Natamani kuachana na wife

Natamani kuachana na wife

Amina. Haya sasa ndo maneno ya kiumeni. Lipinge sana pepo la kumwacha mkeo.

Mjumbe kanambia huyu mchungaji wa manzrse alikuwa na huduma magomeni kwa siku kumi...mliohudhuria jamani naombeni msaada wa kupata number zake kama alitoa
 
Utafanya jambo la maana sana kama utaamua kumpa YESU maisha yako afanyike mwokozi wako naye atatatua shida zako zote kwani anasema tumwite yeye na tumweleze mambo yetu yeye ujishughulisha sana na mambo yetu, na yeye ndiye anaweza kwani hata uwezo walionao matabibu ni yeye Mungu amewapa hivyo atakosa yeye kumponya mkeo CHUKUA HATUA YA KUOKOKA UTAONA MAKUU AMBAYO MUNGU ATAKUTENDEA
Nashukuru sana....nampigia sasa hivi, unajua katika matatizo watu wanasahau kuwa shetani hufanya kazi kubwa, nimejaribu kuongea na wife na kwakweli itabidi tu tuokoke hakuna njia nyingine...
 
Mpaka unaandika hii thread ushapoteza kiasi flani cha mapenzi kwa mke wako. Wrong way mkuu, unachotakiwa ni kumjali na kumpenda mke wako sir, mapenzi ya kweli yanaonekana wakati wa shida. Muombe msamaha kwa lile ulilolifikiria akilini mwako ni shetani tu amekupitia
 
Kijana pole sana kwa matatizo!
Ni ukweli kuwa mliapa kuishi kwa kila hali na hili ndilo unalotakiwa kufanya! Wengi tumemshambulia ku uselfish wake na vitu kama hivi! Kama mtakuwa mmemsoma vizuri hamtachelea kuona kuwa kapitia mengi! Alishafutwa kazi huko nyuma kwa ajili ya matatizo ya mkewe! Sasa kawa mjasiria mali lakini bado yanaendelea! Kuna hapa amesema "Nashukuru mungu amepata nafuu kiasi. Sasa napata mawazo sana juu ya wife na matatizo anayoyapata nawaza the best way ambayo haitamuumiza wala sitaumia mimi,"
Kama angekuwa selfish asingefikiria namna ambayo wote hawataumia! Akaendelea "maana kwakweli nimefikia mahali nimechoka kwakila namna" Amefikia mahali hajui afanye nini labda pia anahisi hatakiwi kumgusa mkewe ili asimpatie madhara zaidi. Hapa ndo napata mashaka kidogo! Kwani ndugu yangu huwa haya yanatokea mkifanya kitu? I mean kukutana kimwili? Kama ndiyo basi tatizo linaweza kuangaliwa kuanzia hapo! Labda!
Mimi nikushauri tu, angalieni historia yenu ya huko nyuma, Mkeo alikuwa na tatizo hili kabla hamjaoana? Je wewe vipi! Inawezekana umejaaliwa pia! Mahusiano ya nyuma kwa maana ya wapenzi wenu kabla ya ndoa yenu.
Kaeni chini ninyi wawili mkubaliane kuanza kulishughulikia tatizo hilo kwa pamoja na sio mlaumiane. Kuchoka na maisha ni kutafuta shortcut! Na hii inaweza kukumiza zaidi. Njia sahihi ni kukabiliana na shida na sio kukimbia shida! Punguza mawazo kuwa jasiri kwa kumtanguliza Mungu mbele. Daima songa mbele kijana nyuma mwiko! Kila la kheri
 
Dunia inapokuwa imekuinamia.ni rahisi kufikiri nje ya mstari mshaurini badala ya kumshambulia na kumuona evilish!!!!!

Mkuu pole sana kaza moyo sikiliza ushauri wanasema ukubwa jalala we vumilia ya hapa lakini utapata jawabu humu naamini!!!!!

Tafuta Gynaecologist sio just daktari pale OPD na akuambie kinaga ubaga nini shida hapo kama ngumu mshauriane kutoa kizazi tu,sounds harsh lakini yaweza kiwa ndio permanent solution(God forbid)!!!!!

La maombi nalo neno think about it!!!
 
kwa shida na raha...................

uombe sana ufe bila kupata tatizo lolote

badala kumsupport mkeo na mkaenda kwa madaktari bingwa unataka kumuacha?

shame on you.....

ulidhani ndoa ni kugegedana tu eee?

Ukiambiwa kuishi kwa shida na kuvumiliana ndio hayo unatakiwa uvumiliee,ila kua na imani muombe Mungu maana shetan anapita katikati yenu
Jaribu kumpeleka kwa ma shekhe kuna dua atasomewa maana huko kubleed sana itakua jini mahaba wengi wenye nayo hutokwa damu sana na pia hiyo mikosi na misukosuko ni yenyewe
Usipoangalia na kuwa makini utampoteza mkeo
Mpende mkeo
 
Mie naomba niwe wa kwanza kutomrushia mtoa mada mawe........................
Natambua kwamba umekata tamaa na hali halisi hasa ukizingatia kwamba watoto umepoteza, mke hawez kukupa huduma yake ipasavyo na furaha na amani ndani ya nyumba yako haipo.

jambo la kufanya kwanza kabisa usikimkbie tatizo bali tatua tatizo, utalitatuaje njia ni kama hizi
Mshirikishe Mungu kwenye hili tatizo lako................pia onana na wataalam wa masuala ya uzazi na wanawake.

ulivyoandika napata hisia kwamba mkeo ana kitu kinaitwa POLICYPTIC OVARIES ama PCO .
 
Mjumbe kanambia huyu mchungaji wa manzrse alikuwa na huduma magomeni kwa siku kumi...mliohudhuria jamani naombeni msaada wa kupata number zake kama alitoa

Wanasema usimkimbilie mungu wakati wa shida ikiisha mnakimbia...ebu kwanza tubuni zab 51 we na mkeo halafu kuna zab 86 muisome asubhui na usiku..hayo mawazo ya kurogwa muyaondoe maana mkianza hivyo sasa hivi mtapata walimu wa waganga mtamaliza pesa zenu..halafu unajua kwenye maisha kuna mengi sana aswaa wanaume mnawaambia watoto wa watu mtawaoa halafu mnaingia mitini.sasa sio wote wana roho nzuri wengine wanakuwa na vinyongo anahapa atakukukomesha.sasa baada ya kudili na wewe anaanza na mkeo ambae ajui lolote..kuna mistari naitafuta ya kuvunja maagano nikiipata nitakutumia lakini trust me ukisoma hizo.zaburi mungu atawaongoza hiyo 51 someni mara moja tu kuyubu halfu ya 86 kila siku asubhui na usike.kila la kheri
 
Amina Asprin

Mkuu Kifulambute.. ngoja ni assume kuwa matatizo ya kumwuguza mkeo na kupoteza watoto mara kadhaa yamekufanya ushindwe kufikiri vyema.. ulichokiandika kinasikitisha sana hasa ukizingatia mkeo hajapenda kuwa hivyo(hujafa hujaumbika)!

Ukimwacha wewe nani atamchukua?
Mkuu hapa ndipo tunaposema ndoa inahitaji uvumilivu na upendo wa kweli (katika shida na raha)? Umumilivu wako ndio umeishia hapo?

Kukimbia tatizo sio kupata suluhu ya tatizo, ni vyema mkaonana na madaktari wazuri wa wanawake kwa uchunguzi zaidi, lakini pia kulingana na imani yenu mwombeni Mungu.. hakuna linaloshindikana kwake.
 
Last edited by a moderator:
Mie naomba niwe wa kwanza kutomrushia mtoa mada mawe........................
Natambua kwamba umekata tamaa na hali halisi hasa ukizingatia kwamba watoto umepoteza, mke hawez kukupa huduma yake ipasavyo na furaha na amani ndani ya nyumba yako haipo.

jambo la kufanya kwanza kabisa usikimkbie tatizo bali tatua tatizo, utalitatuaje njia ni kama hizi
Mshirikishe Mungu kwenye hili tatizo lako................pia onana na wataalam wa masuala ya uzazi na wanawake.

ulivyoandika napata hisia kwamba mkeo ana kitu kinaitwa POLICYPTIC OVARIES ama PCO .

Nashukuru sana kwa ushauri wako...naufanyia kazi ntakuja kukupa majibu
 
wakuu habari zenu...
Kwa mara nyingine tena naomba tushirikishane kimawazo maana kichwa changu kwa sasa kimeishia hapo kwenye heading.
Mnakumbuka thread yangu ya kitambo niliyoweka kwa headibg ya " kuoa ni lazima" na matatizo niliyopitia ya kuondokewa na watoto wawili kila mmoja akifariki kwa style ile ile ya kufa siku ya kujifungua.

Pamoja na matatizo meengi ya mke wangu kubleed mfululizo. Sasa jana pia imetokea hali ambayo kwa kweli nilifikia hatua ya kukata tamaa kabisa, siku ya alhamis nilisafiri nikaenda dar kuchukua mzigo wangu na nilimwacha wife akiwa yuko salama kabisa, ile nafika tu dar nikapigiwa simu na wife akinambia ameanza kutokwa na damu(bleed) tofauti kabisa na siku zake kwani aliishamaliza tangu tarehe 7 mwezi huu.

Basi tukafanya taratibu za kuweza kufika hosp na akapata huduma na akarudi home. Sasa jana ndio ilikuwa balaa maana damu zilianza kutoka kwa kasi ya ajabu kiasi kwamba hata akuweka khanga ilikuwa inajaa damu muda mfupi tu na akawa anakosa nguvu na pumzi, nilimkimbiza hosp na tulipofika wakamfanyia ultrasound wakadai cevix ilifunguka na wakamlaza na usiku walimwingiza thearter kwa tiba zaidi. Nashukuru mungu amepata nafuu kiasi.

Sasa napata mawazo sana juu ya wife na matatizo anayoyapata nawaza the best way ambayo haitamuumiza wala sitaumia mimi, maana kwakweli nimefikia mahali nimechoka kwakila namna. Mnakumbuka nilipoteza kazi kwa ajiri ya kumuuguza, sasa sijui tuishi tusifanye lolote ili nisidisturb tena mfumo wake wa uzazi ama sijui tuachane tu.

Am real tired with this life.
kwani ukimuacha ndo atapona au??kama kweli ni mkeo ujue unatakiwa ukae naye katika shida na raha na hiyo ndio maana halisi ya ndoa,ndoa sio raha tu bali kuna matatizo pia.
 
Wanasema usimkimbilie mungu wakati wa shida ikiisha mnakimbia...ebu kwanza tubuni zab 51 we na mkeo halafu kuna zab 86 muisome asubhui na usiku..hayo mawazo ya kurogwa muyaondoe maana mkianza hivyo sasa hivi mtapata walimu wa waganga mtamaliza pesa zenu..halafu unajua kwenye maisha kuna mengi sana aswaa wanaume mnawaambia watoto wa watu mtawaoa halafu mnaingia mitini.sasa sio wote wana roho nzuri wengine wanakuwa na vinyongo anahapa atakukukomesha.sasa baada ya kudili na wewe anaanza na mkeo ambae ajui lolote..kuna mistari naitafuta ya kuvunja maagano nikiipata nitakutumia lakini trust me ukisoma hizo.zaburi mungu atawaongoza hiyo 51 someni mara moja tu kuyubu halfu ya 86 kila siku asubhui na usike.kila la kheri

Ahsante sana naamini nitapata mwongozo mzuri...unajua saa nyingine ndio maana mtu anajinyonga kwa kitu kidogo kwa sababu hajashirikisha watu wengine wampe mawazo mazuri na akabadiri mawazo yake.
 
huyo shateni anayetaka kuvunja ndoa yako na ASHINDWE! kaka kumbuka maradhi pia tumeumbiwa sisi binadamu, sasa imajin leo (sio kwa nia mbaya lkn) umetoka tu nje hapo unapata ajali labda unapata ulemavu wa kudumu au tu unapata janga lolote lile, ungejisikiaje mkeo angekuwa na maamuzi km yako hayo unayotaka kuyafanya?fikiri ingekuwa ni wewe ndio una maradhi Fulani ungejisikaje kuachwa na mkeo kisa tu maradhi?km hospital zimehangaika sana basi angalieni na upande wapili nendeni kwenye maombi kutegemeana na imani yenu ili tatizo lipate pia mkono wa Mwenyezi Mungu ili apone...mi naamini atapona tu...huo ni mtihani tu ndg yangu, mpende mkeo na uache kbs wazo la kumuacha waweza kulaanika na ukumbuke laana ya mke inashika...kila la kheri.
 
Wanasema usimkimbilie mungu wakati wa shida ikiisha mnakimbia...ebu kwanza tubuni zab 51 we na mkeo halafu kuna zab 86 muisome asubhui na usiku..hayo mawazo ya kurogwa muyaondoe maana mkianza hivyo sasa hivi mtapata walimu wa waganga mtamaliza pesa zenu..halafu unajua kwenye maisha kuna mengi sana aswaa wanaume mnawaambia watoto wa watu mtawaoa halafu mnaingia mitini.sasa sio wote wana roho nzuri wengine wanakuwa na vinyongo anahapa atakukukomesha.sasa baada ya kudili na wewe anaanza na mkeo ambae ajui lolote..kuna mistari naitafuta ya kuvunja maagano nikiipata nitakutumia lakini trust me ukisoma hizo.zaburi mungu atawaongoza hiyo 51 someni mara moja tu kuyubu halfu ya 86 kila siku asubhui na usike.kila la kheri

Zaburi Husaidia Sana...
 
Wakuu habari zenu...
Kwa mara nyingine tena naomba tushirikishane kimawazo maana kichwa changu kwa sasa kimeishia hapo kwenye heading.
Mnakumbuka thread yangu ya kitambo niliyoweka kwa headibg ya " kuoa ni lazima" na matatizo niliyopitia ya kuondokewa na watoto wawili kila mmoja akifariki kwa style ile ile ya kufa siku ya kujifungua.

Pamoja na matatizo meengi ya mke wangu kubleed mfululizo. Sasa jana pia imetokea hali ambayo kwa kweli nilifikia hatua ya kukata tamaa kabisa, siku ya alhamis nilisafiri nikaenda Dar kuchukua mzigo wangu na nilimwacha wife akiwa yuko salama kabisa, ile nafika tu dar nikapigiwa simu na wife akinambia ameanza kutokwa na damu(bleed) tofauti kabisa na siku zake kwani aliishamaliza tangu tarehe 7 mwezi huu.

Basi tukafanya taratibu za kuweza kufika hosp na akapata huduma na akarudi home. Sasa jana ndio ilikuwa balaa maana damu zilianza kutoka kwa kasi ya ajabu kiasi kwamba hata akuweka khanga ilikuwa inajaa damu muda mfupi tu na akawa anakosa nguvu na pumzi, nilimkimbiza hosp na tulipofika wakamfanyia ultrasound wakadai cevix ilifunguka na wakamlaza na usiku walimwingiza thearter kwa tiba zaidi. Nashukuru mungu amepata nafuu kiasi.

Sasa napata mawazo sana juu ya wife na matatizo anayoyapata nawaza the best way ambayo haitamuumiza wala sitaumia mimi, maana kwakweli nimefikia mahali nimechoka kwakila namna. Mnakumbuka nilipoteza kazi kwa ajiri ya kumuuguza, sasa sijui tuishi tusifanye lolote ili nisidisturb tena mfumo wake wa uzazi ama sijui tuachane tu.

Am real tired with this life.

Kama we ni mkristo, basi utakumbuka msomo Hui " for better or worse. And in sickness and health." Hivyo ni mke wako.l Anaitaji support kutoka kwako. mungu awatie nguvu na ujasiri katika kipindi hiki kigumu.
 
Back
Top Bottom