Nataka Rais Magufuli ashindwe

Nataka Rais Magufuli ashindwe

Status
Not open for further replies.
Ndio maana Nagufuli anaamua kuwabana watu wajinga kama ninyi sasa ishu ya viwanda hapa inatoka wapi? Mpinge Magufuli kwa hoja siyo unakuja hapa kwa vimaneno vyako vya jejeli alaf eti unasema ndio unakisoa
Kwani mtu akiongea anamzuia Mtukufu kufanya kazi!! Kwanini asitimize hizo ahadi zake ili kuwaprove wrong hao wakosoaji au wanao mtukana. Mbona Trump kapigwa na kila media kubwa nchini Marekani na Dunia nzima na bado kashinda uraisi!?
 
Mkuu huyo unaweza kuta ni mama wa watoto watano,mme wa mtu mmoja,vimichepuko serengeti sita,kadi ya lumumba na mkopo sugu usiolipika sacos yao huko lumumba ndio inabidi ajiwehushe kuposti ushuzi humu.
True ngoja nimuache. Inawezekana hata tv anaangalia TBC na Clouds tv.
 
Ni lini Mungu alihusika kwenye uchaguzi hapa nchini,acha uongo na usiwe unamhusisha Mungu kwenye vitu vya aina hii.
Alafu hii tabia na ujasiri wa watz kumtumia Mungu kujustfy upuuzi na wizi kwenye chaguzi sijui wana ipata wapi!?
au labda mimi ndio sielewi, labda wana mtaja huyo mungu wa Dar.
 
Alafu hii tabia na ujasiri wa watz kumtumia Mungu kujustfy upuuzi na wizi kwenye chaguzi sijui wana ipata wapi!?
au labda mimi ndio sielewi, labda wana mtaja huyo mungu wa Dar.
Wanajipendekeza tu mitandaoni waonwe.......wanamjua kweli Mungu au wanasikia tu neno Mungu
 
Usijidanganye kua Mungu hausiki kwa kuegemea kwenye ushabiki.
Labda huyu Mungu wa Dar. Mungu ni mtakatifu, mkamilifu na ukamilifu wake hauna mipaka, Acheni kumuhusisha Mungu kwenye mambo ya kijinga bana. Kwa mfano unataka kutuambia Jeicha alitokewa na malaika na akaamua kufuta uchaguzi kule Zenji!?
 
Thinking outside the box.
Aliyeandika uzi huu ana lengo baya na jamii forums.
Hajauleta kwa bahati mbaya.
Hata wanaochangia kwa matusi bila staha nao ni hivyo hivyo.
Justification inatafutwa.
Very unusual watu kukosa woga na adabu kiwango hiki.
Hivi ukikosoa jambo tendo hili linakuwa tusi? Kumbe ndiyo mana mawaziri wamekuwa wakiitika "ndiyo mzee" hata kama kwa jambo lisilowezekana wanaogopa jamaa asiwamafuru. Hebu nikukumbushe unakumbuka mjadala wa tozo la VAT kwenye miamala ya benki kuna viongozi walijitoa ufahamu kwa kuogopa kwenda kinyume na mfalme. Matokeo yake nafikiri unayajua, ukienda kwenye Atm unachapwa kiboko kilekile
 
Miezi michache iliyopita rais Magufuli alisema anatamani malaika ashuke [sijui ashuke toka wapi] aje kuizima mitandao ya kijamii ambayo tumekuwa tukiitumia kupashana habari na kubadilishana maoni na mawazo kuhusu mambo mbalimbali.

Baadhi yetu tuliyachukulia maneno hayo kama ishara ya mambo yajayo kuhusu uminywaji wa hii mitandao na haki ya watu kuitumia kwa kujieleza, kutoa maoni, na kuikosoa serikali.

Sasa kitendo kilichotokea jana cha kukamatwa kwa Max kimethibitisha kuwa huu utawala wa Magufuli umeazimia kutuziba midomo kwa kutumia mabavu ya dola.

Kwa hilo mimi nataka huyo Magufuli ashindwe na alegee kabisa. Sitaki kabisa afanikiwe hata kidogo na watu wote wenye akili zao timamu hawana budi kumpinga na kuifanya hizo azma yake iwe muhali.

Kupinga udhalimu ni jambo la adhama. Na huyu mtu tayari keshaonyesha dalili zote za udikteta. Hivyo tumpinge kwa pumzi na nguvu zetu zote. Kwanza ni mtumishi wetu na si vinginevyo.

Hizi siyo zama za kupelekeshana kwa vitisho. Haogopwi mtu zama hizi.

Akichemka tutamkosoa tu. Akichapia Kiingereza tutamcheka tu. Kama hana ngozi nene ya kuweza kumudu na kuvumilia kuongelewa kwa namna yoyote ile basi aondoke. Aachie ngazi.

Mtu mwenyewe kwanza hafai kuwa rais. Hana haiba ya urais, hana hekima wala busara zinazotakiwa mtu wa kiwango cha rais kuwa nazo. Kila akifungua mdomo wake mtu unaanza kuombea asiongee maneno ya kuaibisha.

Sikuwahi hata siku moja kudhani kuna mtu angekuja kumpiku JK kwenye ubomu lakini ndani ya mwaka tu huyu jamaa keshamuacha mbali mno JK. Pata picha hiyo miaka minne iliyobaki hali itakuwaje.

