Natamani kuachana na wife

Natamani kuachana na wife

We kaka achamawazo finyu huyo ni mkeo na wakat unamuoa ulitabasam sana ulifkil uko kwenye bustan ya eden nn? Ukasahau kuna shda sasa jtambue mpeleke kwenye maomb kwan jehova ndo kila kt akuna limshindalo labda ww ukaid.amna
 
Mpwa wangu nilitamani nikutukane kwa hasira lakini nimekamua kukuonea huruma, kwa kifupi sana matatizo hayakimbiwi, huu ni wakati ambao mkeo anakuhitaji kuliko nyakati zozote zile maishani. Kumbuka anaweza kupona na wewe ukapata matatizo tena makubwa zaidi, je na yeye akukimbie? MUNGU aniepushie lakini ingekuwa mimi nadhani ndio wakati ambao ningemuonyesha upendo wa dhati. Muombe MUNGU akupe uvumilivu manaa sio kwamba hawezi kufanya kazi nyingine anaweza, atapona na ataendelea na maisha kama kawaida.

Nauona uponyaji wake umekaribia sana na mimi nakutangazia uponyaji kwa JINA LA MUNGU alie hai, yeye anayeujua mwanzo wetu na mwisho wetu, maisha yetu na hatima ya maisha yetu yamo mikononi mwake, wala asikudanganye mtu kuwa eti hilo ni jaribu lako No NO, mwambie MUNGU mwamini LEO tu atakuvusha.

Mpende kama vile unamhudumia Mama yako Mzazi, kama vile ambavyo mama zetu hawakukutupa pale ambapo tuliwakojolea na kuwanyea vivyo hivyo do the same. Mpende sana ndio tiba anayoihitaji. Amen
 
wajua ukiwa na mashemegi kama huyu bwana Kifulambute ni hatari, ikiwa mimi naweza kukupiga bistola kabisa......
 
Last edited by a moderator:
Kwanza naomba kujua kama umesha pata kademu nje?
Kisha ndo nitajua nini cha kukushauri..!
 

kwa staili hii kipengele cha kwenye
shida na raha mpaka kifo bora kitolewe tu!!
yani badala umsaidie mkeo unawaza kumuacha
aibu zako!!hujafa hujaumbika babu eee!!
 
Fanya kazi kwa bidii, utengeneze hela za kutosha, kisha umpeleke kwa matibabu mazuri India. Atapona tu. Hayo ni majaribu ya dunia kwako...

Pole sana...ndoa ni upendo ingawa wengine wanasema ni msalaba. Na kama ni msalaba basi muubebe wote, wewe na mkeo.
 
Ahsante sana naamini nitapata mwongozo mzuri...unajua saa nyingine ndio maana mtu anajinyonga kwa kitu kidogo kwa sababu hajashirikisha watu wengine wampe mawazo mazuri na akabadiri mawazo yake.

Usijali mungu ni mwema..mkiwa kitu kimoja na mkeo hakuna linaloharibika ..
 
pole kaka matatizo tumeubiwa wanadamu so huu ni wakati wa kuwa nae na ipo siku mungu atamfuta machozi.. jaribuni hata tiba mbadala kwa mfano huwa wanasema wapare na wahaya huko vijijini wanajua sana dawa za asili..
mimi rafiki yangu alipona kwa dawa za upareni kansa wifi yangu alisaidiwa sana ugonjwa wa sukari huko pareni now anaendea vizuri we thanx GOD.
POLE BRO
 
Watu hapa ni kama hamjanielewa hivi! Suala si kumtelekeza, nampenda xana ila ninahisi kama namuumiza moyo na matatizo anayopata...hakuwahi kuyapata kipindi akiwa alone ila alipokuja kwangu ndio matatizo yanamwandama...hamuoni hapo nina shida?

Hebu tueleze vizuri kijana au kuna kitu unakijua mkeo hajui? Au matatizo hayo umemsababishia we we? Nakushauri tu kuwa karibu nae more than ever! Mpende na mtie moyo kila siku asihisi upweke, mwambie utapigania kwa nguvu zako zote ili afya yake itengemae! Kubwa zaidi mpeleke kwenye maombi Nina uhakika Mungu atamponya!
 
Sina, sihitaji na stahitaji kaka

inawezekana hayo ni mambo ya kishirikina usikatae..kama hospital hapati nafuu anagalieni utaratibu mwingine

mimi nakumbuka wakati nasoma chuo kuna rafiki yangu alitembea na mume wa mtu, mkewe akagundua akamuonya huyo dada aachane na mumewe, lkn hajasikia akaendelea na huyo mama akawafumania tena..kilifouata hapo huyo rafiki yangu alibleed mpaka alisafirishwa na ndege binafsi kwenda nairobi kutibiwa lkn wapi...ndipo akamweleza mama yake mzazi kuwa alitembea na mume wa mtu na huyo mwenye mume alimuapia kuwa kuwa atamtafuta tu sik moja..ndio huyo mama akamtafuta huto mama aliyeibiwa mume na kumuombea mwanae msamaha saaana, huyo dada akapwa dawa za kienyeji akapona lkn pia hadi leo hajapata mtoto..
kwa hivo usidharau mambo ya kienyeji yaweza mponyesha
 
Pole sana kwa mitihani inayo kukuteni,lakini unadhani kumuwacha yeye ndio itakua mwisho wa misukosuko inayokukuta?
jee unadhani huyo mwenzio anafurahia hiyo hali? hakuna mama anaependa kupoteza mwanawe na kama wewe unawapenda watoto wako basi hujafikia hata robo ya mapenzi ya mama kwanawe juu yakua unaumia basi humshindi yeye,rudi kwa mola wako muombe sana tena sana akupe moyo wa subra na jitahidi kwenda kumuona Dr bingwa wa kina mama amchunguze kwa kina na inshallah mwenyezi mungu atakupeni watoto wengine kumbuka hakuna dhiki wa dhiki...
 
Hali vipi mkuu Kifulambute! Umefuatilia kujua nini chanzo cha mke wako kuwa hivyo? Vipi kuhusu haya?
1. utumiaji wa madawa ya uzazi wa mpango.
2. issue ya hormonal balance mwilini
2. Historia ya mahusiano yake hapo mwanzo pamoja na historia ya magonjwa ya zinaa!
But samahani kama nitakuwa nimeku 'offend' mkuu!
Make a thoroughly research on these issues and try to see Doctors specialised in women problems!!!Pole sana mkuu na mwenyezi Mungu akubariki uweze kulishinda hilo jaribu!
Wakuu habari zenu...
Kwa mara nyingine tena naomba tushirikishane kimawazo maana kichwa changu kwa sasa kimeishia hapo kwenye heading.
Mnakumbuka thread yangu ya kitambo niliyoweka kwa headibg ya " kuoa ni lazima" na matatizo niliyopitia ya kuondokewa na watoto wawili kila mmoja akifariki kwa style ile ile ya kufa siku ya kujifungua.

Pamoja na matatizo meengi ya mke wangu kubleed mfululizo. Sasa jana pia imetokea hali ambayo kwa kweli nilifikia hatua ya kukata tamaa kabisa, siku ya alhamis nilisafiri nikaenda Dar kuchukua mzigo wangu na nilimwacha wife akiwa yuko salama kabisa, ile nafika tu dar nikapigiwa simu na wife akinambia ameanza kutokwa na damu(bleed) tofauti kabisa na siku zake kwani aliishamaliza tangu tarehe 7 mwezi huu.

Basi tukafanya taratibu za kuweza kufika hosp na akapata huduma na akarudi home. Sasa jana ndio ilikuwa balaa maana damu zilianza kutoka kwa kasi ya ajabu kiasi kwamba hata akuweka khanga ilikuwa inajaa damu muda mfupi tu na akawa anakosa nguvu na pumzi, nilimkimbiza hosp na tulipofika wakamfanyia ultrasound wakadai cevix ilifunguka na wakamlaza na usiku walimwingiza thearter kwa tiba zaidi. Nashukuru mungu amepata nafuu kiasi.

Sasa napata mawazo sana juu ya wife na matatizo anayoyapata nawaza the best way ambayo haitamuumiza wala sitaumia mimi, maana kwakweli nimefikia mahali nimechoka kwakila namna. Mnakumbuka nilipoteza kazi kwa ajiri ya kumuuguza, sasa sijui tuishi tusifanye lolote ili nisidisturb tena mfumo wake wa uzazi ama sijui tuachane tu.

Am real tired with this life.
 
Last edited by a moderator:
Thread Closed!!!

Naomba kwa Mwenyezi Mungu huyo mwanamke asiye na hatia asipite hapa akaisoma hii thread.

Watu wote wenye mapenzi mema na tuseme AMINA.

cc charminglady

Ameen Babu Asprin, sijui ni kwanini wanaume wengi wana tabia ya kuwakimbia wake zao wakati wa matatizo kama ugonjwa. Hawajui maana ya viapo vya ndoa.

Mie kuna uncle angu aliparalise 4yrs ago lakini aunt hajamuacha hata kidogo. Huwa inafikia mahali anakuwa kama kichaa anapiga mayowe usiku mzima alia kama mtoto na vituko vyote includes kujisaidia mahali alipo lakini aunt anavumilia tu make anajua maana ya kiapo cha ndoa. Lait ingelikuwa ni mwanaume angeshatafuta mke na kumuoa haraka sana


Dah... Mwenyezi Mungu akulaani wewe mtoa mada! si ajabu ukaachana na mkeo ukadondokea sehemu ambayo hutokaa usahau make HUJAFA HUJAUMBIKA.....

Nakumbuka Mchungaji mmoja alisema "Ukimzaa mtoto mtukutu ni wako, ndiye Mungu aliona azaliwe kwako na wewe ndiwe unayeweza kumlea" Ukiwa na mke/mme mwenye matatizo ni wako maana Mungu aliona wewe ndiwe unawezana naye" So huo ni mzigo wako labda kama mlichukuana tu kujikinga mvua ila kama mlifunga ndoa takatifu aaah... Imekula kwako!!!!
 
Last edited by a moderator:
Vumilia mkuu natumai madaktari wataweza kupatia ufumbuzi tatizo la mkeo pia kumbuka:

Wedding Vows

I, (name), take you (name), to be my
(wife/husband), to have and to hold from
this day forward, for better or for worse,
for richer, for poorer, in sickness and in
health, to love and to cherish; from this
day forward until death do us part.
 
Kwa YESU hakuna lililogumu,
YESU anasema"Jitwike msalaba wako na unifuate,maana nitafanya njia pasipo na njia"
Na tena"Onjeni muone jinsi BWANA alivyo mwema.
Ukiokoka,utakuwa umechagua fungu lililo jema,na matatizo uliyonayo yatakwisha!
 
masikini yawezekana kwa mawazo uliyafikia utakuwa unamjibu vibaya akikwambia anaumwa....very very bad and paining.
 
umenikere unavosema unataka kumuacha fikiria ungekua ni wew au dada ako kafanyiwa ivo ingekuaje?MUOGOPE MUNGU KAKA
 
Nahisi network bar za akili yako zimepungua. Mnara hausomi vizuri
 
Back
Top Bottom