Nataka Rais Magufuli ashindwe

Nataka Rais Magufuli ashindwe

Status
Not open for further replies.
Kwani mtu ukitoa maoni yako pasipo kutoa matusi au ukianzisha uzi wenye uhalisia na usio wa kichochezi unakuwa na hofu ya nini?

Tatizo lililopo kuna baadhi yetu tumekuwa maarufu kutunga stori za uongo na kuzijengea hoja then tunataka jamii iamini kama ni kweli kumbe ni upotoshaji

Mtu kama umeanzisha mada yako na ushahidi unao kwa nini uogope? Endapo utahitajika polisi si unapeleka ushahidi?

Fikiria mtu anayeanzisha uzi hapa eti Dangote anahamishia kiwanda Kenya na hizo habari zinasambaa dunia nzima kumbe ni uonge pasipo kufikiria negative impacts kwa wawekezeji walioko huko nje. Mtu kama huyu leo hawezi fanywa kitu sababu tu anatumia ID feki sishangai kesho akaibuka na jambo jingine

Watu wa namna hii lazima washughulikiwe hakuna kulea ujinga. Watanzania tumekuwa maarufu sana wa kupika majungu

Ninakubaliana na wewe kabisa uhuru wa kutoa maoni lazima uheshimiwe na watawala kwani ni takwa la kikatiba lakini uhuru huo lazima uzingatie utu na nidhamu.

Leo mtu akimchukia mtu flani sababu za kiitikadi za vyama au jambo lolote, kesho anamtungia tuhuma na kusambaza kwenye mitandao. Vitu vya namna hiyo siyo vya kulea
Kwani Dangote akihamishia kiwanda chake Kenya inajuzu nini? Maana vizabi zabina waliolianzisha na kulieneza suala hilo ni Wa Serekale wenyewe, sasa kwa nini wadandiaji waonekane wahalifu kuliko waanzilishi!!!
 
DAH, mkuu umeongea POINT sana ,tatizo watu wanaendeshwa ka mihemko badala ya kuufikirisha ubongo na tafakuri za kina,kweli kuna haja ya uwepo wa uhuru wa maoni tena mpana na usio na mwisho lakini uhuru huo usiwe wa mtu kaamka na mindoto yake anakuja humu anatoa stori za ajabu ajabu za kutunga tunga kisha aachiwe tu,

hata huko kwa wenzetu uhuru hupo ila wanautumia kwa nji ipasavyo,mfano kuna mijitu hapa Jf lazima kila siku iweke uzi ambao hauna kichwa wa miguu mradi tu naye aonekane ameweka uzi,kwa kweli ukifikiria sana unaona sisi wenyewe ndio tunajikosea heshima na kuifanya serikali itafute nji ya kuminya uo uhuru,ikumbukwe haijakatazwa kukosoa,kaa kukosoa tukosoe sana tena bila aibu wala hiyana yeyote lakini katika kosoa hiyo tuzingatia ukweli,staha na madhara ya huo ukosoaji wake,

wakati mwingine unasoma uzi unajiuliza huyu ni mtanania kweliii au ni pandikizi la mataifa jirani? ndugu zanguni machafuko ya Misri,Tunisia Libya na nchi nyingin za kiarabu kwa kaisi kikubwa yalitokana na watu kulishana matango pori juu ya serikali zao na hiyo ilikuwa ni mikakati ya nnchi za ng'ambo kuziharibu nchi za kiarabu,atokeo yake watu wakaamini propaganda na kuamua kujiweka rehani kwa kitu ambacho hakina ukweli wowote ule,leo hii hata hawajielewi .

Leo hii walibya wanalia,wamisri wanalia,watunisia wanalia ,wamepoteza ndugu na jamaa zao kwa ujinga ,kwa kudanganywa na kuchonganishwa,

Kuhusu suala la mmiliki wa Jf kukamatwa na leo inasemekana atafikiswa mahakamani,nazani watanzania hapa hatuahitaji kuwa kama WEHU,tusio jua nini maana ya mahakama,maadamu imebainika kile kilichosababisha akakamatwa na kuzuiliwa ndani ,vema tukawa watulivu huku tukiacha mahakama kazi yake ,ndio tuanze kuja na hayo malalamiko yetu mara baada ya maamuzi kutoka kwani ukitazama sheria Mmiliki wa JF na polisi wote wako sawa katika madai yao.

Mwisho watanzania nchi hii ni yetu sote,hakuna mwenye kusema hii ni nchi yangu,kama umezaliwa tanzania mkono wako wa kulia unaalama ya ndui,ni wajibu wako kuilinda tanzania dhidi ya wanapropaganda wanaoishi kwa kueneza maneno ya ajabu ajabu juu ya Tanzania,maneno ambayo hayana hata tone la ukweli.