Huyu mtu tumdindie. Tukinywea atavimba kichwa na kujiona ana nguvu nyingi ilhali hana. Hana nguvu za kuweza kuzidi nguvu ya umma.

Kwa hiyo mimi nataka ashindwe. Tena ashindwe vibaya. Je wewe mdau wasemaje?
Naona umejilipua mkuu
 
UNAPEPO NA NINAONA PEPO WENGINE 106 WAME LIKE
 
Hivi ukikosoa jambo tendo hili linakuwa tusi? Kumbe ndiyo mana mawaziri wamekuwa wakiitika "ndiyo mzee" hata kama kwa jambo lisilowezekana wanaogopa jamaa asiwamafuru. Hebu nikukumbushe unakumbuka mjadala wa tozo la VAT kwenye miamala ya benki kuna viongozi walijitoa ufahamu kwa kuogopa kwenda kinyume na mfalme. Matokeo yake nafikiri unayajua, ukienda kwenye Atm unachapwa kiboko kilekile
Mimi najiuliza tu, hivi watu wanaenda makanisani na misikitini kumuabudu Mungu yupi ambaye anataka watu wake waseme ndio kwenye sio na sio kwenye ndio?
 
Wewe Gamba unaongea ujinga gani!! Ulishawahi kuona wapi au lini mtu ameikosoa serikali ya US au kumtukana Obama akafuatiliwa na CIA, FBI au Polisi wa US!? Wewe kwa hizo akili zako za zilizo fungwa na CCm unadhani viongozi wa US wana muda wa kufuatilia illusion and rumors kwenye mitandao!?
Una uhakika gani na unalolisema wewe gamba original
 
Naomba Waheshimiwa wasijue nimeisoma hii Post
 
Safi sana. Umeongea sawa kabisa.
Kuna wenzetu wanaogopa viwanda vyao vya kufyatua uongo vitafilisika. Shame on them

Kwani mtu ukitoa maoni yako pasipo kutoa matusi au ukianzisha uzi wenye uhalisia na usio wa kichochezi unakuwa na hofu ya nini?
Tatizo lililopo kuna baadhi yetu tumekuwa maarufu kutunga stori za uongo na kuzijengea hoja then tunataka jamii iamini kama ni kweli kumbe ni upotoshaji

Mtu kama umeanzisha mada yako na ushahidi unao kwa nini uogope? Endapo utahitajika polisi si unapeleka ushahidi?

Fikiria mtu anayeanzisha uzi hapa eti Dangote anahamishia kiwanda Kenya na hizo habari zinasambaa dunia nzima kumbe ni uonge pasipo kufikiria negative impacts kwa wawekezeji walioko huko nje. Mtu kama huyu leo hawezi fanywa kitu sababu tu anatumia ID feki sishangai kesho akaibuka na jambo jingine

Watu wa namna hii lazima washughulikiwe hakuna kulea ujinga. Watanzania tumekuwa maarufu sana wa kupika majungu

Ninakubaliana na wewe kabisa uhuru wa kutoa maoni lazima uheshimiwe na watawala kwani ni takwa la kikatiba lakini uhuru huo lazima uzingatie utu na nidhamu.

Leo mtu akimchukia mtu flani sababu za kiitikadi za vyama au jambo lolote, kesho anamtungia tuhuma na kusambaza kwenye mitandao. Vitu vya namna hiyo siyo vya kulea
 
Lakini Ngabu si majuzi juzi tu ulikuwa unawazodoa waliokuwa wanalia juu ya rafu zinazochezwa na awamu ya tano?

Kwani wewe ulidhani ni masihara?

Well kuna watu wanaamini siasa si muhimu kwa mustakabali wa nchi au maisha yao, lakini ukweli ni kuwa siasa kama ilivyo pesa ni mchezo muhimu na wa hatari sana kwa wanaocheza na wasiocheza.
 
Nyani ngabu katukosea sana watanzania. Katukashfia Rais wetu

"Mtu mwenyewe kwanza hafai kuwa rais. Hana haiba ya urais, hana hekima wala busara zinazotakiwa mtu wa kiwango cha rais kuwa nazo. Kila akifungua mdomo wake mtu unaanza kuombea asiongee maneno ya kuaibisha"

Daa we jamaa ni noma...hadi nmeogopa kwenye hiyo paragraph
 
Mtu umekula makukuru(aina ya makande) ganda la maharagwe limebaki kwenye meno kinywani hukujiangalia kwenye kioo ukotoka mbele ya wenzako mnapiga stori kwa kuwa wewe hupendi kukosolewa wenzako wanakuaacha lakini ujue umeaibika na pia wamekujua wewe umekula nini huku ukitamba umekula nyama, lakini kama wewe ni muungwana watakuambia utoe hilo ganda.
Sasa Rais wetu na jeshi la polisi kuweni makini kwani kumsemwa kiongozi yeyote ni vema kwake kutambua na kijirekebisha pale anapoona amekosea kwa kuwa hakuna binadamu aliyekamili kwa 100%.
Pia inaonekana Rais wetu sio mvumilivu na kukosa uvumilivu kunapungaza sifa ya kuwa kiongozi.
 
mitandao ya kijamii pamoja na kupashana, kuelimishana na kuburudishana, inatumika kuondoa mihemuko. ni relief valve. utapoteza muda na raslimali kupambana na kundi hili la mwisho bila mafanikio kama hutafanikiwa kujua chanzo kikuu cha mihemko yao.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom