Taasisi za serikali, LGA’s na nyinginezo huisheni takwimu

jiwe angavu

JF-Expert Member
Aug 28, 2015
19,109
35,940
Wasalaam

Katika uchunguzi mdogo nilioweza kuufanya kwa baadhi ya website za taasisi, mashirika ya serikali na serikali za mitaa.

Nimeweza kubaini takribani 99.9% ya taarifa zilizopo hasa zile za kitakwimu bado hazijahuishwa(updated).

Takwimu za sensa ya watu na makazi zilizopo katika website za taasisi,mashirika pamoja na serikali za mitaa ni takwimu za sensa ya mwaka 2012.

Hivyo basi ni vyema sasa maIT wa taasisi hizo pamoja na serikali za mitaa kufanya uhuishaji wa taarifa hizo za kitakwimu kuendana na uhalisia uliopo kutoka katika takwimu za sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022.

Tujitahidi kwenda na wakati hii ni aibu.

NB:namba za simu na emails za mashirika na taasisi nyingi za kiserikali zilizopo katika website zao huwa ni kama mapambo.

MaendeleoHayanaChama
 
Umeongea ukweli mtupu kaka. Cha kuongezea pia, sio tu takwimu yaani taasisi za serikalini kwenye dissemination ya taarifa kwa ujumla ni tatizo. Tovuti hazina taarifa za kutosha na kuna nyaraka ambazo ni public nazo zinafichwa yaani shida tupu. Ukianza kufanya kazi za research ndo mtu utaelewa zaidi
 
Back
Top Bottom