kusafiria, na leseni ya udereva);
  5. Maboresho ya maswali ya shughuli za kiuchumi ikiwa ni pamoja na idadi ya kaya ziliko kwenye sekta isiyo rasmi;
  6. Umiliki wa ardhi na taarifa za TEHAMA
  • Takwimu za nyumba (orodha, hali ya umiliki na aina ya nyumba)
  • Maswali ya kilimo na mifugo
My Take
It's very unfortunately kwenye hojaji za sensa, hakuna swali lolote kuhusu idadi ya Watanzania wanaoishi kwa kuitegemea ile ajira ya "the oldest professional" inayoongoza kuajiri watu wengi zaidi duniani kuliko ajira nyingine yoyote!.

Hata serikali yetu haiamini kuwa ile ni kazi halali, lakini ipo na inafanyika na ndio imeajiri idadi kubwa kabisa ya watu kuliko ajira nyingine yoyote! inafanyika kwa aina 3.

1. Watu wenye bahati zao, hawa wameajiriwa rasmi full time wengine formally kwa kulipiwa mahari na Huduma zao kununuliwa kwa bei ya jumla na mteja mmoja kumiliki jumla kwa kuandikisha na kupata hati miliki, au wengine ni kuchukuana tuu au kukubaliana lakini Huduma hizo zinakuwa ni kwa mteja mmoja.

2. Watu wenye bahati zao kumpata mteja mmoja wa kununua jumla, ile uwezo wa mteja huyo mmoja hautoshelezi mahitaji yote ya mhusika hivyo mhusika kujikuta analazimika licha ya kuuza jumla, pia inambidi auze na rejareja kufidia nakisi.

3. Wale wasio na bahati ya kumpata mteja mmoja wa kununua jumla, hivyo kuwajibika kuuza reja reja kwa mteja zaidi ya mmoja.

4. Kuna kundi kubwa la watu ambao wana kazi zao lakini bado wanafanya part time ya professional hii.
Serikali yetu ilipaswa ijue data za idadi ya hawa watu wate, wale wenye bahati walioajiriwa rasmi full time, ndio pekee data zao zitakusanywa na wengine wote hazikusanywi!, laiti serikali ingekusanya ikajua tuu idadi, na sio lazima kuirasimisha biashara hii, ila ingejulikana na kurasimishwa ungefanyika in a decent manner na hata serikali ingekusanya kodi ya maana tuu!.

Hitimisho
Ofisi Taifa ya Takwimu, imejipanga vizuri na kutumia rasilimali chache zilizopo na kukamilisha kwa wakati shughuli zote za maandalizi ikiwamo:-
  1. Kazi ya utengaji wa Maeneo ya Kuhesabia Watu katika ngazi ya kitongoji na mtaa ambayo ndiyo msingi wa kufanikisha sensa kwa ubora
  2. Uandaaji wa nyaraka za sensa;
  3. Uundaji wa vikosi kazi/units kwa lengo la kugawana majukumu
  4. Kilichobaki ni kusubiria tuu Agosti 23, kuhesabiwa.
  5. Mimi na familia yangu tutahesabiwa, natoa wito kwako wewe mwenzagu pia uhesabiwe.

Nawatakia Sensa Njema
Paskali
 
Sasa mkuu, unatoa wito kama nani?

Na unaposema tujitokeze kuhesabiwa kwani kuna mkusanyiko mahali?

Sisi tutakuwa nyumbani kuwasubiri hao makarani waje kutudodosa!

Waliposema Agosti 23 hakuna mapumziko uliunga mkono.

Watu wakapiga kelele na kusema haijawahi kutokea siku ya sensa watu wakaenda makazini na hiyo sensa ikafanikiwa.

Hatimaye wakakubali kuweka mapumziko.

Ila bado hiyo siku haitoshi, unajua ni kwa nini? Najua huwezi kujua sababu mpo kulamba viatu vya wakubwa tuu.

Ngoja nipandishe uzi kuonesha how Wizara husika inashindwa kuwa serious.
 
Hivi sisi wa kariakoo itakuaje tutaenda kazini?
 
A
National Bureau of Statistics
Tanzania Census 2022 Maandalizi ya Sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 Yamekamilika, Kazi Iliyobaki ni Moja Tuu, Tujitokeze kwa Wingi kwa Kujituliza, Tuhesabiwe!

Kwa 💯%.

Paskala
Hiyo Ajira unaiita the oldest professional you mean "Dada poa" kimboka au?.
 
