Nataka Rais Magufuli ashindwe

Nataka Rais Magufuli ashindwe

Status
Not open for further replies.
Kakaa sisi tukae kimya tu.
Tumuache Mungu afanye kazi yake. Mkono wa Mungu utainuka siku moja na siku ukiinuka ........sina mengi.
 
Huyu rais nilidhani angekuwa wa maana kumbe bora mpenda safari Kikwete. Huu udikteta angeupeleka kwenye mambo ya msingi angefanya la maana sana. Seems hana shughuli anazi create kama Mjinga mjinga yule taahira Paul Makonda
hapana mkuu jk alikuwa mbovu na historia ilisha andikwa, huyu naye ndo anaandika ya kwake. Nadhani sasa mtnaanza kumwelewa aliye sema dikteta uchwara. kule us trump kagomewa na wafanya kazi wa kampuni za mawasiliano kumpa taarifa za kidini!!!!..........
 
JF ni Jukwaa linalofuatiliwa sana na viongozi.
Inasemekana baada ya viongozi kutoa matamko yao, huja huku haraka kuangalia maoni ya vijana.
Wanakuja huku kwa kuwa waliopo huku wanajielewa.

Vita dhidi ya JF ni vita dhidi ya wanao jielewaa.

Ila wakumbuke kuwa JF haijawahi kushindwa na haitoshindwaa!!
[HASHTAG]#GREATJF[/HASHTAG]
kwi kwi kwi kwo kwo nimejikuta kwenye hali ndani ya mwendo kasi jamaa wananiangalia huyu anacheka nini.
 
Kwani mtu ukitoa maoni yako pasipo kutoa matusi au ukianzisha uzi wenye uhalisia na usio wa kichochezi unakuwa na hofu ya nini?

Tatizo lililopo kuna baadhi yetu tumekuwa maarufu kutunga stori za uongo na kuzijengea hoja then tunataka jamii iamini kama ni kweli kumbe ni upotoshaji

Mtu kama umeanzisha mada yako na ushahidi unao kwa nini uogope? Endapo utahitajika polisi si unapeleka ushahidi?

Fikiria mtu anayeanzisha uzi hapa eti Dangote anahamishia kiwanda Kenya na hizo habari zinasambaa dunia nzima kumbe ni uonge pasipo kufikiria negative impacts kwa wawekezeji walioko huko nje. Mtu kama huyu leo hawezi fanywa kitu sababu tu anatumia ID feki sishangai kesho akaibuka na jambo jingine

Watu wa namna hii lazima washughulikiwe hakuna kulea ujinga. Watanzania tumekuwa maarufu sana wa kupika majungu

Ninakubaliana na wewe kabisa uhuru wa kutoa maoni lazima uheshimiwe na watawala kwani ni takwa la kikatiba lakini uhuru huo lazima uzingatie utu na nidhamu.

Leo mtu akimchukia mtu flani sababu za kiitikadi za vyama au jambo lolote, kesho anamtungia tuhuma na kusambaza kwenye mitandao. Vitu vya namna hiyo siyo vya kulea
ndugu usujidanganye kuwa ukitoa taarifa za ukweli ndo utakuwa salama!. determinant ya usalama wako ni yule anaye athirika na taarifa yako, kama ana nguvu za kukuadhibu atakuadhibu pamoja na ukweli wako wa wazi! kumbuka kupekuliwa kwa kubenea na kumwagiwa tindikali zikitafutwa zinazo daiwa kuwa nyaraka za serikali zinazo husu kagoda, richmond na EPA. Kwa kifupi wistle blowers hawako salama kama taarifa zao zina waumiza wenye mamlaka!.
 
Wewe unasema unaomba ashindwe wakati ameshindwa tayari kauli zake tu zinaonyesha hana nia njema na taifa hata hili la kukamata watu anaoona wanakosoa serikali yake bado ni kushindwa zaidi tabia ya kiongozi mwoga inadhihirisha kushindwa kwa mtu
 
Miezi michache iliyopita rais Magufuli alisema anatamani malaika ashuke [sijui ashuke toka wapi] aje kuizima mitandao ya kijamii ambayo tumekuwa tukiitumia kupashana habari na kubadilishana maoni na mawazo kuhusu mambo mbalimbali.

Baadhi yetu tuliyachukulia maneno hayo kama ishara ya mambo yajayo kuhusu uminywaji wa hii mitandao na haki ya watu kuitumia kwa kujieleza, kutoa maoni, na kuikosoa serikali.

Sasa kitendo kilichotokea jana cha kukamatwa kwa Max kimethibitisha kuwa huu utawala wa Magufuli umeazimia kutuziba midomo kwa kutumia mabavu ya dola.

Kwa hilo mimi nataka huyo Magufuli ashindwe na alegee kabisa. Sitaki kabisa afanikiwe hata kidogo na watu wote wenye akili zao timamu hawana budi kumpinga na kuifanya hizo azma yake iwe muhali.

Kupinga udhalimu ni jambo la adhama. Na huyu mtu tayari keshaonyesha dalili zote za udikteta. Hivyo tumpinge kwa pumzi na nguvu zetu zote. Kwanza ni mtumishi wetu na si vinginevyo.

Hizi siyo zama za kupelekeshana kwa vitisho. Haogopwi mtu zama hizi.

Akichemka tutamkosoa tu. Akichapia Kiingereza tutamcheka tu. Kama hana ngozi nene ya kuweza kumudu na kuvumilia kuongelewa kwa namna yoyote ile basi aondoke. Aachie ngazi.

Mtu mwenyewe kwanza hafai kuwa rais. Hana haiba ya urais, hana hekima wala busara zinazotakiwa mtu wa kiwango cha rais kuwa nazo. Kila akifungua mdomo wake mtu unaanza kuombea asiongee maneno ya kuaibisha.

Sikuwahi hata siku moja kudhani kuna mtu angekuja kumpiku JK kwenye ubomu lakini ndani ya mwaka tu huyu jamaa keshamuacha mbali mno JK. Pata picha hiyo miaka minne iliyobaki hali itakuwaje.

Huyu mtu tumdindie. Tukinywea atavimba kichwa na kujiona ana nguvu nyingi ilhali hana. Hana nguvu za kuweza kuzidi nguvu ya umma.

Kwa hiyo mimi nataka ashindwe. Tena ashindwe vibaya. Je wewe mdau wasemaje?
ndugu yangu unapotamka mh. rais ni dikteta lazima ujue maana ya dikteta and features of dictator but also how dictator come into power?sasa sio unaongea vitu kwa sababu umemsikia Lissu au Lema kaongea so nawe unalopoka tuu ili uonekane ila kabka hujaongea pima impacts ya kauli yako kwako binafsi,,familia yako na jamii itayosikia au soma maneno yako,,kubwa hacheni watu wafanye kazi ili nchi iende mbele,,Rwanda wananchi walipiga kelele kibao while Kagame came into power but leo wako wapi?sasa Rwanda wanatuzidi nini kwa utajiri wa mali asili?hacheni maneno ya uchonganishi na kipumbavu hayo
 
Ha ha ha ha... na hayo ndo mawazo yenu bavicha. yaani inch iingie kwenye shida ili uchaguzi ujao washinde wao!. Haya si mawazo ya kizalendo, watu wa namna hii hata tukipigana vita wanaweza kumsapoti adui ili tupigwe wapate cha kusema kwenye uchaguzi.

Mungu ni mwema, hawezi kuyapa nafasi mawazo haya yatokee. Maana anasisitiza mpende adui yako, waombeeni wanaowatesa. Kumwombea mabaya hamtafanikiwa.

Sasa wewe unadhani kuna haja gani ya kumsaidia vita mtu ambaye hana umuhimu wowote kwenye maisha yangu....sana sana anafanya maisha yangu yanakuwa magumu...ni kweli Kabisa nitaungana na adui yake ili tumshinde na kumvurumishia mbali..
 
ndugu yangu unapotamka mh. rais ni dikteta lazima ujue maana ya dikteta and features of dictator but also how dictator come into power?
Kwani Hitler aliingiaje madarakani kama siyo kwa kuchaguliwa kwa kupigiwa kura? Udikteta siyo jinsi unavyoingia madarakani bali jinsi unavyoishi ukiwa madarakani!!
 
Kwani mtu ukitoa maoni yako pasipo kutoa matusi au ukianzisha uzi wenye uhalisia na usio wa kichochezi unakuwa na hofu ya nini?

Tatizo lililopo kuna baadhi yetu tumekuwa maarufu kutunga stori za uongo na kuzijengea hoja then tunataka jamii iamini kama ni kweli kumbe ni upotoshaji

Mtu kama umeanzisha mada yako na ushahidi unao kwa nini uogope? Endapo utahitajika polisi si unapeleka ushahidi?

Fikiria mtu anayeanzisha uzi hapa eti Dangote anahamishia kiwanda Kenya na hizo habari zinasambaa dunia nzima kumbe ni uonge pasipo kufikiria negative impacts kwa wawekezeji walioko huko nje. Mtu kama huyu leo hawezi fanywa kitu sababu tu anatumia ID feki sishangai kesho akaibuka na jambo jingine

Watu wa namna hii lazima washughulikiwe hakuna kulea ujinga. Watanzania tumekuwa maarufu sana wa kupika majungu

Ninakubaliana na wewe kabisa uhuru wa kutoa maoni lazima uheshimiwe na watawala kwani ni takwa la kikatiba lakini uhuru huo lazima uzingatie utu na nidhamu.

Leo mtu akimchukia mtu flani sababu za kiitikadi za vyama au jambo lolote, kesho anamtungia tuhuma na kusambaza kwenye mitandao. Vitu vya namna hiyo siyo vya kulea

mtoa maada hawawezi mkamata maana ananguvu ya kupambaana kisheria. polisi wkijua mnyonge watakumliza huku wanakungalia usoni
 
Kwani Hitler aliingiaje madarakani kama siyo kwa kuchaguliwa kwa kupigiwa kura? Udikteta siyo jinsi unavyoingia madarakani bali jinsi unavyoishi ukiwa madarakani!!

Lumumba buku saba walishalishwa kasa kuwa ili uitwe dictator lazima uingie madarakani kwa kupindua serikali Mkuu..
 
Mungu atawalaani wale wote wanaokandamiza haki za msingi za kujieleza!
 
Miezi michache iliyopita rais Magufuli alisema anatamani malaika ashuke [sijui ashuke toka wapi] aje kuizima mitandao ya kijamii ambayo tumekuwa tukiitumia kupaana habari na kubadilishana maoni na mawazo kuhusu mambo mbalimbali.

Baadhi yetu tuliyachukulia maneno hayo kama ishara ya mambo yajayo kuhusu uminywaji wa hii mitandao na haki ya watu kuitumia kwa kujieleza, kutoa maoni, na kuikosoa serikali.

Sasa kitendo kilichotokea jana cha kukamatwa kwa Max kimethibitisha kuwa huu utawala wa Magufuli umeazimia kutuziba midomo kwa kutumia mabavu ya dola.

Kwa hilo mimi nataka huyo Magufuli ashindwe na alegee kabisa. Sitaki kabisa afanikiwe hata kidogo na watu wote wenye akili zao timamu hawana budi kumpinga na kuifanya hizo azma yake iwe muhali.

Kupinga udhalimu ni jambo la adhama. Na huyu mtu tayari keshaonyesha dalili zote za udikteta. Hivyo tumpinge kwa pumzi na nguvu zetu zote. Kwanza ni mtumishi wetu na si vinginevyo.

Hizi siyo zama za kupelekeshana kwa vitisho. Haogopwi mtu zama hizi.

Akichemka tutamkosoa tu. Akichapia Kiingereza tutamcheka tu. Kama hana ngozi nene ya kuweza kumudu na kuvumilia kuongelewa kwa namna yoyote ile basi aondoke. Aachie ngazi.

Mtu mwenyewe kwanza hafai kuwa rais. Hana haiba ya urais, hana hekima wala busara zinazotakiwa mtu wa kiwango cha rais kuwa nazo. Kila akifungua mdomo wake mtu unaanza kuombea asiongee maneno ya kuaibisha.

Sikuwahi hata siku moja kudhani kuna mtu angekuja kumpiku JK kwenye ubomu lakini ndani ya mwaka tu huyu jamaa keshamuacha mbali mno JK. Pata picha hiyo miaka minne iliyobaki hali itakuwaje.

Huyu mtu tumdindie. Tukinywea atavimba kichwa na kujiona ana nguvu nyingi ilhali hana. Hana nguvu za kuweza kuzidi nguvu ya umma.

Kwa hiyo mimi nataka ashindwe. Tena ashindwe vibaya. Je wewe mdau wasemaje?
Kwa nini usimdindie wewe mmeo na watoto wako nyumbani kwako mpaka utuhusishe sisi. Chuki binafsi ni matapishi tu unayotuletea hapa. Hatuna muda nazo. Kama umeshindwa maisha hapa duniani kwa nini usijaribu ahera !
 
h
Huyu rais nilidhani angekuwa wa maana kumbe bora mpenda safari Kikwete. Huu udikteta angeupeleka kwenye mambo ya msingi angefanya la maana sana. Seems hana shughuli anazi create kama Mjinga mjinga yule taahira Paul Makonda
hajiamini kwa kila anachokifanya shindwe na kulegea
 
Mungu atawalaani wale wote wanaokandamiza haki za msingi za kujieleza! Mwenyezi mungu pia ataiangusha serikali dhalimu inayoongozwa na kiongozi dhalimu anayejivika utukufu!
Haya madua ya kuku nadhani. Yatawarudia mwenyewe. Serikali ni mimi na wewe! Sasa kama Mungu akiiangusha unadhani wewe na mimi tutaponea wapi. Kamanda jitambue
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom