Natamani kuachana na wife

Kifulambute

JF-Expert Member
May 8, 2011
2,539
755
Wakuu habari zenu...
Kwa mara nyingine tena naomba tushirikishane kimawazo maana kichwa changu kwa sasa kimeishia hapo kwenye heading.
Mnakumbuka thread yangu ya kitambo niliyoweka kwa headibg ya " kuoa ni lazima" na matatizo niliyopitia ya kuondokewa na watoto wawili kila mmoja akifariki kwa style ile ile ya kufa siku ya kujifungua.

Pamoja na matatizo meengi ya mke wangu kubleed mfululizo. Sasa jana pia imetokea hali ambayo kwa kweli nilifikia hatua ya kukata tamaa kabisa, siku ya alhamis nilisafiri nikaenda Dar kuchukua mzigo wangu na nilimwacha wife akiwa yuko salama kabisa, ile nafika tu dar nikapigiwa simu na wife akinambia ameanza kutokwa na damu(bleed) tofauti kabisa na siku zake kwani aliishamaliza tangu tarehe 7 mwezi huu.

Basi tukafanya taratibu za kuweza kufika hosp na akapata huduma na akarudi home. Sasa jana ndio ilikuwa balaa maana damu zilianza kutoka kwa kasi ya ajabu kiasi kwamba hata akuweka khanga ilikuwa inajaa damu muda mfupi tu na akawa anakosa nguvu na pumzi, nilimkimbiza hosp na tulipofika wakamfanyia ultrasound wakadai cevix ilifunguka na wakamlaza na usiku walimwingiza thearter kwa tiba zaidi. Nashukuru mungu amepata nafuu kiasi.

Sasa napata mawazo sana juu ya wife na matatizo anayoyapata nawaza the best way ambayo haitamuumiza wala sitaumia mimi, maana kwakweli nimefikia mahali nimechoka kwakila namna. Mnakumbuka nilipoteza kazi kwa ajiri ya kumuuguza, sasa sijui tuishi tusifanye lolote ili nisidisturb tena mfumo wake wa uzazi ama sijui tuachane tu.

Am real tired with this life.
 
Mkuu Kifulambute hebu mpeleke kwa wataalam wajue tatizo ni nini kuliko hili la kupata matibabu na kurudi na hali inajirudia tena
Ni mke wako mkuu na ulishaapa kuwa nae kwa shida na raha na hayo ni maumivu kama maumivu mengine tafuta wataalam ambao wanaweza kukuambia tatizo ni nini mkuu kabla ya kumuacha
 
Last edited by a moderator:
Wakati unamuoa uliapa utakuwa naye kwa shida na raha. What happened? Imagine wewe ndo ungekuwa unaumwa hlf yeye akachoka kukuhudumia akakuacha ungejisikiaje? Pole.sana lkn acha ubinafsi

Thread Closed!!!

Naomba kwa Mwenyezi Mungu huyo mwanamke asiye na hatia asipite hapa akaisoma hii thread.

Watu wote wenye mapenzi mema na tuseme AMINA.

cc charminglady
 
Last edited by a moderator:
Imagine ingekua ni wewe umepata tatizo...... hujafa hujaumbika brother.
Akitoka hospital mpeleke akafanyiwe maombi. Labda walimwengu hao
 
Wewe ni muamini wa imani gani?

Kama ni Mkristo hebu tafuta kanisa lolote lenye huduma ya kuombea watu wenye shida zisizoelezeka kitabibu kama hizi...

Kuna mauzauza mengi ambayo kwa namna ya kawaida sisi wanadamu hatuwezi kuyatambua, ila yule aliyetuumba anajua namna ya kudeal nayo...
 
mh!umefika mbali sana vumilia na ufanye uchunguzi wa kina kwa wataalamu wa magonjwa ya wanawake kumbuka ulikula kiapo na linaweza kua jaribu kwako upimwe imani yako ucje ukaruka majivu ukakanyaga moto dunia ni mwalimu icje ikakufunza muuguze mkeo na mwombe Mungu akupe ujasiri sana na akuonyeshe mlango wa kutokea.
 
i feel sorry for your wife

unaitimiza vipi ahadi ya kuishi kwa shida na raha,ugonjwa na uzima mpaka kifo kitakapowatenganisha?
hakuna kitu kitamuumiza maishani mwake kama wewe kumuacha kwa sababu ya hali ya ugonjwa aliyo nayo

mpeleke hospitali..afanyiwe uchunguzi zaidi na tiba..

msimsahau Mungu..salini sana
 
Usimuache,hata yeye hakupenda awe hivyo! she is your wife,kuwa tayari kuteseka nae kwani upendo wa kweli haupo ktk maneno,upo ktk vitendo na unathibitika wakati wa shida...thibitisha upendo wako kwake sasa! huwezi jua Mungu atamponya lini,unaweza muacha afu ndio akapona! utajisikiaje?...kwa wale wakristo Biblia inaruhusu divorce only kama mkeo au mumeo kazini(sexual immorality),vinginevyo "NO DIVORCE" mbaka kifo kiwatenganishe...mi naomba Mungu amponye mkeo,True love never dies.
 
Huo ni uselfish wa hali ya juu je unafikili hiyo hali yeye anaichekelea na je umejiuliza kati ya wewe na yeye nani ina mdhuru hiyo hali zaidi acha kuwa na mfume dume usio na kichwa wala miguu.HUO NDIO MUDA MUAFAKA WA KUMFARIJI MKEO NA KUONESHA UPENDO WAKO WA KWELI KWENYE MATATIZO YAKE؛
KIFUPI NIMEKUDHARAU SANA NA UMENIUDHI KWA KUANDIKA WAZI ETI TUACHANE SASA KAMA MTU KAMA HUYO AWE MGENI WA NANI?
 
Back
Top Bottom