Kaka Paskali,
Hili zoezi limeshakosa uwazi na equal participation tokea mwanzo hivyo kuathiri credibility kwa ujumla. Selection process ya wahusika ilijaa bias kutokana na kuingizwa too much politics kwenye mahali pasipostahili. One of the key principles of official statistics ni transparency (WB), hvyo zoezi likishakosa uwazi kuanzia mwanzoni ni lazima matokeo yawe contaminated hvyo kuyapelekea kuwa incredible. Kutokana na lack of transparency participant's wengi watakuwa less motivated kushiriki au kushiriki na kutoa taarifa sahihi ambazo zitapelekea zoezi kuwa useless kwa kutumia gharama nyingi kukusanya irrelevant informations.
Kwa point tuliyofikia, hata methodology wanayotumia ni changamoto mno hvyo kuzidi kukanganya zoeli lenyewe, muda ni silaha na na kwenye aspect hii haupo in favour of the gvt.
 
Wananchi wajitokeze wapi? Wa kuhimiza ni makarani wao ndio wajitokeze majumbani mwa wananchi na wawe fast and professional. Sitegemei maswali ya kuudhi mbele ya familia.

Natoa tena wito; dodoso liwekwe hadharani tujiandae na majibu kurahisisha zoezi. Sijui kwanini inafanywa SIRI.
 
Sasa mkuu, unatoa wito kama nani?

Na unaposema tujitokeze kuhesabiwa kwani kuna mkusanyiko mahali?

Sisi tutakuwa nyumbani kuwasubiri hao makarani waje kutudodosa!

Waliposema Agosti 23 hakuna mapumziko uliunga mkono.

Watu wakapiga kelele na kusema haijawahi kutokea siku ya sensa watu wakaenda makazini na hiyo sensa ikafanikiwa.

Hatimaye wakakubali kuweka mapumziko.

Ila bado hiyo siku haitoshi, unajua ni kwa nini? Najua huwezi kujua sababu mpo kulamba viatu vya wakubwa tuu.

Ngoja nipandishe uzi kuonesha how Wizara husika inashindwa kuwa serious.
Pascal Mayalla kuhesabiwa ni jambo la rohoni au la mwilini? Kama ni la mwilini kwanini Waislam waliisusia sensa na kugoma kuhesabiwa mwaka 2012?
 
Mimi sipo tayari Kaka.. Nishahesabiwa namba saana shuleni, nishawahi saana namba asubuhi shule na sijapata kitu😂

Nikihesabiwa agostu 23 napata nin?
 
My Take
It's very unfortunately kwenye hojaji za sensa, hakuna swali lolote kuhusu idadi ya Watanzania wanaoishi kwa kuitegemea ile ajira ya "the oldest professional" inayoongoza kuajiri watu wengi zaidi duniani kuliko ajira nyingine yoyote!.
Hata serikali yetu haiamini kuwa ile ni kazi halali, lakini ipo na inafanyika na ndio imeajiri idadi kubwa kabisa ya watu kuliko ajira nyingine yoyote! inafanyika kwa aina 3.
1. Watu wenye bahati zao, hawa wameajiriwa rasmi full time wengine formally kwa kulipiwa mahari na Huduma zao kununuliwa kwa bei ya jumla na mteja mmoja kumiliki jumla kwa kuandikisha na kupata hati miliki, au wengine ni kuchukuana tuu au kukubaliana lakini Huduma hizo zinakuwa ni kwa mteja mmoja.
2. Watu wenye bahati zao kumpata mteja mmoja wa kununua jumla, ile uwezo wa mteja huyo mmoja hautoshelezi mahitaji yote ya mhusika hivyo mhusika kujikuta analazimika licha ya kuuza jumla, pia inambidi auze na rejareja kufidia nakisi.
3. Wale wasio na bahati ya kumpata mteja mmoja wa kununua jumla, hivyo kuwajibika kuuza reja reja kwa mteja zaidi ya mmoja.
4. Kuna kundi kubwa la watu ambao wana kazi zao lakini bado wanafanya part time ya professional hii.
Serikali yetu ilipaswa ijue data za idadi ya hawa watu wate, wale wenye bahati walioajiriwa rasmi full time, ndio pekee data zao zitakusanywa na wengine wote hazikusanywi!, laiti serikali ingekusanya ikajua tuu idadi, na sio lazima kuirasimisha biashara hii, ila ingejulikana na kurasimishwa ungefanyika in a decent manner na hata serikali ingekusanya kodi ya maana tuu!.
Huyu ndio Pascal Mayalla sasa. Mzee wa yohana Mtembezi
 
Back
Top Bottom