Habari Wana JF, Kama Heading Inavyosomeka Hapo Juu, Mimi Ni Kijana wa Miaka 29, Nimeajiriwa, Kazi Imenitenganisha Na Familia,( Mzazi Mmoja ambaye Ni Mama, Maana Baba Alifariki Kipindi Nikiwa Mdogo, Nimekua Mlevi Kupindukia, Simu Sipigi Nyumbani, Hela Siioni Inakoelekea, Mama Sina Mahusiano Nae Mazuri, Mahusiano Yangu Hayaeleweki.
Misuko Suko Kibao, Ajali Haziishi, Sioni Wapi Naelekea, Asubuhi ya Leo Wakati Natoka Club , Nikiwa Na Mwanamke Niliempata Huko, Nimepata Ajali Mbaya Sana, Nimepata Majeraha Madogo Tu, Ila Gari Imeumia Sana, Na Kwa Vile Nilikua Nimelewa, Nikampigia GF Wangu Akaja Kushughulikia Kuivuta Gari, Mimi Na Yule Mwanamke Tukawa Tumeshaondoka, Hata Sikufikiria Kama Nitakutwa.
Mbaya Zaidi Nikafumaniwa Na Yule Mwanamke, Ilikua Aibu tupu Mtaani, Naona Siheshimiki Tena, Nyumba Ninayoishi Ni Ofisi Nipo Na Baadhi ya Staff Wenzangu wapo Na Familia Zao, Sijatoka Nje Siku Nzima ya Leo, Kilicho Kichwani Kwangu Ni Kujiua Tu, Sitamani Tena Kuishi, WHY ALWAYS ME? Nimemkosea Nini Mungu, Najua Natenda Dhambi, Ila Niende Huko Labda Nitapumzika. Samahanini Kwa Maelezo Yangu Marefu
Ila Hili Lipo Moyoni Mwangu na Lazima Nilitekeze, Napokea Maoni Yenu Wadau, NAKOSEA WAPI?