Natamani kuachana na wife

Natamani kuachana na wife

When we claim to love someone and stand on their side for better for worse....and we fail to fulfill that in actions.....its shame........stand for your words.....mapito haya...kesho ukapata ajali ukapoteza miguu(Mungu epushia mbali) mkeo akikukimbia utarud kusema apa wanawake wana roho mbaya.....
 
kama ulifunga ndoa, kumbuka kiapo cha ndoa, kumkimbia ni kuacha jeraha kwake, tafakari ndugu yangu, maisha yanabadirika. inasikitisha lakini ndio mkeo. ukiona unakata tamaa mshirikishe MUNGU, maana yeye ni mwaminifu na hajawahi kushindwa.
 
Nachoweza kushauri kwa haraka hebu fanya utaratibu wa kuwaona madaktri bingwa wa akina mama ili wakueleze kwa umakini nini tatizo hasa linalomkabili mkeo?? Kwa maelezo haya Napata mashaka kidogo kujibu chochote kile. Kama utaweza nenda aghakhan hospital (dar) yuko dr. shafiq anaweza walau kukupa mwangaza kidogo.
 
Umepoteza sifa ya kuwa mme na baba.Kwahiyo ungekuwa ni wewe unaugua hivyo na yeye akuache?.
 
Madaktari wamefanya yao......mpe nafasi MUNGU pia afanye yake, shirikisha ndugu wa karibu mfunge kwa maombi,
pia mpeleke kanisan...., trust mi..MUNGU hashindwi na kitu chochote
 
Usisahau pia kama walivosema wachangiaji wengine tafuta watumishi wa kweli waombe kwa ajili yake maana humu dunia kuna vingi tusivyoweza kuona kwa macho ya kawaida.
 
Nakuomba sana, achana na mawazo ya kumuacha kwa sababu ya hayo matatizo, hayo hakujitakia yeye.
 
May she get well soon jamani,dah..she is rly sufferring
 
Imagine ingekua ni wewe umepata tatizo...... hujafa hujaumbika brother.
Akitoka hospital mpeleke akafanyiwe maombi. Labda walimwengu hao

Ni kweli kabisa na hakuna ajuaye kesho yake mpeleke kwenye maombez huyo Mungu atamponya linaloshindikana kwa binaadam kwa Mungu linawezekana
 
Watu hapa ni kama hamjanielewa hivi! Suala si kumtelekeza, nampenda xana ila ninahisi kama namuumiza moyo na matatizo anayopata...hakuwahi kuyapata kipindi akiwa alone ila alipokuja kwangu ndio matatizo yanamwandama...hamuoni hapo nina shida?
 
Bora na ww umeona. Kuna watu hawana mioyo jamani bali mawe! Inahuzunisha sana kua na mwanaume wa hivyo.

Laiti ningekuwa Mungu, ningehamisha huu ugonjwa kwa hili janaume lenzangu. Maadam halina K, ningekuwa nalimwagisha damu matak.oni afu nione kama lingepata wazo la kumwacha mkewe. Kweli kabla hujafa hujaumbika.

Mungu atunusuru na atusamehe dhambi zetu.

Tuendelee tu kuitikia AMINA ili huyu mwanamke asiye na hatia apate uponyaji toka kwa Mungu.

AMINA.
 
Watu hapa ni kama hamjanielewa hivi! Suala si kumtelekeza, nampenda xana ila ninahisi kama namuumiza moyo na matatizo anayopata...hakuwahi kuyapata kipindi akiwa alone ila alipokuja kwangu ndio matatizo yanamwandama...hamuoni hapo nina shida?

Unajuaje kama unamuumiza moyo? Alikuambia? Afu hapo ulipoandika "xana" badala ya sana nimeshakuelewa. Bado we u mvulana sana. Nani alikuharakisha uoe?
 
Maamuzi ya kumuacha mkeo akiwa mgonjwa sio sahihi kabisa labda kama kuna sababu nyingine imejificha maana watu wengi hapa wanakulaumu tu inawezekana kuna kero nyingi umezivumilia sasa unaona hata ile hali ya ubinadamu inakutoka. Ki uweli wanawake wa sasa hapendwi mtu ni pochi lako tu na wana roho mbaya sana nakumbuka wazee watu walituasa ishini nao kwa akili sana. Same woman would possibily have not tolerated the way you did...
Nafahamu rafiki yangu aliachwa na mke wake wa ndoa tgena wana watoto when he was sacked from kibaruani na ametaabika sana mpaka sasa amesimama. Msiangalie tu kuwa anataka kumuacha kwa kuwa mkewe anaumwa ugonjwa sugu bali inawezekani hio ni sababu tu lakini ukweli ni kuwa yawezekana amevumulia sana kero za wanawake wa kileo. Mkuu funguka zaidi ili wadau watoe ushauri stahiki na sio ushauri wa kuoneana huruma kwa tatizo lililojificha...
 
Back
Top Bottom