Natamani kuachana na wife

Natamani kuachana na wife

Nenda kwa wataalamu kwa uchunguzi zaidi. Na pia usisahau kwenda kwenye maombezi, tafuta watu/kanisa ambako kuna huduma hiyo watakusaidia kwani hakuna lisilowezekana kwa Mungu. Ungekua umeenda oka kipindi ulipopoteza mtoto wa kwanza sasa hivi ingekua hadithi tu angeshapona.
 
Shetani huwa anahangaika sana na ndoa,manake anajua akileta matatizo katika ndoa hapo uzinzi ndio unainuka,mafarakano na kutengana kabisa.Huu muda sio wa kukata tamaa na kutamani kuachana na mkeo,kilichounganishwa na Mungu hakuna binadamu anaeweza kukitenganisha.kataa hiyo roho ya kukata tamaa,mkabidhi Yesu matatizo yenu,yeye ndie jibu kamili.Omba sana kwa ajili ya mkeo,tubu pia,mpeleke kwenye maombi Mungu ni mwema na hakika atawavusha katika hili pito.
 
Huyu jamaa amepata stress, ushauri tafuta pesa mingi umtaftie matibabu ya uhakika...kuachana naye kwa kigezo cha ugonjwaaaaa?? Na wewe ungekua mgonjwa ungeachwa? Kaa chini fikiria namna ya kusolve hilo jambo na siyo kusema unaachana naye.

I think definition ya mwanaume ibadilishwe aisee...
 
pole sana mkuu, omba sana na mwenyezi Mungu atawatatulia matatizo haya, mpeleke ktk maombi
 
Inasikitisha sana hebu mpeleke na kanisani aombewe pia,mavitu mengine yawezekana ni spiritual staffs
 
jifunzeni kumtegemea Mungu na muombe yataisha unless ukimuacha utakayemleta matatzo yake yatakua mara kumi,tatzo lipo kwako kuna pepo anakusumbua nenda kafanyiwe maombi epuka waganga awanajibu sahihi
 
Kama salio halisomi sema tupige upatu humu humu daftari litembezwe kumwacha sio suruhisho la matatizo.
Usije kuwa unajishebedua shebedua hapa kumbe pochilow.
 
Pole sana Bro
Unajua kwenye maisha kuna mitihani mingi ambayo tunapaswa tuifaulu ndio tupande daraja.
Hapo mi ushauri wangu wa bure kabisa ambao ndo utakuwa useful kwako ni kwamba; 1. Naomba usikate tamaa, endelea kumshughulikia kwa namana yoyote ile kwa madaktari na kufuata ushauri mnaopewa na kuufuata 2. Usisikilize mashauri ya kipuuzi kwamba uende kwa mganga au umuache mkeo 3. Maombi ni Muhimu, ukishindwa mpeleke kwa watumishi wa Mungu 4. Ondoa kabisa wazo la kumuacha!!! Unapoona mambo yanavyoharibika Mungu anakuwa ndio amekuwekea baraka yako hapo hapo!!!! Umenielewa???? Baraka yako iko kwa huyo huyo mwanamke, we endelea kumhudumia utakuja kuona matokeo yake na bila shaka utakuja kutushuhudia humuhumu kwenye JF Mungu alivyokufanyia.
 
Nahisi uchungu kwa jinsi ulivyoandika, namuonea huruma mwanamke mwenzangu.
Naomba usithubutu kumuacha huyo ni mkeo, hayo yanapita tu. Mpeleke akaombewe.
 
Wakuu habari zenu...
Kwa mara nyingine tena naomba tushirikishane kimawazo maana kichwa changu kwa sasa kimeishia hapo kwenye heading.
Mnakumbuka thread yangu ya kitambo niliyoweka kwa headibg ya " kuoa ni lazima" na matatizo niliyopitia ya kuondokewa na watoto wawili kila mmoja akifariki kwa style ile ile ya kufa siku ya kujifungua.

Pamoja na matatizo meengi ya mke wangu kubleed mfululizo. Sasa jana pia imetokea hali ambayo kwa kweli nilifikia hatua ya kukata tamaa kabisa, siku ya alhamis nilisafiri nikaenda Dar kuchukua mzigo wangu na nilimwacha wife akiwa yuko salama kabisa, ile nafika tu dar nikapigiwa simu na wife akinambia ameanza kutokwa na damu(bleed) tofauti kabisa na siku zake kwani aliishamaliza tangu tarehe 7 mwezi huu.

Basi tukafanya taratibu za kuweza kufika hosp na akapata huduma na akarudi home. Sasa jana ndio ilikuwa balaa maana damu zilianza kutoka kwa kasi ya ajabu kiasi kwamba hata akuweka khanga ilikuwa inajaa damu muda mfupi tu na akawa anakosa nguvu na pumzi, nilimkimbiza hosp na tulipofika wakamfanyia ultrasound wakadai cevix ilifunguka na wakamlaza na usiku walimwingiza thearter kwa tiba zaidi. Nashukuru mungu amepata nafuu kiasi.

Sasa napata mawazo sana juu ya wife na matatizo anayoyapata nawaza the best way ambayo haitamuumiza wala sitaumia mimi, maana kwakweli nimefikia mahali nimechoka kwakila namna. Mnakumbuka nilipoteza kazi kwa ajiri ya kumuuguza, sasa sijui tuishi tusifanye lolote ili nisidisturb tena mfumo wake wa uzazi ama sijui tuachane tu.

Am real tired with this life.
Huna akili
 
Back
Top Bottom