Tukikubali hali hii mwisho wa siku tutajikuta tunalia na kujutia,mifano ya misri,libya na tunusia sio ya kubeza,tunachotakiwa kuzingatia hapa tusikubali yaliyotokea huko yanatokea hata hapa kwetu,japo kweli kuna baadhi ya maeneo ambapo serikali haijafanya vema lakini subra na utulivu ulio na uvumilivu vibaki kuwa mioyoni mwetu, wenzetu wa Ghana walivumilia mwisho akafanya maamuzi ya kistarabu na maisha yanaendelea,so na sisi hatuna budi kufanya hivyo kama tu tumewachoka watawala hawa tulio nao.
Wenye mawazo kama yako ni wale waliovurugwa!!! Upofu wa mapenzi labda na maslahi yanakufanya usione "the sword of damocles which lingers on our heads"
 
Je na wewe hiyo ID yako siyo feki?
Nyani haoni kundule...
Sijui shule huwa mnaenda kusomea kukatika vigodoro!!?
Soma bandiko kwa umakini ili uelewe. Natumia fake ID na ndio maana sijawahi kuhoji Uhalali wa utendaji wa Rais. Tofauti na baadhi ya Wazandiki humu JF.
 
Ukisoma posts kwenye uzi huu utaona jinsi gani tunaendeshwa na mihemko!
 
Kwani mtu akianzisha habari hapa kwamba Dangote anahamishia kiwanda Kenya na wewe ukaamini, unafikiri ni nani anapaswa kuswekwa rumande? Kwa maoni yangu, ni wewe unayeamini vitu hovyo hovyo bila kuhoji. Jinga kabisa. Tena hustahili kuchangamana na jamii. Unapaswa kufungwa. Yaani mtu anakuambia lile likiwanda linahamishiwa Kenya na wewe unakubali tu kama zuzu. Na kwa taarifa yako, investors ni watu makini and very informed. Usifikiri wanayumbishwa kwa taarifa fake unazoweka hapa JF. Umeniuzi sana kwa sababu ni watu wenye mawazo kama yako mnaojenga hoja za kijinga mpaka Max yuko ndani sasa na hatima yake haifahamiki. Eti impacts kwa wawekezaji huko nje! Ndio ulichomwambia JPM na kufanya Max akamatwe? Mijitu mingine sijui kwanini imetokea kuwa sehemu ya jamii yetu. Nalaumu sana elimu yetu. Ndio imetupatia watu wa namna hii. We need to do something guys.
Mkuu...! Nimeiona hasira yako kwa Watanzania aina hii, nafikiri ni robo tu ya niliyo nayo mimi juu yao,sielewi ni kizazi cha aina gani hiki, mbaya zaidi hata wasomi kabisa kabisa kwa wingi tu na wao ni wa hivyo. Taifa linapotea mzee, tunahitaji solution ya haraka na endelevu. Thanks!
 
Mi nipo nje ya nchi siku nyingi. Ngoja nitafute maisha, nisubiri siku ya kiama changu
 
Miezi michache iliyopita rais Magufuli alisema anatamani malaika ashuke [sijui ashuke toka wapi] aje kuizima mitandao ya kijamii ambayo tumekuwa tukiitumia kupashana habari na kubadilishana maoni na mawazo kuhusu mambo mbalimbali.

Baadhi yetu tuliyachukulia maneno hayo kama ishara ya mambo yajayo kuhusu uminywaji wa hii mitandao na haki ya watu kuitumia kwa kujieleza, kutoa maoni, na kuikosoa serikali.

Sasa kitendo kilichotokea jana cha kukamatwa kwa Max kimethibitisha kuwa huu utawala wa Magufuli umeazimia kutuziba midomo kwa kutumia mabavu ya dola.

Kwa hilo mimi nataka huyo Magufuli ashindwe na alegee kabisa. Sitaki kabisa afanikiwe hata kidogo na watu wote wenye akili zao timamu hawana budi kumpinga na kuifanya hizo azma yake iwe muhali.

Kupinga udhalimu ni jambo la adhama. Na huyu mtu tayari keshaonyesha dalili zote za udikteta. Hivyo tumpinge kwa pumzi na nguvu zetu zote. Kwanza ni mtumishi wetu na si vinginevyo.

Hizi siyo zama za kupelekeshana kwa vitisho. Haogopwi mtu zama hizi.

Akichemka tutamkosoa tu. Akichapia Kiingereza tutamcheka tu. Kama hana ngozi nene ya kuweza kumudu na kuvumilia kuongelewa kwa namna yoyote ile basi aondoke. Aachie ngazi.

Mtu mwenyewe kwanza hafai kuwa rais. Hana haiba ya urais, hana hekima wala busara zinazotakiwa mtu wa kiwango cha rais kuwa nazo. Kila akifungua mdomo wake mtu unaanza kuombea asiongee maneno ya kuaibisha.

Sikuwahi hata siku moja kudhani kuna mtu angekuja kumpiku JK kwenye ubomu lakini ndani ya mwaka tu huyu jamaa keshamuacha mbali mno JK. Pata picha hiyo miaka minne iliyobaki hali itakuwaje.

Huyu mtu tumdindie. Tukinywea atavimba kichwa na kujiona ana nguvu nyingi ilhali hana. Hana nguvu za kuweza kuzidi nguvu ya umma.

Kwa hiyo mimi nataka ashindwe. Tena ashindwe vibaya. Je wewe mdau wasemaje?
Ushindwe na ulegee na ikurudie hiyo laana, Nyumbu mkubwa wewe
 
Mkuu,huyu kiongozi sio mbaya ila kuna vitu vichache anakosea kama binaadam kwa kuruhusu mihemko yake binafsi iliyopitiliza kwenye mambo ya msingi,anatakiwa ajicontrol sana kwani mara nyingi jambo hili humuaribia,abadilishe mindset yake juu ya wanaomkosoa,naamini kwa uchapakazi wake akisikiliza hoja zao na kupata ushauri wa watu wake wa karibu anaowaamini zaidi,anaweza kutoboa sana,kwani sio wote wanaokukosoa hawana hoja,akilitambua hilo atafanya mambo makubwa sana

Akizipanga vizuri karata zake,anaweza kuwa the best president ever happened in our country
Sio vichache anakosea hasa kutubagua watanzania WA ccm a Vyama vingine hili ni kosa namba moja analofanya....... Akiwa km raisi kila mkutano na matamko yake anaanza kuwasema wapinzani ili apigiwe makofi ndo anaendelea Sisi tunaJua yeye ndo kiongozi wa nji hii si wa ccm pekee. Hili kosa akiliacha nitaanza japo kusikiza matamko yake hayo
Sababu kwa sasa sisikilizi bora niangalie muvi za kina rufufu... Inanifanya NA mie ni mbague kuwa ccm wenyewe ndo wamsikilize raisi wao........ Mwambie nimesema
 
Staha ninini?
Niwekee Tafsida katika haya maneno ili nizingatie staha ya ushauri kwa Rais.

(KIVUKO CHA MV DAR KILICHOSIMAMIWA KIMUCHAKATO NA WAZIRI WA UJENZI DK.MAGUFURI NA AKAKIKAGUA KWENDA BAGAMOYO NA KUTANGAZA NI KIZURI SANA CHA KISASA NI KIBOVU)

(ZITO KABWE ASEMA NDEGE ZA MAGUFURI NI MTUMBA ZILIPAKWA RANGI)

(UUZWAJI NYUMBA ZA NHC ULIOSIMAMIWA CHINI YA WAZIRI MAGUFURI ULIJAA UTATA)

Nipe mfano staha ipi hapa nitumie?
Baada ya kuambiwa hutadakwa sasa umeota mapembe nakuongeza mkia sio!?
 
Nakubaliana na wewe,jk kamwacha mbali mapema sana,yani kafunika madhaifu yote ya jk saa hizi watu ni yeye na ukimwona mtu anamwongelea vizuri huyu basi ujue hamnazo kichwani mwake
 
Kaka unanfahamu vizuri Raisi wetu, wala usingeandika yote haya.

Atakuwa kasoma na kucheka tu na kuzidi kupanda bichwa la kujisemea na bado.

Uzidi kunwombea apambane na menginr, ya Max nayo imesikitisha wengi na mimi. Bali kuwa na business ya mitandao ni kazi sana na inachanga moto hizi nyingi.

Ila kuna sheria kweli Max amekiuka iliyopo au amechomekewa?
Haha hawezi kusoma NA kucheka bahati muzuri kagonga mwamba
 
Unadhani hata anapoua kama kule mto Ruvu anatoa taarifa,wewe ni kichaa kama yeye.
936eef7d143efe17bebdd4d77e3f057c.jpg
 
Kwani mtu ukitoa maoni yako pasipo kutoa matusi au ukianzisha uzi wenye uhalisia na usio wa kichochezi unakuwa na hofu ya nini?

Tatizo lililopo kuna baadhi yetu tumekuwa maarufu kutunga stori za uongo na kuzijengea hoja then tunataka jamii iamini kama ni kweli kumbe ni upotoshaji

Mtu kama umeanzisha mada yako na ushahidi unao kwa nini uogope? Endapo utahitajika polisi si unapeleka ushahidi?

Fikiria mtu anayeanzisha uzi hapa eti Dangote anahamishia kiwanda Kenya na hizo habari zinasambaa dunia nzima kumbe ni uonge pasipo kufikiria negative impacts kwa wawekezeji walioko huko nje. Mtu kama huyu leo hawezi fanywa kitu sababu tu anatumia ID feki sishangai kesho akaibuka na jambo jingine

Watu wa namna hii lazima washughulikiwe hakuna kulea ujinga. Watanzania tumekuwa maarufu sana wa kupika majungu

Ninakubaliana na wewe kabisa uhuru wa kutoa maoni lazima uheshimiwe na watawala kwani ni takwa la kikatiba lakini uhuru huo lazima uzingatie utu na nidhamu.

Leo mtu akimchukia mtu flani sababu za kiitikadi za vyama au jambo lolote, kesho anamtungia tuhuma na kusambaza kwenye mitandao. Vitu vya namna hiyo siyo vya kulea
HAYA UMESIKIKA KALALE SASA
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom